Wednesday, April 4, 2012

Dada Rose, kuna jambo nataka uliza tunafunzwa kwamba uwanja wa mumeo na wako sikuzote unatakiwa kuwa msafi na uliokatwa nyasi vizuri hata ukiwa wazi unafurahisha, na kweli mwanzo nilivyoolewa mume wangu nilikuwa na enjoy sana kumfanyia hilo na wala hakuona aibu tena alifurahia sana.

Sasa leo tunamiaka mitatu ya ndoa nashangaa siku hizi nikimwambia nataka kumfanyia usafi hataki hata kuoga pamoja na mimi hataki, nashangaa yani sijui kawaje kama mwanamke mjamzito hatabiriki ananuna ovyo na wakati mwengine tunakaa hata mwezi hatujagusana.

Jana asubuhi wakati anavaa chumbani nilikuwa naye japo hatuongeleshani nilijikaza tu nakumuambia kwamba jioni akirudi kutoka kazini nitamfanyia usafi hakunijibu alikaa tu kimya jioni akachelewa kuja nyumbani akarudi saa sita usiku wakati huo nilikuwa nimeshalala kwa uchovu wa siku nzima na haukuwa muda mzuri wa kumsafisha mume wangu.

Asubuhi ya leo wakati anatoka kuoga akiwa anavaa nikagundua nyasi zimekatwa nikashangaa huyu mbona sikumsikia akikata chumbani na alivyorudi hiyo saa sita aliingia tu na kulala, nikamuuliza jibu alilonipa nilichoka kabisa kwamba wewe si ulitaka zikatwe basi nimeshakata shida yako nini sasa???? jamani mtu ukijitahidi kuwa mke mwema mtu hathamini kabisa usipokuwa mwema anakuambia anatafuta wa nje wa kumliwaza. na ninajuwa hakukata zile nyasi mwenyewe maana sijamsikia alivyorudi alilala moja kwa moja. kwahiyo kakatwa nje

Sasa nyie wanaume kwanini hivi jamani, yani mpaka nyasi ukakatwe na hawara? sitaki hata kuendelea kumuuliza maana tutaishia kugombana tu, ila nimemkinai yani ananitia kichefuchefu

1 comment:

  1. Pole sana. Piga goti chini na muombe sana Mwenyezi Mungu akusaidie. Yeye ni mwema na mwingi wa fadhila, husikia sala zetu. Have faith in him.

    Endelea kuwajibika kama mwanamke na usikate tamaa hata kidogo, ipo siku haya yote yatapita and He will come back to his senses. God loves you and He is there for you. Take heart

    ReplyDelete