Tuesday, November 8, 2011

JAMANI KAMA NDIO HIVI SITAKI TENA..

Dada Rosemary natumaini u mzima, dada najuwa wewe umeshakuwa na watoto wawili utakuwa unajuwa mengi kuhusu mimba pamoja na wanawake wengine wote waliozaa wanaopitia blog hii na wale wanaume wenzangu ambao wake zao wameshajifungua wanaweza pia kunisaidia.

mke wangu ni mjamzito anakaribia kujifungua sasa lakini kuna vitu ambavyo naviona kwake ambavyo sivielewi naomba mnieleweshe kwanza jamani hii miezi ya mwisho anakuwa na hasira za ajabu yani nikichelewa kurudi nyumbani inakuwa balaa siku kanifokea mpaka akachukuwa kisu anataka kunichoma na wala haonyeshi roho ya huruma ananilaumu nimempa mimba namuona hafai namrudia usiku lazima nitakuwa nilienda kwa mwanamke wakati wala nilikuwa tu nakunywa na rafiki zangu.

nikimuomba mambo hataki jamani tena anakuwa mkali sana nina mwezi sasa hivi sijapewa yani hata nikimgusa anarusha mkono wangu huko na sonyo juu jamani ndio hivi ama?

nikiwa nyumbani labda nikavua viatu sebleni na yeye yupo yani ni kero atanisema kwa nini sivipeleki sehemu ya viatu, mara nikilalal bila kuoga anahama chumba ananiambia nanuka yani kwakweli ananifanyia vituko ambavyo sielewi kama ni mimba ama ni nini sasa kama jana kaniambia nina hamu ya pizza nikaenda kumnunulia steers nilivyorudi ananiambia hamu imemuisha anataka ale ugali dagaa na dagaa hamna ndani kwahiyo kalala amenuna mpaka leo asubuhi namuongelesha hanijibu.

hiki ni nini?

3 comments:

  1. pole ,msamehe tu hiyo hali inatokana na mimba aliyonayo,
    atakapojifungua inaweza kuisha.ila kuna mahali umesema unalala
    kuna siku unalala bila kuoga....aah jamani utalalaje bila kuoga,
    huoni kama huo ni uchafu tena uliokithiri ana kila sababu ya kukwambia unatoa harufu. Jitahidi usafi bana, hata nichoke vipi lakn kulala bila kuoga ni jambo kisilowezekana.

    ReplyDelete
  2. wewe kaka unaeomba ushauri ni hivi kabla ya mkeo hajabeba hii mimba alikuwa natabia hii?na kama sivyo kaa ukielewa mimba zingine zinavituko sana sio kama anajifanya hapana ni hali ya kawaida kwa mwanamke akibeba mimba wengi wao wanakuwa na vituko mimi hapa ninaekuandikia hapa ni mwanamke mimi nilivyokuwa na mimba nilikuwa sitaki kumwona hata kwa macho mume wangu na nilikuwa nachagua vyakula lakini mume wangu alikuwa muelewa hakunishaa na wala hakunichukia kwasabubu anajua ni mimba ni swala la muda tu mimba inakijeujeu kama kinyonga kwa hiyo isijali haya kaka hayo ni maswala ya muda tu mfumilie mwenzio mpaka hapo mungu atakapo mjalia ajifungue salama tena ushukuru huyo wako ameanza karibia na kujifungua kwani wengine wanaanza vituko kuanzia mimba ikiwa changa. N.B mimi naona ingeanzishwa ushauri nasaa kabla hawa wanaume hawajaingia kwenye ndoa wafundishwe jinsi mwanamke anavyobadilika akiwa na mimba naona itasaidia kuweza kuelewa

    ReplyDelete
  3. Kama hongera kwa kumtundika my waifu wako mimba kwanza. Hizo zote ni sababu ya mimba ndugu. Ila hilo la ww kunuka haliwezi kuisha sababu unalala bila kuoga. Ww umeoa inabidi ubadili lifestyle brother hayo mambo ya kisela kutoka kwenye pombe kisha kulala noma. Mi naweza kuhesabu ni mara ngapi nilipata game wakati mke wangu mjamzito. Hasura hadi siku nyingine nalala stoo. Wakati mwingine unatamani kumpasua lakini unaomba roho mtakatifu akusaidie. Cha muhimu ni kuvumilia na kujitahidi kujiepusha kugongana nae. Besides, ni kipindi kifupi tu na nilipokabidhiwa mtoto pale hospitali basi nikasahau yote na sasa tunalea mtoto wetu tunaenda mwezi wa pili sasa. Hapa ndo kipimo cha utayari wa mwanaume kuingia katika ndoa. Ukimpiga, ukitoka nje ujue ulikuwa hauko tayari.

    ReplyDelete