Friday, August 12, 2011

KANIPA MIMBA, ANANIHUDUMIA, RAFIKI YANGU INAKUUMA NINI?

Rosemary,



leo ninajambo kubwa sana limenikaa kwenye koo limenikaba nataka nilitapike kuhusu rafiki yangu kipenzi maana hata miye sikutegemea kama angenifanyia hivi.


nilipata mwanaume mzuri tu huyu kaka hakuwahi kuwa na mke wala mtoto, baada ya kuanza naye uhusiano nikapata ujauzito na akafurahi sana na kutaka kumzalia, kweli ile mimba nikaibeba marafiki zangu wakawa wanashangaa sana jinsi yule kaka alivyokuwa ananitunza na kunipa fweza nyingi na wakawa wananiambia kweli umemuweka huyu kaka kwenye kiganja..


sasa ujauzito ulivyofika miezi saba kwakweli nilishangazwa sana kwa yule kaka kubadilika akawa anapunguza kunihudumia, nikimpigia mara apokee simu mara anipotezee yani nikachanganyikiwa nitafanyaje na huu ujauzito nikiwa nakaribia kujifungua.


sasa cha kushangaza siku nikaenda kula kwenye hotel ambayo huyu mwanangu huku tumboni anapenda sana tukale ndipo muudumu mmoja aliponiuliza "mbona shosti uhonekani, naona mzee anakuja na yule rafikiyo......" looohh nilihisi kama kumwagiwa maji ya bariiiiddiiii sikuamini niliyoyasikia.


nilipofika nyumbani nikampigia rafiki yangu kumuuliza akaniambia neno kwamba yupo "kazini anatafuta kama miye nilivyokuwa natafuta kwa huyo kaka" jamani nilihisi nimesikia vibaya, kweli mwanzo nilikuwa na mchuna yule kaka na wote walijuwa lakiini baadae nilivyopata ujauzito nikataka kutulia naye, kwakweli niliumia sana..(mashoga hawa na hivi anavyopenga kwa waganga nikajuwa ameshampuliza)



basi nikawa nimeshajuwa huyu kaka haniudumii kwani atakuwa ameshapewa maneno kuhusu miye na yule shoga yangu kwani alitaka kuniharibia miye na kujitengenezea yeye njia, basi sikutaka kumtafuta tena yule kaka nikijuwa kwakuwa anajuwa ninamwanaye basi ipo siku atamtafuta tu, japo mashoga zangu wengine wakaniambia niende kwa mganga sikutaka kwani kwanini nigombee.


basi nikajifungua mtoto wakiume na nikahama kutoka kwenye nyumba aliyoijuwa yule bwana na mpaka leo tunaendelea vizuri tu nasikia tu kwa watu kwamba wale wameachana wameshindwana na yule shosti anamwanaume mwengine sasa, mpaka leo hatujawahi kuongea.




RAMLA















1 comment:

  1. What goes around comes around. We c ulikuwa unamchuna, waachie na wenzio nao wamchune, wewe lea mimba. Kumbuka wanaume sio wajinga, ALIKUWA ANAJUA VYEMA KUWA UNAMCHUNA NA ALIBAKI KWAKO C KWAMBA ALIKUWA ANAKUPENDA! Laaah! Alikuwa anahitaji hiyo kuma tu. Tc girls, mpaka hapo ushajichafua tiyari na probability yako ya kuolewa ishapungua sasa.

    ReplyDelete