Dada Rose, natumaini wewe ni mzima please naomba post this for me in your blog, yani sikuzani kama ningeweza hata siku moja post my own life for people to discuss lakini maji yamenikalia shingoni sina la kufanya zaidi ya kutaka tu ushauri kutoka kwenu.
Mimi ni mdada nilikuwa na boyfriend wangu ambaye kwa nilivyokuwa naona nakujuwa mimi ni kwamba tulikuwa tunapendana sana, huyu kaka ni mchagga na mimi ni msukuma, na anafanya kazi nzuri tu ambayo imemfanya ajenge na kuweza kumudu maisha ya dar es salaam kwa uzuri.
Kuna siku katika uhusiano wetu maana tumekaa kwenye uhusiano miaka sita akaniambia kwamba yeye akitaka kuoa ataoa msichana wa kichagaa lakini kwa jinsi alivyokuwa anaongea nilikuwa nachukulia kama utani maana alikuwa anaongea kama utani ambacho nilijidanganya kumbe mwenzangu aliniimaniishia.
Kwasababu hatukuwa tunakaa nyumba moja siku hiyo nikatoka kwa wazazi wangu weekend huwan naenda kwake na kurudi kwetu jumapili maana hata kwetu wanamjuwa maana tumekuwa wote miaka mingi na wote walijuwa yeye angekuja kunioa, basi mwenyewe kama kawaida yangu nikishafika kwake huwa na vua nguo na kubadilisha nguo zangu za kushindia (maana kwake pia ninanguo kwahiyo siihitaji kubeba nguo kila weeend nikienda) na kuanza usafi wa nyumba.
Nikafanya usafi nyumba nzima nikabakisha chumbani kwetu sasa, nikaingia nikatandika kitanda nikaenda sasa kufanya usafi chooni, nilipoingia nikashangaa kuona nguo ya ndani ya mwanamke imeanikwa ambayo si yangu, sikutaka kuwa na jazba, nikaiacha na kuendelea na usafi na mambo mengine mpenzi wangu hakuwepo wakati huo wa usafi aliporudi kazii jioni nikamuuliza akaniambia alipita dukani akaiona hiyo akaamua kuninunulia wakati akioga aliamua kuifua ili nikija tu niivae nisiangaike kufua kama kawaida yangu kila nikinunua nguo za ndani kabla ya kuvaa lazima kwanza nizifue. (nikamuamini na kumshukuru na kumuomba msamaha kwa ukali niliomuulizia nao).
Zikapita wiki mbili nikaenda tena kama kawaida yangu ya kulala weekend sasa hivi nikakuta viatu vya mwanamke chumbani nikajaribisha usikute nimenunuliwa zawadi lakini nikashangaa havikunitosha hapa sasa ndio nikaanza kuchanganya akili kwamba hiki ni kimada chake sasa nitakikomesha nikaenda dukani kununua wembe na kuchanachana vile viatu kuangalia kwa makini chumbani nikakuta kiko na nguo mbili za hicho kimada zote nikapitisha wembe na kuondoka.
Mpenzi aliporudi na kuona vile moja kwa moja akaja nyumbani kwetu bila hata aibu na kuniuliza nilichofanya (you are cheating on me and talking to me like nothing is wrong?) nilichomwambia ni kwamba dont you ever show your face here again, akaondoka na baada ya miezi mitatu nasikia ameoa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! yani nilitaka KUFA kwa kuchanganyikiwa holding on to him for six years nikamwambia to give me space for what happened then kaoa!!!!!!!
Basi kupeleleza kamuoa nani nikagundua dada mmoja wa kichagga ndio nikakumbuka yale maneno na kujilaumu kwa nini sikuachana naye mwanzo, halafu huyu kaka alivyowaajabu after kuoa miezi sita baadaye anarudi kuniomba msamaha na kutaka niwe naye kama hawara!!!!!!!!! nikamkatalia yani anakuja marakwamara kunibembeleza na kunitumia mazawadi na kunitumia hela kiasi ambacho hata mwanzo alikuwa hanipi hivyo!!!!!! nikimuuliza wewe si hukuniona wa maana unioe anaipotezea kila mara hiyo topic
Sasa sijui nifanyaje tokea kaniacha na kuoa sijawahi kuwa na mtu mwengine kwasababu sijui kama nitaweza, now that he wants me back kuwa na mume wa mtu ni dhambi lakini i feel i so miss him and want him back, lakini nafikiria nitakuwa hawara mpaka lini and i was to be mke wake. now am confused i just dont know what to do.
MY DEAR, don't get confused, that man is not meant to be yours, achana nae kabisa. Mungu atakupa Mume aliyemwaminifu na wa kwako than to be a kimada to somebody. Muombe Mungu, dont loose hope.
ReplyDeleteSamahani kusema ni kama unaniongelea mimi, kila kitu ni sawa, miaka kwenye uhusiano,kubaki single,Kusema ataoa mtu wa kabila lake n.k isipokuwa kabila tu. Wangu alikuwa Mkurya. Kama wewe amerudi kuomba turudiane anioe mke wa pili.
ReplyDeleteLakini nakushauri, USIKUBALI KURUDI, amekupotezea muda na atakupotezea muda zaidi.Ni vigumu sana, naelewa kwa sababu nipo kwenye situation hiyo. MUNGU ana apango mzuri na wewe na mtu muafaka anakuja kwa ajili yako. Jiulize labda ungeishi ndoa ya shida, ndugu zake, wazazi labda wasingekukubali, You have to climb a rough mountain to be on top. The best is yet to come.....!
