Monday, June 11, 2012

Tamaa yangu imekuwa Balaa langu..

Binadamu wote hutamani siku moja kuoa na kuolewa, huwa kila mmoja hujikuta siku moja unatamani na kupanga kwamba siku hiyo nataka iwe hivi, niifanyie hapa, mapambo na chakula kiwe vile, nguo nataka ya rangi hii na iwe vile yani tunaitamani nakutaka yote mazuri yawepo.

LAKINI JE...huyo unayetaka akuoe ama unayemuoa je unauhakika kwamba ni chaguo lako, ni kweli hata kama mmekuwa wachumba miaka zaidi ya mitano ni kweli huyo ndio mume/mke unayemtaka ama mnaoana kimazoea kwamba kwasababu tumeshakuwa pamoja miaka mingi basi muoane, ama ndio zile tunajionea tu uvivu kuanza relationship mpya tunagandana na hawa tulio nao tukizani MUNGU ndiye mume/mke aliyenipa?

Naomba mumshauri huyu kaka jamani maana anamawazo sana, ameshauriwa na bado anahisi hajui la kufanya yani amechanganyikiwa...

SIKIA HII.. 

Kuna couple moja ninayoifahamu wamekuwa kwenye uhusiano miaka mitano sasa, huyu dada ni rafiki yangu sana, kama relationships nyingine zote raha na matatizo ni moja ya viunganishi vya mapenzi, wawili hawa hawakuwahi kukaa pamoja, mwanaume alikuwa amepanga kwake na mwanamke alikuwa anaishi kwa wazazi wake.

Baada ya miaka mitano ya uhusiano wao wakaamua sasa ni wakati waoane waanzishe familia yao, kwakuwa walikuwa wanajuana sasa vya kutosha, maandalizi yakaanza kijana akapeleka barua ya uchumba, baadaye akajibiwa akalipa mahari na akamvalisha bibie pete ya uchumba kila mtu atambuwe kama amechukuliwa na harusi yao kupangwa kufanyika 21/7/2012.

Vikao vimeanza pande zote mbili, mashamsham yanazidi kuendelea, sasa wiki moja iliyopita huyu kaka alitoka kwenye mihangaiko yake (akiwa na mdogo wake kwenye gari) na kuamua kumpitia mchumba wake nyumbani kwao amjulie hali kama anavyofanyaga then arudi nyumbani, lakini alipofika akaambiwa shosti hayupo ametoka na sio kawaida yake huwa kila akitoka lazima amuarifu mchumba wake na kumwambia atarudi saa ngapi.

Wakati anarudi kwenye gari mara nje gari ya mchumba wake ikawa ndio ina park alikuwa na dada yake, sasa akawa anamuuliza umeenda wapi bila kuniaga na sio kawaida yako, yule dada akamwambia alikuwa tu katoka na ndugu yake, huyu kaka akamwambia mbona nilikuwa nakupigia hupokei, yule dada akamwambia hakuwa naziona hizo calls zake yule kaka kwa hasira akamwambia hebu lete simu yako nihakikishe kabla yule dada kumpa yule kaka akawa ameshampokonya ile simu.

Kuangalia calls akaona kweli zipo missed calls zake, akaenda moja kwa moja kwenye inbox looohh bora angeacha ile simu akakuta message ya mwanaume ikimuelekeza katika hotel aliyokuwepo na kumuhimiza afanye haraka amemmiss sana, yule mwanaume hasira zilimpanda na kumkunja yule dada kama anataka kumpiga lakini wale wengine walio kuwa nao wakamuamuru asimpige halafu nje ya geti la nyumbani kwao haitakuwa vyema, akamuachia yule dada eti akamuwasha kibao mchumba wake na kuingia ndani na kuwaacha wale pale nje.

Kesho yake yule kaka alimpigia simu shosti siku nzima hakupokea, kesho yake pia siku nzima hakupokea akaamua sasa kwenda kwao kumuuliza vipi kwa nini hapokei maana aliyetakiwa kukasirika ni yeye aliyeona msg ile kwenye simu ya mchumba wake, alipofika nyumbani akaambiwa dada hayupo wakati gari yake ilikuwepo, akampigia pale hakupokea, na mpaka ninavyoandika hii story hawajaonana tena na wala yule dada hapokei simu ya mtu yeyote hata mimi nimempigia hapokei anachokijuwa mwanaume ni kwamba aliitwa jumapili hii ya jana na kuambiwa shosti amevunja uchumba hataki tena kuolewa.

Yule kaka ananiambia alitaka kufa, kwa nini wazazi wanasema hajatoa sababu ila hataki tu kuolewa tumeonega naye tumemshauri lakini amekataa kuolewa kwahiyo kijana tumekuita tu ukasimamishe vikao vyako vya harusi, kwa uchungu wazazi walimwambia kijana na kuahidi kwenda kwa wazazi wenzao upande wa mwanaume kuomba msamaha.

Kila mtu kachanganyikiwa, upande wa bwana harusi michango ilishakusanywa million 16 ukumbi, mapambo, keki, chakula na vinywaji vilishalipiwa leo unaanzaje kurudisha michango ya watu..upande wa bibi harusi hivyohivyo pia kila kiru karibia kilisha lipiwa yani kila upande wamechanganyikiwa shosti kagoma kuolewa na sababu hajatoa na hataki kuongelea hilo swala tena na mtu yoyote.

