Jamani mimi nakaa mabibo yani uswahili wote ndio pale vituko haviishi siunaelewa tena watu wengi wakiwa kwenye sehemu ndogo halafu makabila ya kipwani lakini i just love staying there maana kila habari ikitoka mtaani lazima niitwe nipewe na miye tena ndio lazima niirushe humu kwa raha zangu niwape funzo nyie ndugu zangu maana ndoa haina ubabe kwamba wewe unajulikana kwa minguvu basi utaiweza..
Sikia Hii....
Gume gume la leo ni dada mtu, yani kuna familia moja inawadada watatu, huyu dada mkubwa akapata bwana mapenzi motomoto ennnhe kila kona wapo wote kila mtu alikuwa anawajuwa, sasa bwana siunaelewa siku hizi uhusiano mmoja lakini pembeni kunamatawi kaa kumi?????? sasa katika yale matawe ya shosti ya pembeni kukawa kunajamaa mmoja balaa, siunaelewa pesa sabuni ya roho hakusita kumuhudumia mtoto mpaka akamfungulia na duka la kuuza maua (haya ya kukausha tunayopamba sana majumbani) ambalo lilikuwa linfanya vizuri tu na gari rav 4 milango mitatu basi wee huku kwa mpenzie anamuona wa nini tena. mwanaume hela unatoa elfu kumi sijui hamsini wakati mwenzio anatoa ya haja..akatupwa huko kwenye dustbin .
Kimbembe kilianza pale shosti alipogundua ana mimba, sasa hajui ya nani maana anakula huku na huku lakini kwa vile kidumu kilikuwa na hela sana na kinajimudu kubeba lita nyingi ya maji (mtoaji sana) baaaaaaasii shosti akambebesha ujauzito kwamba ana mimba yake basi kijana kwa vile hakuwahi kuwa na mtoto yaani shosti alihudumiwaje? alipataje miraha? lakini majirani walimuonea sana huruma yule mpenzi wake(ambaye tunakaa naye mabibo sasa) kijana mapenzi ndio hapewi tena yani kweli kuusaidiwa kunauma..
Yule shosti sasa ndio wakati huo kwa vile anajiamini ana mimba na ndio kashampa baba mimba yake, basi akamwambia yule mpenzi wake ukweli kwamba anamimba na ni yayule kaka na kwamba mapenzi yao yaishe asije kumuharibia kwa baba mtoto, zaidi ya kuchanganyikiwa kama anasaidiwa na mimba juu!!!! akawa kama haamini bado akawa anaendelea kumfwata yule shosti basi akienda pale kwao yule dada hataki hata kumuona tena na kuondoka akawa anaondoka, ama akiwepo anajifungia chumbani hataki kabisa kuwa naye.
Sasa vile yule kaka alivyokuwa anaumia mdogo wa shosti akawa anambembeleza na kutoka naye outings kumliwaza!!!!!!!mara jamaa kulipiza kisasi akaanza kula mdogo mtu!!!!! ndani ya miezi mitatu kaoa!!!!! yani alitaka alipize kisasi mpaka shosti aumie kama alivyoumia yeye.
Sasa shosti naye akawa kama haamini maana jamaa hakutaka vikao wala nini akalipa mahari na ndoa, ilikuwa siyo ya kifahari lakini ilifungwa sasa baada ya kuoa vituko balaa madada wakawa hawaongei tena kisa kamchukulia mpenzi wake yani ni vita vya hali ya juu mpaka vikao vinataka kukalishwa, shosti anamwambia jamaa ile mimba yake ila hakutaka kumwambia maana hakuwa na uhakika kama ataikubali????????(tamaa za hela zimemponza) basi wadada wanatukanana kutaka kutoana roho mtaani matusi makubwa makubwa mpaka kuandika hapa naogopa.
Huyu dada vipi jama kila mtu mtaani anamshangaa na sio kwamba kile kidumu chake hakimtaki bado anaendelea naye ila hasira yake ni kwanini jamaa amuoe mdogo wake? na kwanini mdogo wake akubali wakati anajuwa jamaa alikuwa shemeji yake? Huyu vipi jama...
Wenzako wanasema hivi: Wewe ukimuona wa nini wenzio wanauliza watampata lini
Wonders shall never end yooo!sasa nahapo asali sana iyo mimba iwe ni ya huyo jamaa anayemuhudumia. Kutokana na story yako huyu dada hana uhakika who is a real biological father. Embu ifuatilie tujue mwisho wake. Dah!maisha haya mmhhh!
ReplyDelete