Jamani leo nataka kuongea na wamama haswa wale wenye watoto wa kike, hivi mama unapobeba mimba na kujuwa kama unamtoto wa kike ama baada tu ya kujifungua ukaambiwa hongera unamtoto wa kike hivi nini kinakuja katika akili yako????
Nkumbuka mimi wakati nimebeba mimba na nikaambiwa nina mtoto wa kike nilifurahi sana na wakati wote tokea nimelifahamu hilo nilimuomba sana MUNGU kwanza akizaliwa afanane na mimi halafu pili nikamuomba aniwezeshe katika malezi yake na mpaka sasa bado namuombea mwanangu awe na akili darasani, asiwe na kiburi, aheshimu wa kubwa na wadogo na pia najitahidi kumfundisha kazi ndogo ndogo kama mwanamke na kumfundisha kuvaa vyema na kukaa vyema.
Utamkuta mtoto wa kike msichana mkubwa kakaa mguu mmoja huku mwengine kule na kavaa sketi au gauni kweli hii ni nini?? kuna kipindi nilipataga msichana wa kazi mpaka nikasikia kuchanganyikiwa yani ikifika asubuhi niamke wa kwanza kama mchawi nikamuangalie chumbani nimuamshe maana hata kuamka mapema kwake ilikuwa tabu, na kulala je ndio balaa analala na kanga moja sasa utamkuta kazunguka kama pia miguu mwaa kama anataka kuzaa ama anasubiri kuchumwa tunda!!!eboo huyu mtoto nikasema asije niletea balaa miye akiamua kuvua nguo sasa hata siku moja hafungi mlango anavua kila kitu mlango ukiwa wazi akia nani sitakaa kusahau.
kwavile chumbani kwake ndio tulikuwa tunaweka stand ya viatu na nguo safi kabla sijaziweka kwenye makabati basi mume wangu akiwa anawahi kuondoka siku hiyo na shosti kule ndio dalili ya kuamka hana inabidi tena ndio ukajifanye sweety leo nakuchagulia uvae viatu hivi mpenzi usiende kuchagua mwenyewe vaa hivi kila ukiviona unikumbuke, basi kijana atachukuwa kwa mapenzi tele na kuvaa..mbona dada nilifukuza baada ya wiki nataka balaa za baba mwenye nyumba na house girl mimi mana nimeshasikia wamama wengi sana wakilia hiki kilio.
Kuna mama mmoja mtaani kwetu anamtoto mkubwa tu wakike, inaelekea yule mama mimba ya huyu mtoto ilikuwa ni wakati anajiuza akiwa msichana, siye kwetu uswahilini nyumba zimebanana ukikohoa tu jirani yako lazima asikie, sasa basi kila mwanaye akimuomba hela yule mama humwambia ushakuwa mkubwa hakuna hela ya bure kwani wanaume barabarani huwaoni mwenzio nilipokuwa kama wewe nilikuwa na mihela kibao kwasababu nilikuwa najuwa kutumia usichana wangu wala sikumuomba mama yangu na wewe tumia usichana wako!!!!
Kweli hayo ni maneno ya kumwambia mwanao?? basi yule dada kweli kama umalaya akauanza kweli mpaka sasa kapata mimba akiwa nyumbani (historia imejirudia kama mama yake) basi yupo tu analea mimba inamiezi mitano na umalaya hajaacha kila kukicha na mwanaume mpya na mbaya zaidi anawaleta humo humo nyumbani kwao na mama yake hasemi chochote.
Mimi hii imeniuma yani kila nikiwaangalia wanangu namuomba tu MUNGU anipe rehema na malezi mema juu yao.
No comments:
Post a Comment