Monday, February 21, 2011

UDONDOKAJI VIBAYA WA KITOVU KWA MTOTO WA KIUME HUWEZA KUMSABABISHIA KUWA SHOGA????

Kwanza kabisa namshukuru sana Mungu kwa wema wake kwa kutujalia mimi na mume wangu kupata mtoto wetu wapili siku ya valentine day na safari hii ni wa kiume anaitwa Khreflo....

sasa basi kunajambo ambalo nimekuwa nikilisikia tokea nimejifungua watu wakiniambia ya kwamba nilazima sana niwe makini kwa kuchunguza kitovu cha mwanangu kitakapo dondokea yani kisimdondokee uumeni kwake kwani kwakufanya hivyo inaweza kumfanya baadae kutokuwa mwanaume kamili na kuwa shoga......

jamani hii ni kweli? kwahiyo mashoga inamaana vitovu vyao viliwadondokea ama hiyo ni tabia tu ya mtu? kwa anaye fahamu tafadhali naomba tuelimishane juu ya hili jamani maan ni jambo hatari na zito...

1 comment:

  1. hiyo ni imani potovu aina ukweli wowote kama ni kweli mbana watalaam hawazungumzii hilo wala dada usiwe na wasiwasi wowote wewe endelea tu kumlelea mwanao na kama huwamini jaribu kuwauliza watalaam ninamaana madaktari usikie watakuwambiaje

    ReplyDelete