Sunday, March 6, 2011

MISHUMAA INAONGEZA RAHA KATIKA MAPENZI LAKINI.......................


mishumaa ni kiungo kikubwa sana katika mahusiano, haswa ukijuwa kuitumia vizuri, raha ya mashufaa hukufanya upumzishe akili na kuondoa mawazo pindi unapokuwa na mpenzi wako, na mishumaa huwashwa bila taa ndani ili mpate ile ladha ya mapenzi...

mishumaa sio ya aina yeyote inaweza kutumika pindi unataka kuliwazana na mpenzi wako, kuna mishumaa ya mapenzi yenye manukato na maua kama nilivyoonyesha maana hutaki kuwa katika mapenzi na kusikia harufu kali za moshi na utambi...

weka mishumaa bafuni wakati manataka kuoga, weka mezani mkitaka kula chakula kwa mapenzi, ama weka chumbani ukitaka kutoa penzi la kiutu uzima...

mishumaa inaleta ladha sana katika mahusiano nyumbani lakini pia ni lazima kuwa waangalifu maana mishumaa ndio chanzo kikubwa cha vifo, pale penzi litakapozidi ukasahau na kulala bila kuizima...

No comments:

Post a Comment