Monday, January 9, 2012

UNAJUWA YA KWAMBA..

Najuwa kina baba nitakuwa na wakwaza kuhusu hii mada, lakini huu ni utafiti niliofunya na watu waliokwenye ndoa, tumegundua ya kwamba wanaume wengi wanaingia kwenye ndoa wakiwa wakijuwa vizuri tendo la NDOA tu kulala na mke wake na kumpa raha za kitandani ambazo wanawake wengi wamekiri kutimiziwa na kufikishwa kilele na wame zao kwenye sita kwa sita.

Lakini wanawake wanaingia kwenye ndoa wakitegemea mengi sio kumridhisha tu mumewe kitandani, lakini wanakuwa na mapenzi tele, wanafanya mengi ili kumfurahisha mwanaume, mwanaume utabembelezwa ukiwa umekasirika, utaombwa msamaha bila pingamizi atakapokuwa amekosea, utaenda kuogeshwa, na mambo yote ya usafi na afya.

Lakini leo nataka kuongelea ubinafsi, nimegundua kutoka kwa watu wenye ndoa zao kwamba wanalalamika sana wame zao kuwa wabinafsi, wao ndio wa kwanza kutafuta wanawake nje japo wanatimiziwa yote ndani lakini bado wanatoka nje, wao ndio watalewa na kuja nyumbani hoi wakati mwengine kutapika halafu mkewe amfanyie usafi, wao inaweza kupita hata wiki mbili mwanaume hajala chakula alichopika mkewe, wao haohao inapita mwezi hajakutana kimwili na mke, akimkosea mkewe inamchukuwa muda sana kumuomba msamaha, yani kwa ufupi matatizo mengi ya kwenye ndoa asilimia 7 kati ya kumi husababishwa na wanaume.

Jamani huwa ninamsemo wangu napenda sana kuutumia kwamba ndoa sio mchezo wa kuigiza, kweli kuna ndoa nyengine huingia matatizoni kwasababu ya matatizo ya mke yalioshindikana lakini nyingi sana wanaume ndio wanaumiza mioyo ya wake zao, ukiwa kama baba mwaka huu unapoanza hebu tubadilike kwenye ndoa zetu maana mke wako huyo ni MUNGU ndiye aliyekupa aliona wanaume kibao tena usikute wazuri na wenye hela kuliko wewe lakini kwanini alikupa wewe huyo mke na sio hao wa nje unaokimbilia kwani alijuwa huyo ndio ubavu wako na ndio starehe na raha yako.

Na haya matatizo ya magonjwa sugu kama ukimwi katika wanandoa hii ni laana jamani kweli unamuacha mkeo/mumeo unalala nje bila condom halafu unamletea ukimwi ndani ya nyumba masikini yeye anajitunza anaamini siku utabadilika!!!!!!! jamani hii ni hatari


0 comments:

Post a Comment