Wednesday, July 6, 2011

USHAURI KUHUSU KIFUNGA KIZAZI...

kwakweli katika watu wenye vizazi vya karibu ni mimi mmojawao, kwenye ndoa yangu sasa nina watoto watatu na sasa ninatarajia kujifungua mtoto wa nne, kwa akili zangu za kibinadamu naona nimefika mwisho wa kuzaa na ninataka kufunga kizazi..

nimeongea hili swala na watu wazima wapo wanaonishauri nifunge na wengine wananiambia nisifunge kwani sijui MUNGU amenipangia nini huko mbele lakini jamani sasa ninamiaka 35 na hmana kitu ninachokiogopa kama kutoa mimba kwani kwa sisi walokole hiyo ni dhambi kubwa sana..

kizazi changu kutwa kipo wazi yani chakula kidogo tu mimi nishashiba, na nasikia ukizaa sana unazidi kuzeeka na ninasikia hizo njia za uzazi wa mpango zinasumbua sana ukiweka sasa nitafanyaje maana sitaki kuzaa asubuhi na usiku wala jumamosi na jumapili.

Halima

No comments:

Post a Comment