Wednesday, September 19, 2012

Tahadhari na Choo..

Kuna jambo leo nimejifunza nikaona sio mbaya kama nitawajuza na nyie, labda kuna wengine walikuwa wanalifahamu na wengine hawakujuwa basi wapate kujuwa.

Mara nyingi tumesikia watu wanadondoka chooni, na wengi hupoteza maisha  je ikikutokea wewe labda nduguyo na mtu wa karibu sana kwako amedondoka chooni na kupoteza fahamu unajuwa utafanyaje, nimeambiwa kwamba haswa wenye vyoo vile vya kizamani ambayo ndani kwasababu ya maji huwa panaota utandu utandu na mara nyingi huwa wakijani, nasikia utaukwaruza kama unaukomba ule utando kwa mkono na kumpaka mtu aliyedondoka hapohapo chooni kabla hujamtoa..

Sasa najiuliza kwa siku hizi vyoo vilivyo vyakisasa yani unaingia nyumba ya mtu choo mpaka unaweza kula humohumo bila kinyaa sasa akidondoka mtu atafanywaje?? ama vyoo vya uswahilini ndio watu wanalogana na kuangushana vyooni tu...mhhhh

Haya

No comments:

Post a Comment