Tuesday, March 20, 2012

SOMO......

Leo nataka niongee na wewe baba ama mama uliyeoa na kuolewa halafu kwa sababu yoyote ile mkatengana na mumeo/mkeo unapotaka kuingia tena kwenye uhusiano mpya na mtu mwengine je unamwambia ukweli kama una watoto/mtoto????? jamani tuwe wazi katika hili maana ni jambo zito sana.

Sehemu fulani mdada mmoja aliamua kuachana na mume wake ambaye walizaa mtoto mmoja wa kike basi yule dada baada ya muda akapata mwanaume ambaye alimpenda lakini huku kaka yeye hakuwa na watoto wala hakuwahi kuoa kwahiyo baada ya muda kuwa pamoja wakaamua kuoana bila huyu dada kumwambia mchumba yake kwamba ana mtoto wa ndoa iliyopita baada ya ndugu wa mwanamke kuona huyu mtoto anapata tabu wakaamua kumchukuwa kwenda kukaa naye.

Basi wakaoana na baadaye MUNGU akawajalia wakazaa watoto waili ambao sasa ni wakubwa tu kinachotuuma sisi majirani zake ni kwamba japokuwa yule mwanaye anakaa na mdogo wake karibu lakini hataki hata aende nyumbani pale kumsalimia akidai atamuharibia ndoa yake (kweli mtoto wa kumzaa mwenyewe).

Basi yule mtoto mpaka anaumwa yule mama wala hana habari naye, yani isningekuwa huyo mama yake mdogo ndio akauze vitumbua huko apate hela kidogo ndio ampeleke hospital amtibie wakati mama yake anauwezo mkubwa anapesa kwa maana yule kaka aliyemuoa kweli anahela lakini hamjali kabisa mwanaye yani nilitamani kulia juzi yule mtoto kaumwa yani mpaka kaishiwa nguvu, anatapika mpaka akadondoka watu ndio kukimbilia kwa mama yake maana ndio karibu lakini yule mama wala hakushtuka wala kutoa msaada alichosema tu ni kamtafuteni mama yake anayekaa naye wakati huyo mama yupo ilala kwenye mihangaiko mpaka akirudi huyu mtoto si angekufa..ndio wasamaria wema kumchukuwa na kumpeleka hospitali.

Ndio watu kuoana hivyo wakaamua kwenda kwa mjumbe na kumueleza, yule mjumbe kwenda kuongea na yule mama akamwambia yeye familia yake ni ile aliyokuwa nayo ndani (jamani bila hata aibu) eti huyo mtoto akamfwate baba yake popote alipo!!!!!! ama kwasababu ya geti kali? kwanini watu wasichukuwe jukumu la kumfwata yule mumewe na kumwambia ukweli wa kuhusu huyo mtoto wa mkewe maana kweli yule mtoto anateseka kisa ugomvi wa baba na mama ambao masikini yeye hata hakuwa na hatia lakini leo ndio fimbo yake inayomchapa maishani.

Jamani haipendezi na inasikitisha, kweli mwanamke mtoto umebeba miezi tisa, ukapata uchungu kuzaa leo kisa umegombana na baba yake umepata mwengine ndio mtoto wako unamuona si kitu??? kwanza ugomvi wenu watoto unawahusu nini kama unaona huwezi kulea mtoto siungemuachia baba yake labda yeye angemudu ama kama unaona naye hawezi wapeleke kwenye vituo vya kulelea watoto kuliko kuwatesa watoto.

2 comments:

  1. huyo mama nimshenzi na alaaniwe pumbavu zake ameniudhi sana

    ReplyDelete
  2. ama kweli bado kuna wanawake malimbukeni na wanaotutia aibu. kwani hata kama hataki mwanae akae na huyo mume wake wa sasa hivi, kwann aimuhudumie mwanae hata akiwa huko kwao kwa dada yake?? huyo dada ni mbinafsi. kama baba wa huyo mtoto yupo na anaweza kumlea mwanae apewe tu amlee kuliko mtoto kukaa kwa masononeko analelewa na watu wengine.
    dunia hii haina siri, soon huyo mume wake mpya atapata tu habari, siombei mabaya lakini asije kosa huyo mume na huku mwanae akamkataa, na hao wanae wengine wakaenda kulelewa na mwanamke mwengine. mungu anusuru tu.

    ReplyDelete