Friday, May 18, 2012

UMEPELEA....?

Najuwa wote mnaijuwa kahawa ama kama wenzetu wa kule huuita gahawa, lakini je unajuwa kama kahawa ni dawa ya kuongeza nguvu kwenye kuchuma matunda? tunajuwa wakati huu wanaume wengi sana katika kuchuma tunda hawaendi zaidi ya mzunguko mtatu labda kama wanaamua kuchuma tunda siku nzima, wengi hulalamika kuumwa miguu, mara hamu huwaisha, hii hutokana na masiaha watu huishi siku hizi kunywa sana pombe, kula sana vyakula visivyokuwa na virutubisho, na kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja unakuta nguvu za kiume zinapungua sana na wakati mwengine hata kushindwa kabisa kumpa raha mpenzi wako.

Baaaasi dawa hii hapa kama wewe ni mpenzi wa kahawa ama japo huipendi lakini unaweza kunywa ndio tiba ya ugonjwa wako kahawa chungu kabisa kama hizi tunazouziwa mitaani ni safi sana ukinywa ile ukashushia na karanga zako ama korosho ukatulia kwa muda halafu ukaenda sasa kuuzunguka mti uupendao na kuchuma matunda.

Uzuri wa kahawa ni kinywaji cha asili haina madhara sio kama hizi dawa za kisasa zakutengenezwa na binadamu unazoambiwa zinaongeza nguvu za kiume lakini baadae zikaja kukudhuru, basi kama ulikuwa hujiamini katika mzunguko hofu yako wala isikunyime raha dawa hiyo hapo jipe raha sifa akupe mkeo/mpenzio

No comments:

Post a Comment