Friday, May 18, 2012

Dada Rose,

Natumaini wote humu hamjambo, leo nimeona nikuandikie kuhusu jambo linalomuhusu mama mkwe wangu ambalo linanikera sana na sijui nimwambiaje aelewe bila mimi kumkosea heshima.

Nipo kwenye ndoa mwaka wa nne huu sasa na nina watoto wawili wote wakiwa ni wakiume, na wakwe zangu wanaishi hapa Dar lakini mimi wazazi wangu wapi kijijini Songea.

Kinachoniudhi mimi ni kwamba mama mkwe sijui hanipendi ama vipi yani simuelewi ameanza tabia ya kumtafutia mwanaye mahawara mpaka anamlipia gesti mwanaye ya kukutana na hao hawara zake najuwa utajiuliza nimejuaje kutoka kwa mama mkwe mwenyewe yani akija nyumbani kwetu hata raha sina na siku hiyo ndio nikasikia akiongea na mwanaye kwamba kuna mdada kamuona ni mzuri na angependa aende kumuona akampa namba ya simu na akamwambia nitampeleka sehemu utamkutia huko.

Nikiwa jikoni nasikiliza wao wlikuwa sitting room yani mume wangu wala hakukataa na sijui ni kwanini hakukataa nikaenda kuwauliza nani huyo mnaneda kukutana naye maana nilishindwa kuvumilia mama akaniambia hayanihusu hayo ni mambo yao ya kifamilia, nikamuuliza kwani mimi sio familia yenu jamani mama mkwe akaniambia familia yako ipo Songea hapa wewe ni mpitaji tu.

Kwakweli niliumia sana na ninamshukuru Mungu mume wangu naye hakuyapenda yale maneno, baada ya mama yake kuondoka akanifwata chumbani na kunieleza yote kama kweli nilivyosikia nikamuuliza kwanini unaniambia haya na usifanye kama mama yako alivyokwambia akaniambia ni kwasababu sijawahi kuwa mke mpumbavu na ananipenda na hataki mtu na kitu chochote kiingilie ndoa yetu.

Nilifarijika japo sijataka kumuamini sana mume wangu maana anaweza kusema hayo ili nisijisikie vibaya lakini kama akiamua kutomkosea mama yake je? nilitaka tu mpate picha sasa mama mkwe kuingilia ndoa yangu na kunikosea heshima nimfanyaje maana yani hajali machungu yangu yani anamjali mwanaye tu, mume wangu mwenyewe hata sijui kama nimuamini ama la nimechoka kabisa.

Warda 

5 comments:

  1. mpenzi pole sana jitaidi kumuomba mungu ili mume wako asibadilike inaonekana anakupenda sana,and for mama mkwe achana nae ibaki heshima tu!

    ReplyDelete
  2. Warda unaamini kuwa kuna uchawi na wachawi? Na je ukimkuta mchawi anawanga atakwambia mie ni kweli mchawi au atajitetea?

    Hao bwana wana mambo yao ya kifamilia na inaonekana hiyo familia inaabudu mashetani maana duh, unless hii story umetunga kwa sababu na maradhi haya yaliyopo, na statistics haziongoki watu kibao wanaishi na virusi vya ukimwi mkiwa watu 3 basi mjue mmoja wenu anao iweje huyo mama mkwe wako amkuwadie mwanae mahawara na hali yenyewe ni mbaya kama hivyo? Si bure hapo kuna mambo ya kishirikina zaidi na ukifanya mchezo utaliwa nyama. Fanya uchunguzi wako mwenyewe ujiridhishe na ujue namna ya kujikinga!

    ReplyDelete
  3. sali dada yangu mpendwa huku ukinukuu mistari ya biblia ukimwambia kama zaburi na mingine ukimwambia MUNGU kuwa ulisema nikuite nawe utaniitikia na hakika atakuuitikia. Mimi nilikutana na magumu wakati fulani nilimwambia Mungu amenisaidia yameisha.

    ReplyDelete
  4. duh...wakunyumba pole. hivi hili swala la mama wakwe kuwachukia wakwe zao hapa duniani mbona linazidi kushamiri. binafsi naona ni ngum sana kuwaridhisha viumbe hawa..yani asipokubali kuwa wewe ndo chaguo la mwanae, kazi ndo inaanziaga hapo....nafikiri hili linahitaji busara, uvumilivu uliopitiliza mana kwa kweli inaboa! watu kama hawa wanataka mgombane ili mumeo aonekane ameoa mwanamke mwenye gubu..usiwape nafasi. mpende mumeo, mheshimu ili hata kama itatokea akafanya upuzi bila wewe kujua...ajutie. nasema hivi kwa kuwa ni ngum sana ku m control binadam. ila ndo na sisi tusije tukawa vikwazo kwa wanetu wakiume kama hawa mama zetu...kizazi hiki cha mama zetu wamekubuhu kwa hilo. mtu akipata mkwe anampenda, anasali asibadilike...kwanza anakuwa haamini amini!

    ReplyDelete
  5. warda my dia, vitu kama hivo visikutie mawazo na kukunyima raha, wewe kama mke endelea na majukumu yako kama kawaida, na uongeze mapenzi kwa mumeo, chonde chonde usiyapekua hayo mambo, cjui uanze kumfwatilia mumeo, utajikuta unatoa maamuzi sivyo ndivyo. mie nakuomba ujitulize na wala usitie hofu, mbivu na mbichi utaijua, kama ulivoweza kulijua hili kwa wazi na hilo utalijua.
    usije kumpa mumeo sababu ya kwenda huko au kuendelea kwenda, ila mwenyewe kashasema hawataki hao anaotafutiwa, wewe amini na kua mke bora, mbona penye ukweli uwongo hujitenda.
    tafadhali usijemgombanisha na mama ake, mwache mama afanye visa vyake, dawa ya mjinga mwache usijibizane nae. usitafute sababu ya yeye kuanza kusema mengine. kaza buti kwa mumeo mamie, na mama mkwe muheshimu.
    hamna jambo lisilokua na mwisho, mama huyo atakuja kuaibika.
    kua na subira na moyo wa uvumivilivu. kile ulichoambiwa unyagoni leo ndo uvitumie. ndoa ngumu mamie, lkn kwa mwanamke mwenye akili anaona ni mapito na anaimudu ipasavyo.
    mugnu atakutanguliza na kukuongoza

    ReplyDelete