Friday, November 5, 2010

MAMA MKWE ANANIFANYIA VITUKO KWASABABU SINA WATOTO....

jamani nilikuwa nasikia yakwamba wakwe wansambua haswa wamama sikuamini mpaka yalivyonitokea mimi yani mama mkwe wangu hana upendo kabisa na mimi kwasababu sijabahatika kupata watoto na mwanae...
akija kutoka kijijini ananifanyia vituko vya kila aina mara nikipita ananifyonya, mara mume wangu akirudi kutoka kazini anajichekesha kwake na kuchukuwa muda wake mwingi kuliko hata mimi, mara tukiingia chumbani baada ya muda nikatoka kwenda bafuni anafyonya na kuongea maneno ya kejeli jamani mpaka nimechoka...
imefikia wakati sasa anamkumbushia mwanae kuhusu mwanamke wake wa zamani labda ungemuoa yule ungepata watoto maaana huyu uliye naye anatumia tu vitu vyako bure haswa pale mume wangu anapo nipa hela yeye anataka kufa..
kwakweli huyu mama ananikalia kichwani nimechanganyikiwa kabisa, saingine natamani hata kumpiga sema tu ndio mama wa mwanaume ninaye mpenda... nisaidieni jamani

1 comment:

  1. Mungu aweza kumpa mtu watoto kumi kisha akamnyang'anya woote akabaki yeye kama alivyo. Hata yeye huyo mama mkwe mkumbushe kuwa watoto ni zawadi kutoka kwa mungu hajaamua tu kukupatia. Na ndoa yenyewe mbona hujaolewa siku nyingi za watu kuanza kuchungulia kama kuna watoto au hakuna?

    Na anajuaje kama huyo anayeambiwa mjukuu wake ni mtoto wa mwanae? Zaidi ya asilimia 60 wamebambikiwa watoto na wanawake upo hapo?

    ReplyDelete