Jamani wanawake hapana aisee, kweli unaambiwa duniani hapa usimuamini mtu bali MUNGU wako pekee nashangaa miye siwezi hata kidogo yani mwanamke mzima unamla shemeji yo inahusu jamani unajuwa kabisa yule mwanamke wa dada yako na wamezaa halafu wewe unajipitisha unajitongozesha mpaka unaliwa, utakuwa unagundu wewe ndio maana huna wa kwako mpaka umchukuwe wa mwenzako kama unajiona mzuri si ungepata wako wa nini wa mwenzio haipendezi.
Mwanamke kujiamini bwana sio unakazi na kukaa kwako unajiita unajiamini huku unakula mume au mwanaume wa mtu kujiamini ufanye vyote hivyo na uwe na wako wa kukuweka ndani ndio tutakuona kweli wewe mwanamke, mwanamke kudandia wa watu hukujuzwa wewe kujitunza na kutafuta wako..LAKO HILO kama linakuhusu.
Kuna rafiki yangu kila mara penzi lake linatingishwa kila tukilifanya jioni lazima alisikie kwa baba mtoto wake, katika urafiki wetu pia yupo mdogo wake mtoto wa mama yake mdogo kumbe yule shoga siku nyingi alikuwa anamtamani shemeji yake anammezea mate!!!! mwanamke kila kimuona kijana chini kashaloa, akawa anatafuta sababu ya kumuharibia ndugu yake ili ampate yeye, ndio visa vikaanza kila atakalotuhadithia rafiki yake jioni lazima alikute kwa baba mtoto wake mazuri hayapelekwi mabaya tu ndio shoga anamfikishia shemeji yake..
Wanaume mwanamke bwana kama wewe unamuona wa nini kuna mwenzio anawaza atampata lini sasa jishauwe kujiona wewe ndio wewe utaisoma junejuly, basi kunakipindi dada wa watu kapendwa na mkaka mmoja mwenye hela zake za kutoa shoo (nadhani mnajuwa kutoa shoo ni nini) kamuita siku hiyo akamwambia tukutane bar fulani njoo na rafiki zako ukitaka, shoga dada yako nami nikabebwa hao safari tukambeba na yule mdogo wake sasa..kumbe ndio alipojichinja
Shoga siye tumeenda tumekunywaaaaaaa,tumekulaaaaa yule kaka sianamtaka shoga yangu kakaa naye karibu wanaongea na yule kaka alikuwa na marafiki zake wawili lakini sio wa kwetu ni kuchangamsha kijiwe tu, basi mida ikafika tukaondoka shoga tulivyoondoka tu akamfikishia shemeji yake mkanda mzima na yule baba mtoto wake alibyokuwa hana uvumilivu akampigia mwanamke wake na kugombana na vituko vyengine vingi tu yule dada mpaka akalipata lake nakuanza kuliwa na shemeji yake sasa.
Mapenzi yakanoga, yule ndugu mtu anakaa kwetu mabibo, shoga yangu anakaa sinza madukani na baba mtoto wake anakaa ubungo, sijui alichomfanyia nini mpaka ndugu mtu akamuamishia yule bwana mabibo na wakaendeleza mapenzi mpaka akabeba mimba!!!!!!!! sawa umeamua kumlia dada yake bwanaake na mimba ndio ukajibebeshe inahusu!!!!
Shoga ndio baadaye anakuja kumwambia ndugu yake kwamba yeye mke mwenziye na anamimba ya baba mtoto wake, yule rafiki yangu ndio kuchanganyikiwa na kuanza kutukanana na kupigana na ndugu yake basi shoga yangu mpaka leo kachanganyikiwa anajifungia tu ndani hataki kutoka nje yaani amechanganyikiwa tumeshaongea naye kwamba unapodondoka kwenye maisha unakikung'uta vumbi na kuendelea na masiha lakini huyu naona kama ngumu kuelewa bado naona anataka kujipa moyo labda yule baba mtoto wake atarudi kama zamani na wakati kule kwa mdogo wake pia mapenzi motomoto.
Ndugu na ukoo wamemtenga yule ndugu mtu kwa kosa alilomfanyia mwenziye..je kama ni wewe ndio umetendwa ungefanyaje? na unamshauri nini huyu dada maana hajiwezi kabisa..
No comments:
Post a Comment