Friday, July 6, 2012

SOMO...

Kama hataki nipe miye, kama kasusa nipe miye,Kama hataki nipe miye, Kasusa nipe miye  soda ya kopo...............Piga bastola...toooosshhhhhh...

Ndugu yangu hayo siyo maneno yangu, hayo maneno ya Mfalme mzee yusuph, maneno kuntu hayo, maneno mazito yanahitaji uyafungie kibwaya hayo sijui kama utakuwa umenielewa..

Somo leo nataka liwaendee wake wote, wake wale halali waliofunga ndoa kama kanisani, kama msikitini kama bomani lakini wake halali siwabagui wale wakuja tukae tuendeleze maisha mmhh hata miye wangu namba moja waliovalishwa pete mkono wa kushoto kidole cha pili sehemu hizo nilizotaja hapo juu..

Wake sikuhizi mmekuwa na kijitabia fulani nimeshasikia wengi wakiongelea na kujisifia, utamkuta mtu kagombana na mumewe ili kumkomoa unamnyima unyumba, heeeee shosti inahusu nini sasa, utamkuta mtu wiki nzima kalala kaa mninga, utazani umebebwa msukule hugeuki kitandani tena ndio unageukia ukuta kabisa hugeuki upande wa pili mpaka asubuhi, kama mtoto wa watu kabanwa pumzi ghafla kafa utamla nyama kisa unasusa, inahusu?

Wake siku hizi ndugu zangu dunia ishaharibika, unaambiwa mapenzi ya kugandana kama ruba hamna ukimyima akitoka nje akipiga hatua mbili tu anarusha wanawake kumi roho, akigusa mmoja hapigi kapigiwa upo hapo? sasa wewe jitie unanuna wenzio wakusaidie, unategemea yeye shida zake atamalizia wapi na akirudi nyumbani sura umeikunja huna hata nuru loohhh..badilika

Mwanaume kama mtoto wako wewe ndiye unayemlea hakushindi kitu mtafutie adhabu nyengine ili ajuwe kitu fulani hupendi kama ukiongea naye hakuelewi lakini sio kumnyima haki yake..maana ingekuwa haki yako kilichokufanya ukaolewe naye nini kwani kwenu ulikuwa huli, huvai, hunapakulala?????????????

Ndoa nyingi zinaingiliwa na mapepo ya kutoka nje kwasababu ya vitu tu vidogo kama hivi, ni heri atoke kwa tamaa zake mwenyewe lakini sio wewe kushindwa kumuhudumia ni aibu..hukufundwa wewe???

Jirekebishe..

No comments:

Post a Comment