Dada Rose, mimi ni mwanaume na kwetu tumezaliwa watatu na mtoto mmoja wa baba wa nje ambaye ni wakike sisi watatu wote ni wa kiume, baba na mama yangu walipokutana tayari baba alikuwa na huyu mtoto na akamueleza mama yangu ukweli naye wala hakusita kuwa na baba yangu kisa huyo mtoto wakaoana na kutuzaa sisi wa tatu.
Wakati kaka yangu wa pili amezaliwa ndipo baba akaamua kumleta yule dada yangu wa kambo nyumbani ili tuishi naye mama wala hakumbagua alimpenda kama mtoto wake, mara mimi nikazaliwa maisha yalikuwa tu yakawaida na wote tulipendana sana, mara ikaja kipindi baba yangu akabadilika sana akawa mtu wa pombe sana na mara akaanza kulala nje mpaka asubuhi na wakati mwengine anampiga sana mama yani kaweli manyanyaso yalikuwa ya hali ya juu hatukukuwa na lakufanya bali tu kuwa upande wa mama yetu na yule dada upande wa baba yake.
mara mama yangu akaumwa na kufariki, kwakweli lilikuwa pigo lakini tulikuwa hatuna la kufanya tukiamini MUNGU alimpenda zaidi yetu baba huku ndiyo akazidi kuwa kicheche na hela akawa haachi kwahiyo tulikuwa tunahangaika wenyewe kufanya kazi, kujisomesha mpaka tukapata kazi na kujitegemea dada yeye hakuondoka maana tuliona hana shida kila siku anapendeza mara nguo mpya mara kwa mara kumbe hatukuwa tunajuwa dada yetu wa kambo alikuwa akitembea na baba yetu yani dada anatembea na baba yake mzazi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Kwakuwa tulikuwa tumeshahamka nyumbani dada yeye aligoma kabisa kuhama, lakini kwa vile hatukujuwa linaloendelea hatukuona kama ni mbaya kwani tulijuwa hapo pia si kwake, sasa kunakipindi baba akaumwa sana kumpeleka kwenye matibabu wakagundua alikuwa na ukimwi, ndipo mara dada tukawa tunamuona kama kachanganyikiwa hatumuelewi wakati wote tunamuuguza baba dada wala alikuwa haji yani akawa amejitenga kabisa nasi na baba kuna kipindi baba akazidiwa kabisa akatuita ili atupe urithi naye dada alikuwepo ndipo kwanza akaanza na msamaha kwa kutueleza kuhusu yeye na dada.
Kwakweli ilikuwa ngumu sana kukubali lakini sasa tukajiuliza hata tusipokubali tutafanyaje, dada naye ndio mgonjwa vilevile lazima tusimtenge, basi baba akasema kwavile dada yenu ndiye mkubwa natumaini mtakaa naye vizuri nawaachia nyumba(atasimamia dada) na kiwanja kingine mtasimamia wote, baada ya mwezi baba akafariki.
Miezi mitatu sasa imepita tukamfwata dada nakumwambia tupangishe nyumba naye tutampangia pakukaa ili hela tukipata itusaidie dada sasa kagoma na tumetumiwa ujumbe sasa twende kwa mjumbe tunatakiwa tusishughulike na hile nyumba kwani dada anasema ni yake na sio yetu yani hataki kabisa tujishughulishe na ile nyumba na tumeletewa barua kwamba kesi ipo mahakamani!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Kuandika kwangu hapa kwa wanaojuwa sheria unadhani tunaweza kukosa nyumba ya baba yetu hata kama aliachiwa dada aisimamie? ama watadhani kwasababu yule mtoto wa nje tunataka kumuonea? naombeni msaada wenu tafadhali
Jambo la kwanza nendeni huko mahakamani mkasikilize kafungua kesi ya nini. Kama kafungua kesi ya mirathi basi wekeni pingamizi kuzuia asiwe msimamizi wa mirathi kwani hataweza kutenda haki, na pili lazima kuwepo kikao cha wanandugu kuchagua msimamizi wa mirathi. Na nyie mtasema kuwa hakuna muhtasari wa kikao (anaweza kuwa kafoji au kahonga huko mahakani muhtasari wa kikao) ambao una signature zenu kumchagua yeye kama msimamizi wa mirathi.
ReplyDeleteNa kama ni kesi nyingine tu ya kipuuzi kaifungua mahakama ya mwanzo (huwa hakunaga haki mahakama za mwanzo ni pesa tu zinatembea) nyie nendeni kwa wakili na summons (samansi) yenu mliyoletewa mumuombe awe wakili wenu. Yeye atawapa barua ya kuipeleka mahakamani siku ya kesi, kisha hakimu wa mahakama ya mwanzo atashindwa kuendelea na hiyo kesi atamuamuru dada yenu akafungue kesi yake mahakama ya wilaya (angalau huko kuna nafuu na haki yenu mnaweza kupata) kwa hiyo hatasikiliza wala kutoa uamuzi kuhusu shauri lenu maana mawakili hawaruhusiwi hata kukanyaga mahakama za mwanzo.
Na kama hajafungua mirathi, fungueni kesi ya mirathi na kugawa mgawanyo wa mali, na mahakama ndio itaamua kama ana haki au la. Na mtagawana kila kitu including hiyo nyumba. Hata sie mdogo wetu wa tumbo moja alitusumbua sana kwenye mirathi tulimuweka kama msimamizi akageuza kila kitu mali yake, tukamtoa kuwa msimamizi huko huko mahakamani.
Kaka kuna taratibu za kufuata, kama unahitaji msaada zaidi, nitumie namba yako kwenye isaac_mwaipopo@yahoo.com then ntakujulisha namba yangu nikupe ushauri wa kisheria kwani kwa taaluma mimi ni mwanasheria, lakini kwa ufupi kama Baba hakuacha wosia kwa maandishi itabidi kikao kikae cha wanandugu kimchague msimamizi wa mirathi, then muende mahakamani (MAHAKAMA YA MWANZO) iamthibitisha au kumbatilisha msimamizi wa mirathi then kama kuna mtu anapingamizi anapeleka mahakamani kupinga kuteuliwa kwake, kwa ufupi kuna process ndefu na hamuwezi kupoteza haki zenu.
ReplyDelete