jamani kweli humu duniani kuna vitu vya kushangaza na vyakusikitisha, yani tumekuwa kama sijui wanyama ama nini nashindwa kuelewa na kitu mapenzi na upendo wa ukweli wengi wetu tumekuwa hatuna tena, kweli wewe unamuacha mwanamke wake siku yenu ya harusi kweli jamani hii si balaa......
kisa hiki kimetokea huko uswazi kwetu MABIBO..
jamaa mmoja alikuwa na mchumba wake msichana mdogo tu, mrembo ana nyamanyama yani kwa ufupi anavutia, akapata kaka mmoja naye huyo kaka pia anavutia kwa kweli ngoja nimpe sif a zake, cha kushangaza wakati wa uchumba wao walikuwa wanapendana sana jamani (kwa kuona kwa macho) yule mwanaume akija nyumbani kwa mwanamke na mappenzi tele na kwajinsi yule dada alivyokuwa anamzungumzia mpenzie tukiwa wote kweli utaamini walipendana sana.
wakaamua waoane wakavalishana pete ya uchumba na sherehe ikafanyika nzuri tu wakupombeka wakanywa gambe sana, kufurahia, basi baada ya mwezi tukaanza vikao kwa mwanamke vya sendoff na k/party, vikaendelea vizuri tukapata michango kwa sana mwanaume yeye hakuwa na vikao vya kuchangisha alisema gharama zote atazilipia mwenyewe.
siku ya k/party ikafika ilipendeza sana binti akapewa mazawadi tele, send off pia ikaja pia ikapendeza na wawili wale walivyokuwa kweli tuliamini wanapendana.
SASA KASHESHE LIKAANZA HAPA.....
harusi ilikuwa wiki moja baada ya send off waliamua kuziweka mbalimbali ili mwanamke apate muda wa kupumzika, hapo katikati kabla ya harusi yule mwanaume akaaga akasema anaenda mbeya ameitiwa kazi aliyokuwa amesha fanya interview kwenye kampuni kubwa tu hapa tanzania (sitaiweka hadharani) lakini angerudi siku moja kabla ya siku ya harusi.
siku ya harusi ikafika chaa ajabu yule kaka jamani hakurudi, kumpigia simu yake haipatikani, dada wa watu, ndugu zake, kila mtu amechanganyikiwa ikabidi harusi ife, yule dada akawa analia tu siku nzima mara simu jioni ikapatikana ya mchumba wake.
akiulizwa kwanini amefanya hivyo anasema hata akimuoa watakula hewa ? kwasababu hawa walikuwa waislamu nasikia waislamu unaweza kuolewa mke kama wewe haupo basi ndugu zake mwanaume wakamsihi wamuolee huyu dada akija atamkuta yani yule kaka alikataa katukatu na akasema atakayemuoa huyo dada ndiye atakayekuwa mke wake.
ikabidi harusi ife kwa aibu yule dada kahama mpaka mtaa, yule kaka kimya hata simu ya salamu kwa mkewe hamna zawadi na makorokoro yote imebidi akapange aanze maisha upya ya bila mchumba.
HII NI AIBU JAMANI...
No comments:
Post a Comment