Tuesday, May 8, 2012

Yalaaaaah....

Dada Rose nimeona umeandika mada moja ya kuhusu mganga hapo imenikuna na kufundisha nimeamua na mimi nitoe hii hoja yangu iwe fundisho kwa wenzangu wengine wote kwamba mtu anayeweza kukusaidia katika shida zako ni MUNGU tu na sio mganga kwani wengi ni uongo mtupu.

Mimi nimeolewa na nina watoto wa tatu mume wangu hapa katikati amekuwa na matatizo kweli yani kama kaota mabawa hakamatiki nyumbani haonekaniki hata wiki moja nzima, na hela haachi ya matumizi, kwenye kuchuma matunda ndio hata miezi mitano tunakaa bila kugusana na hivi tunavyolala mzungu wa nne ndio balaa kabisa.

Basi rafiki yangu mmoja akanishauri twende kwa mganga mbagala, kwamba huyo mganga ni mzuri na wengi sana amewasaida basi na miye kuona hivyo nikamwambia jumamosi twende basi jumamosi hiyo tukaongozana mguu kwa mguu, kufika kwa mganga nikamueleza yote akaniambia tuondoke halafu kesho saa tano usiku nirudi peke yangu basi bila kipingamizi tukaondoka.

Kesho yake kama nilivyoambiwa nikaenda hiyo saa tano usiku mganga akawaaga wake zake wawili kwamba anaenda kunifanyia tiba, tukaongozana na mganga usiku huo akanipeleka mpaka kwenye njia panda moja akaniambia niiname kama nasali basi nikafanya hivyo akaongea maneno yake baadaye akaniruhusu kuamka na tukaendelea tena na safari mpaka tukakuta njia panda ya pili napo akaniambia nifanye kama nilivyofanya pale mwanzo nami nikatii.

Tukaondoka hapo giza linazidi kutanda, tukafika sehemu moja hivi ambapo karibu na makaburi akatoa kitambaa na kukitandika na kuniambia nivue nguo nilale anichanje dawa, ili nikirudi nyumbani nikikutana na mume wangu hatakaa tena kutoka nje basi nikatii nikavua nguo zangu zote mganga akanichanja chini ya maziwa, juu ya tumbo, na nyuma ya kiuno nilisikia maumivu lakini sikuwa na lakufanya ila kilichonifanya niogope ni hiki....

Akaniambia wakati nimelala nitanue miguu aniwekee dawa ukeni, nikajuwa labda ni ya kupaka sijui alinisokomeza nini huku ndani yani nilisikia maumivu akaniambia tu nivumilie lakini ili dawa ifike mbali ilibidi aingize uume wake kuisokomeza maana ilimume wangu akiingia asijuwe kama kuna kitu basi nikamuacha mganga akaiingiza dawa, alipomaliza akaniambia tayari nenda lakini kesho lazima utanitafuta.

Basi nikasubiri pakakucha nikaondoka kwenda nyumbani nikaenda kuoga na kulala lakini nilipoamka kunajambo lilinitokea nikataka kulia yani nilishikwa na hamu sana yakufanya mapenzi yani sana hata nilikuwa tayari kufanya na mwanaume yeyote vile maana mume wangu hakuwa amerudi nyumbani basi ile hamu ikanichanganya nikajikuta nakata kiuno mwenyewe chumbani hamu ikanibana mpaka nikachukuwa simu na kumpigia mganga, akaniambia nilijuwa utanitafuta basi njoo nikutoe hiyo hamu kama mumeo hayupo.

Nikaanza kuchanganyikiwa kwa mawazo sasa nimefanya hivi kwa ajili ya mume wangu hajarudi sasa mganga akaniingie tena kwa mara ya pili basi mimi huku hamu ikiwa bado inanichanganya nikajikuta napijishika ukeni ili kuitoa ile hamu maana sikuwa na mtu wa kunitoa mara nikasikia kizunguzungu na kudondoka.

