Tuesday, September 11, 2012

Heka Heka za Mtaa...

Jamani mimi kunajambo limetokea nimeshindwa kabisa kuelewa hii dunia inaenda wapi sasa hivi, mtaani kuna mama mmoja anawatoto wawili wa kwanza anamiaka kumi na tatu na wapili saba, ni mama tu mwenye biashara yake ya mama lishe na hana mume inaelekea watoto wake hawa aliwazaa tu bila ndoa.

Huyu mama anadada yake mmoja anakaa mwanza, ambaye ndugu na ukoo mzima wanamsema yule mama kuwa mchawi na mshirikina sana, hata ndugu hawaendi kabisa kumtembelea japo anahela sana, sasa kunakipindi cha bomoabomoa huyu mama lishe banda lake likabomolewa akawa anamaisha magumu sana na mpaka ikafika akawa anaombaomba kwa majirani apate pa kula na watoto.

Mambo yalivyozidi kuwa magumu akaona kuliko kufa njaa na watoto hawasomi ngoja tu ampeleke mtoto wake mmoja kwa dada yake mwanza, yule mtoto akaenda huko mwanza, mtoto alikuwa anaongea vizuri na mzima kama watoto wa miaka saba walivyo basi ameenda ana miezi mitano yule dada yake akampigia simu huyu mama na kumwambia mtoto anaumwa sana, wanahangaika aweze kutibiwa, mara baada ya wiki akampigia simu kumwambia mtoto haongei amekuwa bubu!!!!!!!!mama mtu akalia wee lakini akasema cha muhimu mwanangu hajambo basi hamna shida.

Baada ya wiki yule mtoto akazidiwa sana ikabidi dada mtu amlete dar mama yake ahangaike naye wakati anajuwa kabisa yule mama huwezo ana, basi yule mama kuhanmgaika huku na kule bahati nzuri watu waliokuwa wanamjuwa mtaani wakamwambia kaombe msaada alipoweza kumpeleka hospital aliambiwa kwamba mtoto anamatatizo ya moyo kama anaweza ampeleke India.

Yule mama kumbukeni hajiwezi jamani sijui alifanya nini mara akampeleka mtoto wake hospital yaani hapo ndipo unapojuwa uchungu wa mama kwa mwanaye, kwenda India yule mtoto akachekiwa akaambiwa hana matatizo yoyote kwenye moyo wake, yule mama akawaambia nimeambiwa anamatatizo ya moyo lakini madaktari wakamwambia hamna kitu mama rudi tu nyumbani haya ni mambo ya kifamilia mama

Basi yule mama akarudi na mwanaye lakini mtoto bado alikuwa anaumwa, rafiki yake mmoja akamwambia waende kwa waganga wakanza sasa kusaka waganga wazuri wa mjini kila mganga alipoenda walimwambia dada yako ndio amemfanya hivi mwanao!!!!!! waganga kama wa tatu anasema wamempa jibu moja..

Baada ya wiki mbili nyengine yule mtoto alifariki, wamemzika juzi tu yani majirani wanavyosema yule mama kama alichanganyikiwa alilia na kumsema dada yake kwenye msiba na kwavile ndugu wanamjuwa yule dada hawakushangaa bali walilia tu na yule mama, cha kushangaza yule dada mtu hakuja kwenye msiba jana siku mbili baada ya yule mtoto kufariki akasafiri kwenda africa kusini.

Yule mama alikuwa analia anasema bora angemtoa mwanaye sadaka ajuwe anaendesha magari na kuishi maisha ya furaha na majumba tele kuliko mwanaye kutolewa kafara maisha mazuri anayomwengine yeye anataabika!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Nasikia na ndio maana yule dada hakuudhuria mazishi angepatwa na balaa kama ni kweli amemtoa kafara yule mtoto kama mama na ndugu wanavyosema.


1 comment:

  1. Mbona hayo yapo sana tu! Utajiri huu kwakweli kila mtu ana source yake alikoupatia ila utajiri wa kishirikina ni mbaya sana maana ni lazima makafara ya damu yawepo. Huko kwa Mungu tutajibu mengi sana!Poor innocent baby may her soul rest in peace.

    ReplyDelete