Wednesday, September 26, 2012

Makubwa haya...

TANGU Waziri wa Haki wa Swaziland, Ndumiso Mamba, anaswe kitandani anavunja amri ya sita na mke wa Mfalme wa nchi hiyo, Makhosetive Dlamini ‘Mfalme Mswati III’, hali ni mbaya kwa wake wa kiongozi huyo.
Mamba, alinaswa kwenye kitanda cha mke wa 13 wa mfalme huyo, Nothando Dube na tangu wakati huo, walinzi wa Mfalme Mswati, wamepewa madaraka makubwa ikiwemo kuwacharaza bakora hata barabarani na mbele za watu.

Inaelezwa kwamba wake wa Mfalme Mswati wanafungiwa ndani kama kuku, inapotokea wanakwenda sehemu wanakuwa chini ya ulinzi mkali.

Ripoti zinasema kuwa endapo barabarani mke wa mfalme atachepuka kwenda hata msalani bila taarifa au atasalimiana na mtu ambaye walinzi wanamjua, hata kama ni ndugu yake, mwanamke husika hucharazwa bakora kama ng’ombe.
“Ukiwa mke wa Mfalme Mswati ni mateso makubwa. Unavyoishi haina tofauti na ng’ombe anavyochungwa. Ukiwa unatembea barabarani unatakiwa ufuate uelekeo anaotaka bodigadi, ukikosea kidogo unachapwa bakora na vIrungu.

 “Mambo yalikuwa mabaya lakini sasa ni mabaya mno. Kwa sasa nataka kutoka lakini mfalme hataki kuruhusu niondoke. Nipo kama mfungwa, saa 24 nachungwa, sina uhuru hata kidogo,” alisema Nothando.

Mwanaharakati wa demokrasia anayepingana na mtindo wa maisha ya Mfalme Mswati, Lucky Lukhele, aliwahi kuwaambia waandishi wa habari kwamba siyo Nothando tu, wake wake wote wa kiongozi huyo wanaishi katika mazingira magumu afadhali ya wafungwa.

“Kuna mke mmoja wa mfalme alikutwa getini na walinzi, tena getini kwenyewe kwa ndani halafu geti lilikuwa limefungwa na funguo wanazo walinzi. Ajabu ni kwamba walinzi walipomkuta pale hawakuuliza mara mbili, walimpiga na kumuumiza mno,” alisema Lukhele bila kutaja jina la mke huyo wa mfalme.

Kwa upande mwingine, inaelezwa kuwa mtindo wa mai
sha ya Mfalme Mswati na wakeze, umesababisha mpaka sasa akimbiwe na wanawake watatu.

Mke wa sita wa mfalme huyo, Angela “LaGija” Dlamini, ndiye anatajwa kuwa mwanamke wa hivi karibuni zaidi kuondoka katika himaya ya mfalme huyo.
Mke wa 12 wa mfalme, Inkhosikati LaDube, alitimuliwa Desemba mwaka jana kwa kile kilichobainishwa kwamba aligombana na bodigadi wake.

Taasisi ya Swaziland Solidarity Network ilieleza kwamba Dlamini, alikimbia makazi ya mfalme baada ya kuwa kwenye mateso kwa miaka kadhaa.

Dlamini, aliaga anakwenda kuwasalimia wazazi wake kwenye Mji wa Hhohho, lakini aliporuhusiwa alitimka jumla.

Mfalme Mswati pamoja na tabia ya kupenda kuoa mabikra, vilevile anatuhumiwa kujilimbikizia utajiri wa kutisha, hivi karibuni Jarida la Forbes lilimtaja kwamba anamiliki utajiri wenye thamani ya zaidi ya dola milioni 200 (shilingi bilioni 300).

Source: Global Publishers

No comments:

Post a Comment