Nilipoamka nikajikuta hospitalini, kwamba mdogo wangu alinikuta nikiwa nimezimia na kunipeleka hospital nikatundukiwa dripu na kupuumzika baadaye niliporudi nyumbani nikawaadithia yaliyotokea, namshukuru MUNGU sikurudi tena kwa mganga na wala sijaisikia tena ile hali ya kutamani kuingiliwa ukeni mpaka sasa.

Ushauri tu kwa mtu yeyote awe wa kike ama wakiume hawa waganga wanatudanganya sio wa kweli jamani hakuna penzi la kuloga linalodumu ni heri ukamuacha tu mtu kama atakupenda akupende jinsi ulivyo hata kama mumeo anamatatizo ni heri ukaachana naye kuliko kujikita kwa waganga.

2 comments:

  1. Pole sana na yaliyokukuta. Wapendwa "GOD IS NOT A MAN". Hata siku moja hatuwezi mfananisha MUNGU na binadamu. MUNGU wetu yupo jana leo na kesho. Hakuna na haijawahi tokea MUNGU mwingine aliye mkuu zaidi yake. MUNGU wetu ni mwema na ana upendo kupita kiasi, yaani upendo wake haupimiki hata kidogo.

    Mungu aliyekubariki akakupa mume na watoto, huyo ndo tegemeo lako. MUNGU pekee ndie anayekupa pumzi na ndie aliyekulinda siku zote hizi pamoja na matatizo yako ya ndoa. Embu tazama jinsi anavyukupenda, amekubariki na akakupa watoto na anaendelea walinda mpaka leo hii. Kama nilivyosema upendo wake hauna kipimo. Kweli Mungu anakupenda na inakubudi umuombe msamaha mana ndo huyohuyo aliyekuokoa, badala ya kurudi kwa mganga ili kupunguza haja zako ulizimia na kupelekwa hospitali. Mshukuru sana Mungu wako na tena katoe sadaka.

    Amri ya MUNGU inasema ivi"Ndimi bwana Mungu wako usiabudi miungu mingine". Waganga wote hapa duniani ni waongo. Mganga yeyote yule unayemfahamu ni muongo.Nasema ivi kwa sababu hamna mganga anayeweza kujiganga. Kwa ufupi ni matapeli. Hamna mganga anayeweza kukupa uhai, furaha,upendo na amani katika maisha yako. Ni Mungu tu ndo anayeweza fanya hivi vyote. Mganga anakufa lakini MUNGU hafi. MUNGU wetu ni yuleyule jana leo na kesho.

    Tatizo letu sisi binadamu tunapenda vitu vya haraka sana. Mtu unaomba na unataka majibu yaonekane hapohapo. Waganga ndo hapo wanapowakamata hasa mtu unapotaka shortcut. Kwa MUNGU hamna shortcut. Enbu kaa na tafakari ni mambo mangapi ambayo umefanya na mengine ukijua kuwa hayampendezi Mungu lakini yeye anakuvumilia tu, tena ndo kwanza anazidi kukupenda na kukupa uhai ili uweze tunza familia yako.

    Hapa duniani hamna mtu yeyote yule asiyepitia matatizo. Problems are part of life. YESU pia alipatwa na matatizo mengi hapa duniani katika kazi yake ya utume. Hata mitume pia walipitia misukosuko hapa duniani na kuna wengine waliuliwa kutokana na kazi ya kuhubiri neno la Mungu. Mtu unaweza dhani unashida kubwa lakini kuna wengine wana mamatatizo makubwa zaidi yako

    Wakati wa shida na hata wakati wa raha tusiache kumuomba Mungu. Mungu wetu ni mwema na wa haki. Yeye hujibu maombi yetu.

    I hope watu wote tutajifunza kupitia story yako.

    ReplyDelete
  2. dada ulieingiliwa na mganga,umeingiziwa vitu vibaya sana ndani yako na sidhani kama utaishi na mumeo kwa furaha, yani mganga amekuharibia kweli, nakushauri nenda kwenye maombi mweleze mtumishi wa Mungu alieokoka akusaidie ufunguke.
    usipuuze najua ninachozungumza
    by grace

    ReplyDelete