Sunday, June 27, 2010

SHUGA MAMII.....

najuwa hilo neno nimeliandika kiswahili sana, lakini nimeliandika kama nilivyoambiwa huitwa, sasa basi kuna familia moja kuna kisa chan kunishangaza sana kimetokea ambacho nimeona haiwezekani mpaka nikiandike humu....
kuna kaka mmoja mwenye umri kama miaka (36) ameoa kama miaka minne iliyopita, bahati nzuri huyu kaka yeye anafanya kazi kama messanger kwenye kampuni moja ya kizungu hapa mjini, na mke wake ni mama tu wanyumbani na wamebahatika kupata mtoto mmoja......
wakati huyu kaka anafanya kazi, kuna boss wake mmoja wa kike ambaye ana umri wa miaka (50) akatokea kumpenda huyu kijana, kwa kuwa huyu kaka alikuwa hana hela na yule mama alikuwa na pesa sana akajikuta anapata tabu sana ya vishawishi akiwa ofisini alikuwa anataka kumkubalia ili amchune huyu mama hela lakini kila alipokuwa akimuwaza mkewe alikosa raha kabisa....
siku moja aliporudi nyumbani akamueleza mke wake kuhusu yule mama na jinsi anavyomtaka kimapenzi, na akamueleza jinsi yule mama alivyokuwa tajiri, kwa kweli ilikuwa vigumu sana na ilimuuma sana mke wake kusikia yale maneno yanayomtoka mume wake....
kwakuwa huyu kaka na mkewe hawakuwa watu wenye pesa basi akamshawishi mkewe amuachie tu amkubali yule mama ili amchune wapate kujiendeleza wao ukiangalia yule mama hana mme wala mtoto, anakaa peke yake kwenye jumba la kifahari huko masaki kwahiyo huyu kaka akaona hapa ndipo pakumalizia shida zake......
baada ya kumshawishi sana mke wake na akiangalia jinsi walivyokuwa wanashida huyu dada aliamua tu kukubali maana na yeye alitamani kuwa na maisha bora, awe na nyumba yake nzuri na gari pia...
huyu kaka akamkubalia boss wake, na kwa kufanya hivyo tu yule mama akamnunulia nyumba sehemu ya sinza, akampa gari na kila wiki akawa anampa hela ya matumizi nyingi sana, na yule kaka wala hakumwambia yule mzungu kwamba ameoa alimwambia tu kwamba anaishi na dada yake na mtoto wa dada yake....
maisha yakazidi kuwa nyookea wakapata gari la pili la mke wake, akamfungulia duka la nguo na salon kubwa tu, na mtoto wao akaenda shule nzuri hapa mjini na maisha kwao yalikuwa kama mbinguni, kwahiyo huyu kaka alikuwa anaenda kwa yule mzungu akitoka kazini kwenye mida ya saa sita alikuwa akirudi kwa mke wake......
matatizo yakaanza kuingia pale kaka alikuwa akirudi kwa mkewe, lakini anashindwa kumpa mkewe raha, mzee asimami kabisa kila akijitahidi bila bila, maana mzungu anamshughulisha mpaka basi, ikafika kipindi huyu mzungu akataka wawe wanakaa pamoja na huyu kaka, hapo ndio balaa ilipoanza angemwambiaje mkewe?
na huyu kaka alishachanganyikiwa na mali alizopata kwa mzungu na alitaka zaidi, basi akaamua kuhamia kwa mzungu na kumuacha mkewe, jambo ambalo mke wake lili mchanganya sana ikabidi aite kikao cha familia na kuwaeleza yaliyotokea, familia ilimshangaa sana na kusema hawana la kumsaidia kwani walishirikiana na mumewe kwahiyo akae tu peke yake kama mwanaume ameamua kuondoka.....
dada anasema umasikini umemponza, shuga mamii kamnyang'anya mume kisa mali, sasa ameachwa na mtoto na hiyo biashara ambayao haiendi vizuri kwasababu ya madeni na shule atashindwa kumpeleka mwanae, yani anajuta amechanganyikiwa kabisa ukimuona utadhani mgonjwa wa ngwengwe alivyokonda jamani....

SHUGA MAMII MMMMMHHHHH......

No comments:

Post a Comment