Friday, September 7, 2012

TUNU'S KNIGHT...

 Cousin yangu Tunu anatarajiwa kuolewa MUNGU akipenda jumamosi, kwahiyo jana tulikuwa kwenye sendoff yake..na mimi nikiwa katibu wa kamati hiyo

Hapa bidada akiwa salon pale sinza legho, upande wa geti la nyuma la rombo green view jamani wanahuduma nzuri hata mimi nilitengeneza hapo nywele zangu kwanzia retouching mpaka kusukia weave niliwapenda kwakweli

Tunu akiwa tayari kupakwa makeup..dada yako yule nashonewa pale kwa nyuma kama unaona..


UUiii alipendezaje sasa Tunu jamani, niliipenda sana hiyo nguo yake..


Hapa ukumbi ulikuwa Zonghwa i hope nimeandika vizuri, kwakweli walipamba vizuri ila walichoniboa mimi ni hiyo red carpet hebu ona ilivyopauka na hata haijanyooka..jamani haya ilimradi siye tulimaliza salama


Mwanamke akikata keki..akimaanisha anawakatakata magume gume yote ya mjini yatakayojitokeza ama ambayo yapo yanayotaka muharibia ndoa yake..Inahusu hujafundwa wewe ukapata wako ndugu wameshushwa kwa vitabu mchaguwe unayemtaka sio kuganda wa watu..hehe heiya lako hilo kama linakuhusu


Hapa akimkabidhi mama yake keki na kumshukuru kwa kumlea mpaka amefikia hapo sasa anamuaga na kumwambia yupo tayari kwenda kulea mtoto wa mwanamke mwenziye..mmhhh nitasutwa miye


Mwanamke kusutwa sunna..hehe heiya hapo sasa akitoa utambulisho wa ndugu na jamaa zake..chezeya mwalimu wewe..lazima upite hapo


Hapo sasa kitambaa cheupe kikapigwa tukaserebuuuuukkkaaaaa



Hawa ni wadogo zangu, huyu wa kulia ananifwata mara mbili wakushoto anamfwata wa kulia..umeona tulivyofanana macho..hapana chezea totoz za kichagga...


Hii nguo jamani ilinitia aibu mwenzenu isinikatikie sasa kwenye heka heka ya kukata viuno kwenye tarabu hapo ikabidi niifunge tu ilimradi shughuli iishe ndio maana unaiona inapinda pinda kama inadegedege..haituliii inayumba tu mara ipande mara ifunguke..aghhhh


Wapi mama Tunu..



Namtafuta wangu miye..


Hehe heiya chezea mtoto ya Tanga wewe hakunaga mazawadi makubwa hapa mahaba tu..kijana alikuwa anapuliziwa perfume akale hapo..


Twende mume wangu mtarajiwa...


Hehe heiya wapi Isha Mashauzi unaambiwa kila mtu na mtuwe....



Jamani mume wangu nitakulisha vinono milele


Ahsante mke wangu


Na mimi nitakupa vinono milele..hehe heiya


Chezea siye..utuache bibi miaka 100000000000000

No comments:

Post a Comment