Tuesday, July 12, 2011

UGUMU WA KAZI YAKO ISIMNYIME MPENZIO RAHA...



jamani kazi tunazofanya sisi leo ni baraka kutoka kwa MUNGU haijalishi unafanya kazi ya kulipwa sana ama unalipwa kidogo cha muhimu mkono unaenda kinywani na unauwezo wa kujihudumia mwenyewe na kama unafamilia na unaihudumia hiyo ni vizuri zaidi, maana kunawenzako kutwa wanazunguka barabarani wakitafuta kazi japo hata ya kulipwa kidogo hawapati..





sasa basi ugumu wa kazi uliyokuwa nayo wewe kaka ama wewe dada isiwekisingizio cha kumyima unyumba mwenzako, ndio najuwa baada ya kazi mtu unakuwa umechoka na mwili kuuma basi rudi nyumbani kwako mapema ili upate muda wa kupumzika kama mama uhakikishe vitu nyumbani vipo sawa jinyooshe kitandani ili uupumzishe mwili hata baadae mwenye mamlaka nawe akikuhitaji uwenanguvu za kumparaha sio ndio visingizio vya kazi vinaanza utasikia leo nimeongea sana na wateja na kusimama pia basi nimechoka sijiwezi...



ama ndio kama baba utamsikia yani leo mikutano ilikuwa mwengi nimeongea sana nimechoka mno, ama nimezunguka hapa na pale ofisini kuelekeza watu kwahiyo nimechoka sana hata kukushika siwezi ebooo unachanganyikiwa kwani wewe ndio wa kwanza kuajiriwa??????


haipendezi jamani hebu muda wa kazi ubaki wa kazi na wa mwenza wako nyumbani ubaki wa kwakwe hata kama umechokavipi mtafutie mwenzako muda wa kumpa raha zake...sasa ukishindwa kumpa wewe akapate wapi?????

No comments:

Post a Comment