Wednesday, January 18, 2012

Dada Rose natumaini u mzima leo nakuja na mada kwako ya hawa wame zetu ambao ndio kilio kikubwa katika ndoa zetu za sasa, mume wangu amenitenda na wala sikutegemea kama angenitenda, tulioana mwaka elfumbili na nane, tukabahatika kupata mtoto mmoja, hivi mwaka jana nikapata tena mimba na nikajifungua mwezi wa kumi na mbili.

Mwaka jana mwezi wa saba mume wangu akaanza vituko sana, mara hali nyumbani, anachelewa kuja, mara akaacha kabisa kuwa karibu na mimi na mtoto yani tukawa tunagombana kila mara na kumbuka nilikuwa mjamzito, na wala hakuona huruma akawa ananipiga hivyohivyo ni MUNGU tu aliyenisaidia nikajifungua salama na ikafika kipindi akawa harudi tena nyumbani hajali kama tumekula wala hajali hali yangu na nilikuwa sina mtu yeyote wa kunisaidia zaidi ya mimi na mwanangu wa miaka mitatu.

Hivyohivyo tukajikongoja na mwanangu bahati nzuri mdogo wangu yeye kaolewa hapa dar ndio tukahamia kwake mpaka nimejifungua hadi leo, mara mwezi wa kwanza nikasikia mume wangu kauza nyumba kapata kama milioni 20 yaani hatakusema haje kumuona mtoto huyu mpya ama yule mwengine hata kututumia hela ya matumizi hamna, sawa hata kama mimi hanitaki kwani watoto wake wamemkosea nini.

Ninachosikia kwamba sasa hivi anaishi na mwanamke mwengine na maneno kibao anatapakaa kwa watu kuhusu mimi ndugu zake wananiambia huyo mwanamke mwengine atakuwa kamloga hawezi tu kuitelekeza familia yake kwamba nimuombee tu arudi lakini kwa dharau na maumivu aliyonionyesha kwakweli itakuwa ngumu kumsamehe kwanza nitaanzaje???

Najuwa wengi huishi na wame zao ama wake zao kwa sababu ya watoto lakini kwa chuki niliyokuwa nayo kwa huyu mwanaume wala sintoweza kumsamehe hata akija anatambaa kwa tumbo. naomba hili liwe fundisho kwa wanawake wenzangu kwamba wanaume hawa tunahitaji kuishi nao mguu nje mguu ndani hata ukiwafanyia mazuri na mapenzi tele hawana shukrani wala fadhila.


3 comments:

  1. Pole sana mdogo wangu, mbona hata raha ya ndoa hujaifaidi. Lakini kilio na laana yako vilikuwa vikali mno vimemfika huyo mumeo, hakurogwa wala nini, maana kuuza nyumba ili ukastarehe hata kama ni ya miti au chumba kimoja ni laana tosha. Midamu umeamua kuendelea na maisha yako msamehe tu ili uweze kumove on, maana hapo alipo si kazi hana hata senti, milioni 20 si pesa ya maana sana akichange mara mbili tatu hana kitu.

    Tafuta shughuli ya kufanya ya kukusaidia kulea watoto wako, huyo ndio keshapigwa na fimbo ya ulimwengu pesa zikimuishia atarudi anatambaa, mpokee kwa masharti mojawapo ni kupima Ukimwi na usitembee nae mpaka arudi tena kupima baada ya miezi 3. Atakuwa keshapata somo huyo, na hao nduguze si wao wamuombee ni ndugu yao wao sio wewe. Wewe msubiri tu atarudi mkia nyuma keshafunzwa na ulimwengu na atakaa kwa adabu zake.

    ReplyDelete
  2. Mhhhh dada pole sana...

    ReplyDelete
  3. Pole sana mdogo wangu, naomba kuogeza wadau wangu, siku zote mwanaume sio mwenzio, akina mama mwanaume mpende tu pale panapo bidi maana hawaeleweki na pia tujitahidi kutafuta shughuli zetu wenyewe kuliko kumsubiri mwanaume, usijari tayar ameshapata laana kuuza nyumba kwaajili ya demu wa nje, Muombe mungu akupe nguvu yakupata akili ufanye mambo yako na atakushindia wangu pole sana, Dada grace wa Kimara

    ReplyDelete