Wednesday, November 9, 2011

WANAWAKE TAMBUENI..

Hii, ni kwa wanao taka kuingia kwenye ndoa na walio kwenye ndoa, biblia takatifu inasema MUNGU alimuumba mwanaume na katika ubavu wake akamtoa mwanamke na wote wataacha wazazi wao na kuambatana na kuwa mwili moja mpaka kifo kiwatenganishe, kwahiyo kabla hujaingia kwenye ndoa tafakari je huyo ni ubavu wako na kama ndio olewa naye kwa shangwe, na pia biblia inasema mwanamke atamlinda mume wake basi ...mama kuwa mstari wa kwanza kumlinda mumeo manung'aembe kila kona kutwa kuganda wame wa watu unadhani mchezo kuolewa na kudumisha ndoa, kueni makini sana wakishamuona mume kapendeza anaafya wanaanza kujigongesha na wanaume hawaachagi watakula na watakuambia kwamba yule anajipendekeza kwangu namaliziaga shida zangu tunapokuwa tumegombana nakupenda mke wangu, basi utamsamehe na kuendelea na ndoa yako kwani mwanamke mpumbavu huibomoa ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe... mke ni mmoja tu kwa mumewe yeye ndiye wako peke yako hao wengine wasikutishe.... Mwanamke ndoa bwana, heshima ni kuwekwa ndani sio kuliwa na kuachwa kama mzoga...

1 comment:

  1. ni kweli kabisa minung'aembe kibao siku hizi inafwata waumeza watu lazima tuwe makini tulio kwenye ndoa.

    ReplyDelete