Jamani mi ni mwanaume na ningependa nimshauri dada aliyetuma swali lake pamoja na wewe uliyesema umepitia situation kama ya huyo dada. Jamani jalini maisha yenu kwanza kuliko ya wengine, hebu fikirien kama mtu kakuacha kaenda kuoa huyo mwingine kumbe kaoa Muathirika kisha anarudi kwako akuambukize maana huwezi mtambua kwa kipindi kifupi. Lakini cha zaidi ni kwamba Mungu ana mpango mzuri na wewe mtu hawezi tokomea kwa miezi6 na kisha kuoa moja kwa moja inamaanisha alishakuchoka akaanza kuingiza na kimada ndani, kupenda sio upofu kama wanavyosema wengine, kaza moyo chagua kuteseka au kuishi kwa raha, huyo ni mume wa mtu, utajaribu kutembea nae kwa kificho mwisho wake itajulikana kama tulivosoma kwenye hiyo story ya juu ya mtu na shoga yake kumuibia mme, na wanawake wengine wanaweza kukutumia hata majambazi wakumalize kwa kuwachukulia waume zao. Achana nae utamsahau na utampata mwingine na mtafika mbali tu. Narudia tena, achana nae utakuja kuliamara3 ya ulivolia mwanzo dada yangu.
ReplyDeleteisaacmwaipopo@gmail.com Aizoo hapa.
from East Zu, Dodoma.
My dear hebu naomba msahau ingawa ni ngumu sana mtu mliyekuwa pamoja miaka sita. Muombe sana Mungu akupe nguvu ya kushinda hiki kipindi huyu kaka hakuwa mtu mzuri kwako alikuwa anakutumia kumaliza shida zake. Achana naye kabisa Mungu atakupa wako maana hata ufanyeje yule tayari ni mume wa mtu. Usiharibu maisha yako na wala usikate tamaa utakuja mpata wako atakayekupenda sana.
ReplyDeleteThere is a good man outside there waiting for you. Never give up. Just trust in the Lord. Huyo mwanaume achana naye kabisaa tena usimuentertain kabisaaa, hivyo visent vyake akamlishe mke wake wa kichaga. Mwambie you are not that cheap.
ReplyDeleteJamani wadada mie ni mwanamke mwenzenu lakini siwaelewi kabisa mnaposema umekaa na mtu miaka 6 bila kujua hatima yako kwenye huo uhusiano. Miaka 6? Nauliza tena seriously miaka 6? Ungezaa mtoto ndani ya huo uhusiano si angekuwa keshaanza std 1? Mtu anakwambia wazi siwezi kuoa mtu ambae sio kabila yangu bado unakaa unasubiri? Kweli kupenda upofu.
ReplyDeleteMimi dada yenu usichana wangu nilikuwa najipenda mimi mwenyewe kwanza kabla sijampenda mtu mwingine kwanza. Na hilo lilinifanya kutoingia kwenye mahusiano kirahisi mpaka nilipomaliza high school. Na kwa kuwa nilikuwa na malengo na maisha yangu mahusiano yangu baada ya high school kabla sijaanza chuo yalikuwa yale ya kuwaste time, ya uboyfriend na ugirlfriend lakini nilivyoingia University tu sikutaka ujinga huo.
Na mtu niliyekuwa na uhusiano nae hapo chuoni ndiye mume wangu. Mwanzoni kabisa nilimwambia wazi kama unatafuta hit and run anza mbele sina time na relations isiyo na malengo usinipotezee wakati ukanizibia nikaacha candidates ambao wako serious na tayari kuanza kujenga maisha na mimi. Msione aibu wasichana kuwauliza bluntly wanaume lengo na madhumuni ya huu uhusiano ni nini? Kwa sababu nina uhakika huyo dada aliyeleta hii mada na hata huyo aliyesema na yeye yamemkuta ndani ya miaka hiyo 6 wako watu walionyesha nia ya kutaka kuwaoa lakini waliwatolea nje. Lakini kipindi hicho wanafuatwa na wengine wangewaface wapenzi wakawauliza bila kupepesa macho "bwana wee naona mwaka wa 2 unakatika huu una mpango gani na mimi? Kama huna mpango nianze mbele unanizibia watu wananiona niko tayari najenga ujumba kumbe hamna kitu." Of course atakujibu haraka ya nini? Mjibu my biological time inatick I dont want to waste my time nipe jibu ndani ya wiki".
Na ukiona baada ya wiki hakuna jibu linaloeleweka anza mbele, kauguze maumivu ya moyo lakini baada ya muda utaheal na utampata mtu mtakaejenga nae maisha. Miaka 6 kwa mwanamke is a hell of wasted time. Wengine jifunzeni hapo msirudie makosa ya wenzenu.
Ni mimi your big sister from another mom.
ee h hicho kitu kinauma sana acha mchezo.but jipe moyo utaweza mimi nimeachiwa mtoto ana miaka 16 na mtu ambaye alitoa bikira yangu , lakini kwa sasa hata salam hatupeani.inauma sana mi nauguza kidonda mpaka leo and i still love him
ReplyDelete