Thursday, July 12, 2012



Dada Rose,

Hivi wanaume wengine walizaliwa na wadudu au wanyama gani? Kweli mwanaume uliyezaliwa na mwanamke unawezaje kufanya ukatili kiasi hiki kwa mwanamke tena mke wako aliyekuzalia watoto wa 4 m tired of hearing these things ooh lord save us now enough is enough.. 

Kuna madada amefariki leo inauma sana tena alikuwa mrembo mno eti alimfumania mme wake na mwanamke and so akaamua kuachana nae na kwenda mahakamani kwa taratibu zingine ss mwanaume akawa anamfata fata kubembeleza wap cku hy alimkuta anatembea wakati ye anadrive prado akamwomba aingie ndani waongee lakini yule dada akakataa na kuendelea kutembea alichofanya shetani huyo alimgonga mke wake na kumburuza mita kadhaa nyama yote ya mgongo na sikio liling'oka amelazwa miezi 6 akiwa hajitambui mpaka amekufa.

ulaaniwe popote ulipo we mwanaume nani atalea watoto wako na we uko bize na umalaya wako? Yaan nina hasira sana.

Tully

No comments:

Post a Comment