Habari ndio hio, watu wanaloga kupata ndoa, wengine wanapata wanatupa huko kwenye dustbin






7 comments:

  1. Kwa kweli namhurumia kaka wa watu na alimpenda kweli bado amekuta vithibitisho vyote lakini siku ya pili akaendelea kupiga simu. Nampa pole sana kwa gharama alizotumia na maandalizi aliyofanya. Halikuwa chaguo sahihi kutoka kwa Mungu inawezekana ameepushwa jambo kubwa ambalo lingemtokea baadae. Aliye wake atakuja na wataoana kwa mapenzi ya dhati. Huyo dada kweli ni fisadi wa mapenzi kwanini kumtenda mwenzake hivyo? Mkataa pema pabaya panamwita..... kilio na sononeko la huyo kaka halitapita bure.

    ReplyDelete
  2. Pole yake huyo kaka. Kwa sasa ni ngumu sana kujua Mungu amemweupushia nini ila avute moyo konde. Kuhusu mandalizi, mi naona watu waje kama kawaida wale wanywe na kuondoka zao mana kila kitu kimeshalipiwa. Mwambie huyo kaka atafute mwakilishi kwenye familia ambaye atasimama siku hiyo na kueleza watu kilichotokea. Tunambiwa tumshukuru Mungu kwa kila jambo.

    Huyo dada wala asimlazimishe. Ashukuru kamkataa sahizi kuliko angeenda kumkatalia kanisani.This is not the end of the world. Atapata mwingine na akumbuke sana kumshilikisha Mungu katika kila jambo atakalolifanya.

    ReplyDelete
  3. hii nikama movie vile duh!kuna mambo duniani pole kaka mwenye hili tatizo mimi ushauri wangu ni kwamba kwanza be strong haya yote ni majaribu na majaribu tumeumbiwa ss wanadamu na siyo wewe peke yako mwenye matatizo japo matatizo hutofautiana sana kakak unajua everything happens for the a rison sasa usipata frustration kaa chini na kupiga magoti umwombe Mungu wako sana akuongoze na hili na akufungulie njia maana uko ktk kipindi kigumu sana mimi sijuii huyu mchumba wako amepatwa nanini mpaka akubali kubadilika gafla tena dakika za majeruhi hatujui kilicho msibu ingekuwa kunauwezekano na yeye ajieleze shida gani au tatizo gani ameona au kusikia kutoka kwako tungeelewa anewe mimi sasa nakushauri kutoka moyoni kaka kama unarafiki mwengin wa pembeni mshaushi haraka sana azibe hilo pengo mfunge hiyo arusi wanawake ni wengi tu wanatafuta kuolewa labda huyu dadahakuwa chaguo lako huwezi jua Mungu amekuepusha kwa nini tafuta mwingine haraka sana utapata mzuri zaidi yake maana anataka uwaibike lakini Mungu atakupigania usiabike huyu dada anaroho ngumu sana kumchanganya mwezie kiasi hichi lakini malipo ni hapahapa kama amedanganyika amepata ambaye anamwona zaidi dada hii blog pls fuatilia hii ishu urudi kutuabarisha sisi mafans wako kinachoendelea kwa kwa pande zote kijana msichana maana hii ni movie tosha asnte kwakutuletea hichi kisa

    ReplyDelete
  4. huyo dada atavuna alichopanda kaka muombe sana mungu akusaidie kusahau ili uendelee na mambo yako km kawaida!

    ReplyDelete
  5. Anonymous 2, nimependa ushauri wako wa kumwambia huyu muhusika amuombe Mungu ili amsaidie. Ni kweli Mungu ni mwema na anampenda sana huyu kaka ivo asikate tamaa na aendelee kumuomba kwani yeye husikia sala zetu.

    Ila mi sikubaliani na wewe unapomwambia kama ana mtu mwingine wa pembeni amchukue. Mambo kama haya yakitokea ni lazima mtu kujipa break kidogo mana anaweza ingia pengine pabaya.Anaweza pata mke wa voda fasta lkn moto wake ukaja kuwa mkubwa kupita huu wa sasa so ni bora ajipe nafasi na kuendelea kumuomba Mungu. Mungu wetu ni mwema na husikia sala zetu.

    ReplyDelete
  6. Mimi naomba niwape ushauri. Mimi si mtu wa sala sana ila mama yangu ni mcha Mungu sana. Wakati nakaribia kuolewa mama alifunga novena akanambia mwanangu binadamu si wema. Unaweza shangaa kanisani mume hatokei. Wakati mwingine usipommshirikisha Mungu kipindi kama hicho wanga wengi. Ni wangapi wangependa kuolewa au watoto wao waolewe na bado hawajapata? Miji hapa kuna mchanganyiko wa watu tusowajua.

    ReplyDelete
  7. Nimependa ushauri wako, Mungu akishirikishwa ukweli hujitenga na uongo, au unaweza kuta ni mpango wa Mungu waoane ila Shetani kapitia katikati yao. God is first.
    Izoo, wa East Zu, Dodoma.

    ReplyDelete