Tuesday, June 22, 2010

MAFUNZO KIPINDI CHA NDOA.....

jamii yetu ya leo haswa hapa Tanzania maranyingi watoto wao wa kike wanapoolewa huwaandalia kitu kinachoitwa KITCHEN PARTY hii ni kumfundisha mwanamke jinsi ya kukaa kwenye nyumba na kutunza familia yake na haya hufunzwa na wamama na wadada....
na siku hizi naona na wanaume pia wanafanyiwa sherehe hii ya kupewa maneno jinsi ya kuishi katika nyumba na wake zao na haya mafunzo pia hufanywa na wamama pamoja na wadada na kwenye sherehe hizi huwa hupewa zawadi za matumizi ya nyumbani...
lakini je tumeshajiuliza wanawake hufunzwa jinsi ya kumtunza mmewe, je tunajuwa wanaume hependa nini ama kwasababu mama zetu walitangulia kuolewa ndio maana watakuwa wanawafahamu wanaume kwa uzuri zaidi kwanini hizi kitchen party baada ya kufanyiwa na wamama wasifanye tena nyengine itakayoandaliwa na wababa ili nao wapate kuwafunda watoto zao mambo ambayo wanatakiwa kuyajuwa ya wanaume kwani najuwa ndoa nyingi sana zitadumu pindi wababa watakapo weza kuwafunda watoto wa kike kuhusu mume...
na kwavile vile watoto wa kiume wakafundwa na mama wakajuwa nini wanawake hutaka na kupenda kwenye nyumba, hii nadhani itapunguza idadi ya ndoa kuvunjika katika jamii...

HILO NI WAZO LANGU TU....

1 comment:

  1. Rose, asante kwa wazo lako, however kwangu mimi na kwa sasa hali iliyvyo kitchen party ni sehemu ya sherere, watu wale wanywe na zawadi tu, swala la mafundisho ni kwa wanandugu,ndo haswa watoao somo la ndoa na nyumba... nimefanyiwa kitchen party, kwa kweli yalikuwa mambo machache sana tena ni nyongeza tu niliyoambiwa na wanandugu nyumbani.. kwa kweli, kwangu mimi kitchen party ni sehemu ya zawadi.. hata kwa wanaume, elimu ya nyumbani ni bora zaidi.. kwa sisi tunaofuata misingi ya dini, dini zetu makanisani na misikitini kuna mada kabisa ya darsa za ndoa... kuvunjika kwa ndoa dada ni source ya mengi, wangapi wamefundwa kitchen party na wamekaa siku 60-90 tu kwenye ndoa zao?

    ReplyDelete