kuna mahali nimesikia kwamba kuna watu wengine pindi wanapopata ujauzito na kuzaa mtoto ambaye hajakamilika viungo vya mwili ama ametoka anamatatizo labda ya akili watu hawa huamini ya kwamba wake zao huwa wamelogwa........
wewe umeshawahi kusikia kitu kama hiki sehemu na je ni ukweli? kwa maana mara nyingi watu huwaficha kabisa watoto wao wenye ulemavu wasitoke ndani kisa aibu ama hata wasiseme kabisa kama wanahawa watoto ili waepukane na aibu....
na hawa watoto mara nyingi hukosa kabisa mapenzi ya wazazi na jamii kwa ujumla, na mara nyingi pia hawapati elimu bora kisa aibu ya wazazi wao..........
huku ni kumkomoa mtoto kwani wewe kama mzazi jukumu lako nikumlea na kushukuru Mungu amekupa kwani angeweza kukunyima kabisa, ni vigumu sana kukubaliana na hali ya mwanao akiwa hivyo lakini kama wazazi na jamii nzima hebu tuwajibike katika kuwalea ili hatakama leo hatutakuwepo tena wapate mwanga wa kujiendeleza kimaisha na Mungu atazidi kuwabariki...
No comments:
Post a Comment