Monday, February 28, 2011

UNYANYASAJI HUU KWA WATOTO WA KIKE MPAKA LINI JAMANI??????

swala la watoto kuwa na uhusiano na wazazi ni jambo ambalo nimelisikia kwa mda mrefu, lakini mara nyingi ni ambapo baba anamtaka kimapenzi mtoto wake wa kike mimi binafsi sijawahi kuona ama kusikia mama anamtaka kimapenzi mtoto wake wa kiume...

jamani kina baba hivi mtafanya vituko mpaka lini????? yani wewe hujatosheka na mke wako, ukatafuta hawara barabarani, huyo naye hakukutosha ukamuingilia mpaka msichana wa kazi nyumbani naye ukaona bado hakutoshi mpaka sasa ukaamua kwenda kumuingilia na mtoto wako wa kumzaa mwenyewe!!!!!!!!!!!!!!!!!!

hii ni laana mbele za macho ya Mungu na ni aibu kwa familia, najiuliza inakuwaje mpaka wewe mwanaume ukamfwate mwanao na kumdharilisha na mara nyingi watoto hawa huwa ni wadogo ama kwa akili zako baba unaona pale ngoma bado mbichi kitu kimekaza kwa akili yako ya ujinga unapopata ile starehe ya kitu kilichokaza unajiona unafahidi sana cha kukufanya umuingilie kila mara mwanao....

sasa kama unataka vilivyokaza kwa nini humuelezi mkeo akahangaika????? kwani hujui kuna vitu kibao vinaweza kumfanya mkeo akajikaza najuwa wanaume wengi hamvifahamu lakini wamama wanavijuwa na kama hawavijui watauliza lakini tusitafute sababu kujiletea laana ya kizazi chetu kizima mbele za Mungu...

wababa haipendezi jamani.....

1 comment: