Monday, March 12, 2012

Aunty Rose, i hope you are all doing well, leo mimi ninahasira ile mbaya i just found out that my mum is dating this guy and i hate it.

My mum is a single woman, ametuzaa wawili mimi na mdogo wangu wote ni wakubwa sasa lakini hakuna aliyeolewa, sasa katika nyumba yetu hii kuna vyumba ambavyotumepangisha na katika chumba kimoja na sebule ameamia this dude ndio ni mzuri lakini way too young for my mother to date.

Tokea huyu kaka ameamia nikanotice my mum keeps coming back home early, halafu kila siku anamuulizia then akiwepo lazima atamualika nyumbani kuja kula na sisi yani imeshatokea mara nyingi tu as for me nikajuwa labda kwavile jamaa hajaoa kwahiyo mum is trying to act like his mother.kumbhe haikuwa hivyo.

Until siku moja nikasikia watu wanamsema vibaya barabarani kwamba walimkuta bar gani sijui na huyo kaka wakikumbatiana yani aibu tupu lakini sikuyachukulia maneno na kuyaacha nikaenda kumuuliza mama na yeye alikataa katu. basi na mimi nikaamua kumuamini mama yangu nikawa nipo peace tu hata na yule kaka.

Sasa juzi jumamosi nikiwa nimeenda kazini nikaamua kuwahi kurudi kuliko kawaida na mdogo wangu yeye alikuwa ametoka, sikumkuta mtu nikajuwa wote hawapo lakini mlango ulikuwa wazi basi nikaingia na kukaa sebleni nikiangalia tv mara nasikia watu wanaongea chumbani kwa mama nikasogelea mlango na kuanza kusikiliza nikasikia sauti ya kiume na mama nilishtushwa lakini nikajuwa labda mama kaamua kuleta mpenzi wake nyumbani maana ndio tulijuwa mama lazima tu atakuwa na mpenzi after she and my dad left each other a long time ago.

Mara baada ya muda nikiwa naangalia tv bado mlango wa mama ukafunguliwa wakawa wanatoka huku wakicheka ndipo kufika sebleni wakashtuka kunikuta nimekaa yani kilichoniuma ni kumuona kile kikaka kimemshika mama yangu kiuno nilitamani nimrukie na kumkatakata mara akaenda nje moja kwa moja, nilipomuuliza mama kwanini alinidanganya akaniambia kwa ukali kwahiyo kila bwana yangu nikuonyeshe mbona huna adabu hayakuhusu we mtoto.

Mapenzi yao kweli mimi yananikerea halafu ukizingatia yule kaka ni kijana mdogo sana kwa mama yangu, halafu kapanga kwetu then i know ana.....mama yangu yani mara nyengine sijisikii hatakurudi nyumbani maana nikwaona nasikia tu kufa. na ninachoogopa mimi ni aibu mtaani maana watu wameshaanza kumdharau mama yangu naumia sana basi tu sijui nifanyaje.

Rehema

3 comments:

  1. Pole sana,
    Kila mtu ana haki ya kupenda na kwa upande wa mama yako naona ameamua kujipoza na kijana. Hii hutokea sana katika jamii na hata akina baba pia wao hudate wasichana wadogo.

    Ningependa kunukuu huu mstari "kuanza kusikiliza nikasikia sauti ya kiume na mama nilishtushwa lakini nikajuwa labda mama kaamua kuleta mpenzi wake nyumbani maana ndio tulijuwa mama lazima tu atakuwa na mpenzi after she and my dad left each other a long time ago"Sasa ndugu ina maana kama mama angeingia na mbaba anaye endana na umri wake ungeona ni kitu cha kawaida? au usingeshtuka? au hiii ni tabia ya mama yako? mana hapa lazima uwe muwazi!Hamna hata mstari mmoja kwenye story yako inayosema mama hakuwahi ingiza mwanaume nyumbani kwenu.

    Kwa upande wangu naona kama wewe pia umedevelop some feelings for this boy. Na nukuu "ameamia this dude ndio ni mzuri lakini way too young for my mother to date". My dear you had better be careful otherwise you are likely to crash with your mother, and its going to be worse than u have ever imagined.If you have developed some feelings for this guy,na unafanya kazi tena unalipwa mshahara basi tafuta chumba chako na upange kama hii kitu inakuuma sana tena iwe mtaa mwingine mana haya mastori ya mtaani yanaweza kukupa headache.

    Au unaweza chukua muda wako ukakaa na mama ukaongea naye kwa utaratibu bila ukali kama ulivyofanya mara ya kwanza mana hapa mmoja wenu lazima ajishushe. Mueleze mama ukweli jinsi unavyojisikia na hasa ukizingatia anatembae na serengeti boy. Mueleze mama kuwa huyo kijana inawezekana anamtumia ili kukwepa kodi mana vijana wa siku hizi ni wajanja kweli, au pia anamchuna ili ajipatie msosi. Na pia ajue kwamba huyu kijana hawezi muoa ni lazima atafute msichana mwingine anaye endana naye. Kwa ufupi huyu kijana anapunga upepo tu. Inabidi mumchunguze kwa kina usikute ndo tabia yake kutembea na mama wakubwa. Na pia mama akumbuke kuwa kuna magonjwa awe mwangalifu sana.

    ReplyDelete
  2. Dada usisahau huyo ni Baba yako .. kwani ndiye anayemliwaza Mama yako.. Nampongeza Mama yako kwa kuweza kupata kijana atakayekuna Roho yake ... Jenga heshima kwa Mama yako .. aibu ya mitaani isiharibu ustawi wa familia yenu

    ReplyDelete
  3. sika dada we hama then mwambie mama yako wafanyie humo humo ndani wasiende nje coz huko nje ndowataonwA nawatu itakuwa aibu sana japo now nikitu chakawaida sana mama kutoka navijana coz ndotuna damu moto natunakata kiu coz tunakaa muda mrefu hewani

    engineerbigboy@gmail.com

    ReplyDelete