Friday, September 28, 2012

Ulijuwa Kama...

Hehe heiya chezea waswahili weye..

Ulikuwa unajuwa kama mtoto akivimbiwa dawa yake nini?

Shoga kama hukujuwa ngoja nikujuze, kwetu mabibo wanasema mtoto akivimbiwa unamlaza kitandani unachukuwa mkaa unausaga chini halafu unachukuwa yale masizi unamchora kwenye tumbo..sio kumpaka unamchora kama niishara ya msalaba ama kuchora kitu gani unajuwa wewe, baada ya muda ile hali ya kuvimbiwa inaisha kabisa..

Hehe heiya chezea kungwi wewe, njoo mwenyewe ujione siku hiyo 21/10/2012 uyaone ya dunia na uyasikie mengi ambayo ulikuwa huyajui, wewe niendee hewani 0717 019320 kwa malipo shoga nikupe dira na kadi yako..

Shoga usimuache wifio maana wale nao vidonge vyao vipo pale, japo wengine wanajifanya wa sikuhizi hawana roho mbaya shoga ndani ya moyo wa mtu huujui kumbe linamsaga na kumsigida wivu juu yako..Inahusu 

Anakwambia Sakina wa lioka unampandisha unamshusha Unamtupa huko kwenye dustbin

Chezea ndoa wewe..

1 comment:

  1. habari da Rose! asante kwa posts zako huwa kila siku nakatiza hapa japo huwa sicoment kutokana na muda ila naipenda sn hii blog. naomba kama unaweza utuweke hapa habari ya kwenye gazeti la ijumaa jana kuhusu Jacklin Wolper kumwaga siri za mchumba wake,na kuhusu yaleo kwenye gazet la sani,kama hutajari lakini maana wewe ni mama wa mihangaiko na majukumu hujabweteka.

    ReplyDelete