Rosemary, mimi nimetolewa mahari na mchumba wangu ambaye tumekutana sio mda mrefu sana, kwa mapenzi tele niliyokuwa nayo kwake nikakubali tuanza mipango ya kuoana, mahari ikalipwa na pete nikavalishwa ndugu jamaa na marafiki wote wanajuwa ninataka kuolewa chakushangaza ni kwamba mchumba wangu huyu kutwa tukiachana anaonekana na wanawake wengine na pindi atakapokutana na rafikiyangu anayetufahamu ama ndugu yangu basi anajifanya kama hayupo pamoja na huyo mwanamke aliyekuwa naye wakati huo..
rafiki zangu wengine huniambia kwamba wamekuta gesti akiwa na mwanamke mwengine na sio mara moja ni mara kibao, na mpenzi wangu huyu ana bestfriend wake mmoja ambaye ni mwanamke na huyu dada na shangaa kwanini ananichukia mimi sijui anamtaka huyu mchumba wangu yani nimechanganyikiwa sijui niachane naye tu ama nifanyaje?
Rahma
JIBU,
Rahma kwanza hongera kwa kupata mchumba wa kukuoa na kumbuka ndoa sio mchezo wa kuigiza ukiitaka lazima ukubaliane na yote mabaya na mazuri, sio wakati wote ndoa ni raha, kuhusu mchumba wako mimi sikushauri uachane naye kama ucheche yeye sio wa kwanza na wala hatakuwa wamwisho kuufanya, na sio kabla ya ndoa hata baada ya ndoa kama akiamua atafanya tu cha muhimu amekuchagua wewe kuwa mke wake basi muache nitakupa msemo mmoja mume wangu huniambia "kuku wako mwenyewe manati ya nini" hao wanaume wanajuwa kabisa huku nje napoteza muda tu changu kipo ndani ambacho anakithamini ndio maana kutwa utawakuta leo na huyu kesho na yule kesho kutwa na mwengine lakini wewe hatakubadilisha milele wewe ndio wake mpaka kufa, basi achana na hayo mambo ya watu yasikuharibie ulichonacho mpende mchumba wako na usimuache..utaniambia siku
ROSEMARY
No comments:
Post a Comment