SIKU ambayo mwanamke Sitabai Chouhan alipolazwa katika Hospitali ya Maharaja Yashwant Raoin huko Indore, India, kwa jaribio la kutaka kujiua kwa kunywa sumu ya panya, ndiyo siku manesi walipogundua kwamba mwanamke huyo alikuwa amefungwa kufuli dogo kwenye mlango wa sehemu zake za siri.
Mume wake aitwaye Sohanial Chouhan (38) alifikishwa polisi baada ya kugundua kwamba alikuwa ana tabia ya kumfunga kufuli mkewe sehemu hizo kwa muda wa miaka minne kwa madai kwamba asingefanya hivyo angekuwa anatembea nje ya ndoa.
Imegundulika kwamba Chouhan alianza kumwenyesha mkewe madawa ya kulevya na kisha akatumia sindano kutoboa matundu sehemu zote mbili za mlango wa uke wa Sitabai kisha akaweka kufuli dogo ambalo alilifunga kila asubuhi akienda kazini, na kulifungua wakati anaporejea.
Katika uchunguzi huo, polisi waligundua ufunguo huo ukiwa umefichwa kwenye soksi zake.
Kisa cha mama huyo kujaribu kujiua kwa sumu ni pale alipogundua kwamba mumewe alikuwa anamtongoza binti yake wa kwanza ili afanye naye mapenzi.
Mwanamme huyo ambaye ni makenika na aliyemwoa mkewe akiwa na umri wa miaka 16 na sasa wakiwa na watoto watano, alifunguliwa mashitaka ya kudhuru mwili.
Source: Global Publishers
No comments:
Post a Comment