Thursday, March 8, 2012

WAZO LANGU TU AMA LAWEZA KUWA KWELI?

Dada Rose, natumaini u mzima wa afya, dada leo mimi nakuja kwenu nikiomba nipewe ushauri maana nahisi kuchanganyikiwa, nimeolewa na nina watoto wa tatu huu ni mwaka wa kumi sasa katika ndoa yangu.

Mume wangu kwao wamezaliwa wavulana saba na wasichana wawili, kwa bahati mbaya wazazi wao walishafariki na kuwaachia mali nyingi tu zikiwemo nyumba ambazo zimepangishwa ila kodi zikitoka wanagawana sawa kwa sawa. halafu hawa kwao wanamambo ambayo kama hawamsikilizi kabisa mwanamke yani kwao mwanamke ni kama sichochote yani hata huitwi kwenye kutoa ushauri wala hata siku moja hata kama mkewe hawaombi ushauri. mpaka kuna wakati katika haya mambo ya kugawana hela za kodi kuna shemeji zangu wengine wakashauri wale dada zao wasipewe kwa sababu ni watoto wa kike, japo wa kwanza kulikataa ilikuwa mume wangu, na kweli mpaka leo wanapewa haki yao.

Ninachoogopa mimi ni kwamba hawa shemeji zangu wengine kwa jinsi walivyo naroho mbaya mpaka kwa dada zao siku mume wangu akifa sindio watatufukuza nje na kutunyang'anya kila kitu kwa madai ya kwamba ni ya kaka yao maana hawa hawana utu kabisa, japo mume wangu ananiambia hawawezi kufanya hivyo nikimwambia mume wangu basi twende kwa mwanasheria ukaniandikie kabisa vitu vyako kwamba ni vya watoto kila siku anasema sawa lakini haendi na kinachonichanganya zaidi ni kwamba kila tukigombana inafikia mpaka mume wangu kuniambia kama umechoka basi ondoka, hiki ndio kinazidi kunichanganya ama mume wangu naye ananichukulia poa.

Naombeni mnishauri jamani nifanyaje na hii familia?

2 comments:

  1. Pole sana dada yangu kwa mkasa huo cha msingu mrudie Mungu kwani kwake hakuna linalo shindikana.

    ReplyDelete
  2. Mi ningependa kujua kama unafanya kazi au ni mama wa nyumbani?
    Kama unafanya kazi basi kuanzia leo fanya kazi kwa malengo ya kwako na watoto wako. Na ukitaka hili lifanikiwe fanya kama mme wako kasafiri kaenda USA kusoma na maisha yamekuwa magumu na hawezi kukutumia pesa. Kwa kila pesa unayoipata kumbuka kusave. Katika maisha ya kiafrika hatuna utamaduni wa kusave pesa kwa sababu ya shida na majukumu tuliyonayo. Lakini wewe ni mwanamke ukiweza nunua SHARES cheza upatu fungua FIXED ACC etc fanya lolote lile ilimradi uweze kujiwekea fedha kwa ajili yako na watoto. Waswahili wanasema haba na haba hujaza kibaba.

    Kama wewe ni mama wa nyumbani na hauna lolote lile unalolifanya basi huu ni wakati wa kuamka na kutafuta kitu cha kufanya. Hata kama mumeo anakupa kila unachokitaka mwambie sasa inatosha wacha na wewe ujishughulishe. Hii karne si ya kukaa na kukuna nazi na magold yananing'inia kwa shingo...hizo zama zilishapitwa na wakati. Kama wanawake wenzio wanaweza kuamka asubuhi saa kumi na moja na kupika chapati na kuzipeleka posta kuuza baasi na wewe unaweza pia.Usijibweteka mamaa.

    Watu wengi huwa ni waoga wa kuandika husia mana wanaona ni kama wanajitakia kufa. Inabidi mumeo umwandae kisakolojia ili kuandika hii kitu.

    Nataka nikwambie katika haya yote niliyoyataja huwezi kuyafanya bila kumshirikisha Mwenyezi Mungu. Sala zinahitajika sana na wala usikate tamaa, yeye husikia sala zetu na hamna hata siku moja Mwenyezi alimwacha mtoto wake aibike. Imani bila matendo ni sawa na hakuna kitu kabisaa. Usikae na kuomba wakati hamna lolote lile unalolifanya. We umekaa tu unamtegemea Mungu akushushie kila kitu...hiyo sahau.

    URITHI mkubwa ambao unaweza kuwapa watoto wako ni ELIMU. Kama kila mtoto ataenda shule na kupata cheti chake hamna mtu yeyote yule anaweza wanyang'ang'anya cheti. Mnaweza kuwa na magari na majumba lakini watoto wakagombana na kuvisambaratisha tena within a day, kila mmoja akadai chake.

    Kwakuwa umeshaona ndugu wa mumeo walivyo sasa wewe tumia muda mwingi kuwalea watoto katika maadili yaliyo mazuri tena bila kubagua kuwa huyu ni wa kike au huyu ni wakiume. Wafundishe umajo na kujitegemea na kuwajibika tangia wakiwa wadogo. Waswahili wanasema samaki mkunje angali mbichi.

    Usikate tamaa mana mambo mengine tunjaifunzia ukubwani.

    ReplyDelete