Jamani mwanamke kusutwa sunna, lakini hapana nimeshindwa kuvumilia, hivi sisi wanawake mwanaume anawezaje kukuchanganya kama tui na maziwa inahusu????
Mtaani kwetu kuna jamaa mmoja anatarajia na yeye kuuaga ukapera mwezi wa tisa anamuoa mwanamke ambaye ni jirani yake, maandalizi na vikao vyote vimeshaanza, mara tukasikia kwamba mtaa wa pili kuna mwanamke anamimba ya huyuhuyu kijana tena jamani!!!!!!!
Shosti bi harusi habari hizo hana, maana tumeamua kumpeleka kinondoni mwezi kwenda kufundwa, huyu mwanamke wa mtaa wa pili naye analeta kizaa kutaka kuharibu ndoa kwamba haolewi mtu hapa yeye si anajifanya spoku kutoboatoboa kila mahala ataisoma sasa..mmhhhhh
Miye shoga nipo upande wa huyu bi harusi maana ni mdogo wa rafiki yangu, na yeye pia ni mjamzito miezi sita na shosti kule miezi mitano umeiona shughuli hapo!!!!!! sasa jamaa kuona bomu karibia linataka kumlipukia juzi kampigia mfunda wa huyu bi harusi mtarajiwa kwamba anamtaka mchumba wake akamnunulie vitu vya harisi kumbe kambeba huyu bi harusi mtarajiwa mguu kwa mguu mpaka msikitini kufunga ndoa ya kimya kimya!!!! kabeba dada yake mmoja na dada upande wa biharusi haoooooooo
Mtaani si ikavuja jana kama jamaa kaoa, watu wakataka warudishiwe hela zao za michango, maana kama keshaoa shughuli tena ya nini weee uwaone sasa waswahili na maneno, mama wee nadhani mtakuwa mmepata picha, basi bwana harusi ikabidi awaambie kwamba alienda kumslimisha biharusi kutoka ukristu kwenda uisilamu, kwamba ndoa bado mpaka hiyo mwezi wa tisa!!!!!!!
Basi tena ndio waswahili kutulia, turudi kwenye somo langu bibi chonde chonde usione ushapata mwanaume kaja kwako anajifanya mpole anataka kukuoa shoga chunguza kwanza, siku hizi magube gube kibao kukuoa atakuoa lakini hekaheka zitakurusha rohoo usikae na amani kwenye ndoa, na ogopa sana wanaume wapole wanaotembea vichwa chini yani ukimuona yule bwanaharausi miye mwenyewe sikudhani kama na yeye anahekaheka zote hizo.
Namuombea tu kwa Mungu kweli hiyo ndoa ya bomani ifungwe huo mwezi wa tisa, yule shosti wa mtaa wa pili asije kuvuruga maana bidada tokea avalishwe pete ya uchumba mbona tunayakoma mashauzi yake, na ndio maana tumeamua kumpelekwa akafundwe mwezi maana asijekututia aibu baada ya ndoa maana hakuna kuachika hapa wala hakuna kumpa huyo shiti wa mtaa wa pili muda wa kuharibu ndoa...heheh heya
No comments:
Post a Comment