tunajua ya kwamba karafuu ni zao linalonukia saaana na tena harufu yake ni nzuri sana sasa jamani kuna watu fulani siku hizi wanasema mwanamke ama mwanaume shurti uogeshwe na karafuu ama iliki ili unukie vizuri na kumvutia mpenzi wako haya mambo zamani yalikuwa yanafanywa na watu wa pwani lakini siku hizi kila kabila bibi lina manjonjo...
kwa mimi binafsi harufu ya karafuu ama iliki naipenda tu kwenye chakula lakini kwenye mwili wa mpenzi wangu wala sitaki kuisikia, na kwa wengine ambao wapo kama mimi wasiopenda harufu kuna vitu vyengine ambavyo vinaweza kuchukuwa nafasi ya karafuu na iliki kama udi wa vanilla, roses, ama hata wa lily flower.. manukato hayo unayachoma kwenye kifukizo na kuyaweka chumbani kwangu kuliko hiyo harufu kali ya karafuu (huu ni kwa upande wangu)...
na kabla mwanamke hujaamua kuweka hizo karafuu na iliki kumpendezesha mpenzi wako hebu muulize kwanza maana usije ukanunua ukaweka chumbani kumbe mwenzako badala aingie ndani anakimbia chumba, itakuwa aibu...
wote tunapenda chumbani kwetu panukie vizuri lakini wapenzi wetu huwa wana matatizo na harufu iwe nzuri ama mbaya wao kutwa na chafya, mafua mpaka utawaonea huruma...
kwahiyo tusijifanye tunaujua ufundi hebu kabla ya kumuwekea mpenzi mankodinkodi hebu tuulize tujuwe kipi kina faa na kipi hakifai....
No comments:
Post a Comment