Thursday, June 24, 2010

HUYU VIPI JAMANI ANANISHANGAZA.....

ROSEMARY MIZIZI,
nipo kwenye ndoa mwaka wa saba sasa, na mwanzoni mapenzi yalikuwa motomoto kabla ya ndoa na alikuwa anaweza kunipa mapenzi ya ajabu na mapenzi tulikuwa tunafanya mara kwa mara sasa nina watoto wa tatu wawili wana miaka minne na mitano na huyu mdogo ana mwaka lakini huyu baba ukiacha kunipa mapenzi ili nipate ujauzito hanipi kabisa....
ikatokea kipindi akaanza kupunguza kunipa mapenzi kila akirudi yeye amechoka, mara akaaza kusingizia mara naumwa, mara sijisikii na visingizio vingine kibao sasa imefika kipindi kwa miezi miwili ananipa mara mbili tu heee....na hivyo mpaka nimuanze mimi
nikimwambia nampenda hanijibu, ama ananiambia nifanyaje sasa, nikimkumbatia ananisukuma pembeni, nikimbusu anatoa mdomo yani vituko kibao mpaka najisikia mpweke kwani nami nahitaji mapenzi kutoka kwake..
nikiwa namuhitaji ataanza kwa visa na kununa halafu baadae ndio anipe, sasa nikavumilia saana ikafika siku moja nikawa ofisini na siku hiyo nikawa na hamu sana na mume wangu, lakini nilijuwa hata nikienda nyumbani mpaka nimuombe na kumbembeleza sana inaweza kufika mpaka atake kunipa mimi huku hamu imeisha..
pale ofisini kwetu kuna kaka mmoja ambaye alitokea kunipenda sema kwasababu nilikuwa nampenda sana mume wangu sikumkubalia, na vituko vya mume wangu vilivyozidi kwangu siku moja ikabidi nimkubalie yule kaka (yeye hajaoa) kijana akanipa mapenzi tena kwa vile alikuwa anasubiri kwa mda mrefu akatoa ufundi wake mwanamke nikachanganyikiwa...
tukaaza uhusiani na yule kaka, mapenzi yakawa motomtoto na raha kibao ikafika wakati sasa mapenzi kwa mume wangu yakaanza kupungua, na kupungua na kupungua mpaka leo huyu kaka ameniteka kila kitu naishi na mume wangu kwakuwa nina ndoa naye nakulea hawa watoto wetu......
mume wangu sasa ameanza kujirudi, utadhani alikuwa amelogwa sasa ndio ameamkaa kwenye ile laana maana ameanza mapenzi motomoto mpaka nahisi labda atakuwa amehisi nina mpenzi nje, na hatakama ameamua kubadilika sidhani kama nitaweza jamani kumpenda tena kama zamani maana moyo wangu wote umeamia kwa huyu kaka wa ofisini kwetu...........
kila akijaribu kunipa penzi mimi hata raha sioni najikaza tu ili afike kilele, hata akinibusu sioni raha kabisa, ata akinikumbatia sijisikii mapendo kwake kila anaponishika nakumbuka vile vituko vyake alivyokuwa ananifanyia.......
nifanyeje ama niachane naye tu, awe ananiletea pesa za matumizi za watoto?
HELLEN.

1 comment:

  1. Dear Helen,

    Kwanza nikupe pole kwa hayo manayopitia na mmeo, ukweli ni kwamba wewe ndiye umefanya kosa kubwa zaidi, umetembea nje ya ndoa yako! Umesahau kuwa uliapa utaitunza ndoa yako katika raha na shida, sasa mmeo kabadilika na wewe ndiyo hivyo umeharibu moja kwa moja.Kwa ujumla hakukuwa na ushahidi kuwa mmeo alikuwa anatembea nje ya ndoa na wala wewe hujasema hivyo kwenye maelezo yako ,ila ninaweza hisi kuwa uliwahi kuwaza hivyo kuwa labda kwa kuwa anamaliza shida zake huko nje ndiyo maana alipunguza upendo kwako. Yawezekana ni kweli au hapana, ila ninavyojua mimi sisi wanaume (sijui kwa wanawake) kuna kipindi hujisikii kabisa kufanya mapenzi na mmkeo(mimi kuna kipindi ninafanya mapenzi na mke wangu na uume wangu unalala tukiwa katikati, sikwamba nina mpenzi nje ya ndoa na wala siwazi kuwa naye), si kwa sababu humpendi bali kutoka na mtindo wa maisha jinsi ulivyo, mwanaume ukisha pata kijitatizo kidogo tu, basi hata hamu ya kufanya mapenzi inaisha na hata hupendi kusemeshwa na mtu yeyote, ndiyo maana hata wakati ulipokuwa unamuambia unampenda alikuwa akikujibu vibaya, hiyo ni hali ya kawaida sana kwa mwanaume(waulize wanawake wengi walioolewa), nafikiri akina mama inabidi muwajue waume zenu, ukiona hayupo kwenye mood ya kuongea wewe achana naye hilo likiisha atajirudi. Sasa inawezekana kujirudi kwa mmeo siyo kwamba amehisi unatembea nje(ingawa hilo linawezekana pia, ila kama angehisi hivyo asinge jirudi kufanya mapenzi na wewe na kukupenda, angekufanyia vituko hadi ushangae mwenyewe) isipokuwa inawezekana ameona umeteseka sana kutokana na yote aliyokutendea au labda kilicho kuwa kikimsumbua kimeisha hivyo yale mapenzi yake kwako yakarejea. Namalizia kwa kusema hivi, dada yangu kosa umeshalifanya inatosha, muombe Mungu akusamehe kwani unazini, hiyo ni dhambi moja kwa moja ila ulifanya kutokana na hali ilivyokuwa, shukuru Mungu hadi sasa hivi mmeo hajagundua, akigundua hiyo ndoa inayokupa heshima sasa hivi haipo tena, wengi wanazitafuta ndoa hawajabahatika kuzipata(soma maelezo ya muomba ushauri mmoja hapo juu), ndoa yako ikivunjika usitegemee huyo kijana atakuoa, sana sana utaishia kujuta kuona watoto wako wakilelewa na mwanamke mwingine (maana mmeo akikuacha ataoa mwanamke mwingine)na utaishia kuitwa mwanamke aliye achika. Nakuomba sana, achana na huyo kijana maro moja, inawezekana hii ndiyo nafasi yako ya mwisho kabla mmeo hajagundua, rejesha mapenzi yako kwa mmeo,sahau yoet yaliyotokea miongoni mwenu watatu, mrejeshee mapenzi anayokupa mmeo na muendelee kama zamani, kama ulishayapoteza taratiiibu yatarudi! Zaidi ya yote omba sana Mungu ili mumeo isitokee hata siku moja akajua ulichokifanya! Nakutakia ndoa njema na yenye mapenzi tele! Obazega!

    ReplyDelete