Wednesday, March 30, 2011

MUME WANGU AOA MSICHANA WANGU WA KAZI KISA SIJAMZALIA MTOTO WA KIUME....

kama ni uchizi jamani basi nakaribia kuchizika, nipo kwenye ndoa mwaka wa ishirini sasa na nina watoto watano wote wa kike, mume wangu hafurahishwi kabisa na uzao wangu, sasa ameanza uhusiano wa kimapenzi na msichana wetu wa kazi kwa madai anaweza kumletea mtoto wa kiume...

mapenzi yao yamekuwa motomoto ndani ya nyumba yangu madharau naonyeshewa nje nje na huyu msichana sasa amebeba ujauzito anamlazimisha mume wangu waoane ili mtoto atakapozaliwa awe wa ndani ya ndoa ili aweze kurithishwa mali za baba yake...

anamdanganya mume wangu kwamba ameangalia na amekuta ana mtoto wa kiume basi mume wangu kawa kama kachanganyikiwa mapenzi kwangu hakuna na huyu msichana wa kazi dharau zimemzidi ambazo sijawahi kugundua anazo mpaka nashangaa amebadilika kama kinyonga, watoto wakimuuliza baba yao anawajibu mambo ya ajabu haelewi cha ndugu wala mshenga kisa ameambiwa ana mtoto wa kiume ambaye hana hata uhakika kama ni kweli ama mbinu tu za huyu dada kutafuta ndoa...

nimefukuza ndani ya nyumba lakini mume wangu ameniambia kama sitaki kumuona huyo msichana basi niondoke mimi na wanangu....

kweli jamani nikubali kumfanya msichana wangu wa kazi mke mwenzangu ama kweli niondoke maana hizi ni aibu mtu mzima kama mimi kudharauliwa na mtoto mdogo...

1 comment:

  1. Pole sana dada yangu kwa yaliyokukuta mi ushauri wangu usiondoke hapo kwani hapo baadae watoto wako ndo watateseka kumbuka umetoka mbali na mumeo mmechuma vitu pamoja leo mtu mwingine tu aje kukuaribia pia usali sana kwani yote haya yana mwisho kwa muweza wetu,uwe makini sana na huyo dada kwani anaweza fanya lolote na hata kama ukiondoka lazima mgawane vitu pasu kwa pasu ila mama ng'ang'ania ili watoto wasije pata tabu baadae kwani kama ndoa yako ni ya kanisani haiwezi vunjika kamwe.

    ReplyDelete