Thursday, March 31, 2011

NAMPENDA LAKINI WAZAZI WANGU HAWAMTAKI.....


mimi ni msichana wa makamu sijaolewa ila nimepata mkaka ninaye mpenda ambaye ni mzungu, japo mimi nampenda sana lakini wazazi wangu hawataki kabisa kusikia nikiolewa naye(wakidai ni bora nitafute mume muafrica na mtanzania mwenzangu kama nataka kuolewa)....

kwasasa mimi ni mjamzito na bado sijawaambia wazazi wangu kwani najuwa hawatafurahia, lakini mimi na mpenzi wangu huyu tumefurahi sana kujuwa tunaleta mtoto duniani, na yeye anataka kunioa ili tuwe pamoja katika kumtunza mtoto kasheshe inabaki nyumbani wazazi nitawaelezaje wanielewe???????

saa ingine nafikiria kutoroka tu na yeye tukaishi bila ndoa lakini sisi ni binadamu kuna leo na kesho itakuwaje tukigombana na nyumbani nimetoroka? jamani nitafanyaje?

1 comment:

  1. pole dear, mi hiyo imenikuta kwa namna flani hivi, na nilpokuwa na mimba niliambiwa hata kuitoa nikakataa. mimba ilipoendelea kukua wenyewe wakaandaa harusi. waeleweshe ndoa, mapenzi hujengwa na mapenzi si nani anakuoa.

    ongea na dada zako wakubwa ndo wawe wanaongea na mama na si wewe mwenyewe. ongea hata na rafiki kipenzi wa mama wataongea kikubwa yataisha. pole

    mama B

    ReplyDelete