Monday, December 31, 2012

SHUKRANI ZA 2012.....

1: Napenda nikushukuru wewe ambaye ukiingia ofisini asubuhi na mapema kabla hujaanza kufanya reports na majukumu yako ya kazi unafungua libeneke na kusuuzwa moro halafu unapata nguvu ya kuendelea na shughuli zako...Ahsante sana


2: Nakushukuru wewe ambaye unajuwa kabisa kwamba hili libeneke nilakitanzania halafu upo nje ya nchi unapojisikia kutuma au kupiga simu kuuliza jambo huangalii muda wa kupiga tanzania ni saa ngapi unajikuta unapiga hata saa kumi usiku na kuniletea balaa kwenye ndoa yangu..Ahsante sana


3: Nakushukuru wewe ambaye unajuwa kabisa mimi ni mke wa mtu na profile yangu inasema hivyo halafu unanipigia simu ya kunitongoza na kusema imeandikwa kwenye libeneke kwamba natafuta mchumba..Ahsante sana


4: Nakushukuru wewe unayeniandikia email kuniambia mambo chungu mbovu kuhusu mume wangu na anayofanya mtaani unapomuonaga ukae kujuwa yule ni kidume na ukitaka hata wewe atakupa ni makubaliano tu, na email zako hazinifanyi nimuache na hatutaachana na ujuwe ubavu wa kuniacha yeye hana mpaka nitake mimi mwenyewe..Ahsante sana


5: Nikushukuru wewe mume wa mtu ambaye ukitaka kutongoza mwanamke unaanza kusingizia kwamba nyumbani kwako kuna matatizo na mkeo hakupi kabisa unyumba na mambo kibao kumbe ni uongo mtupu..Ahsante sana


6: Niwashukuru mahawara wote ambao unapotongozwa na mume wa mtu unajitapa kabisa kwamba kaona mkewe hafai ndio maana kaja kwangu mwenyewe unajidanganya nakutoa machejo yote ukiwa na moyo utazidi kupendwa cha kushangaza mume wa mtu mwenyewe hana habari ya kumuacha mkewe unatumiwa na kuachwa..Ahsante sana


7: Niwashukuru wanawake wote wanaoenda kuloga wapate ndoa wakiwa hawajiamini kwamba wao ni wazuri na wanastahili kupendwa na kuolewa, unaloga halafu unapata mwanaume ambaye hata dalili za kukuoa anakuwa hana unarudi kwa babu umekasirika dawa hazifanyi kazi...Ahsante sana


8: Nakushukuru wewe ambaye umri umeenda, umeolewa una watoto na bado unatafuta serengeti boy wa kukupa mzunguko, kama unajijuwa wewe umeenda umri na mabwana zako ni umri chini ya umri wako hiyo ni yako nasema..Ahsante sana


9: Niwashukuru wanawake wote wanaoolewa kwasababu ya kutoa nuksi ndio maana ndoa siku hizi hazidumu watu hawavumiliani wala hawabebeani misalaba wakiudhiana kidogo wanaachana..Ahsante sana


10: Niwashukuru wame za watu wote wakitoka majumbani mwao wamevaa pete zao za ndoa halafu wakiingia mitaani zinavuliwa na kuachwa kwenye magari..Ahsante sana


11: Niwashukuru wame za watu wote ambao wakipata hawara mpaya usiku huo wanalala hukohuko mpaka asubuhi na wakirudi nyumbani wanasingizi walipata matatizo..Ahsante sana


12: Nawashukuru wame za watu malaya wote ambao wanapogundua au kuhisi wake zao wanaliwa nje wanawapiga na kuwafukuza nyumbani wakati wao wenyewe ni malaya mbwa kweli mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu..Ahsante sana


13: Niwashukuru wanandoa wote wanaotoka nje ya ndoa zao nakufika kwa mahawara zao wanajipinda na kutoa machejo ya mzunguko ambayo ndani ya ndoa hamna kabisa..Ahsante sana


14: Niwashukuru mahawara wote ambao wakikutana na wame za watu wanalia na kumsifia mwanaume kwa raha anazopata wakati mioyoni mwao wanajuwa wanaumizwa hakuna raha yoyote bali wanamuibia baba wa watu ukitoka hapo unamsifia sana kwakuwa unajuwa unaachiwa pesa nyingi wakati moyoni unamtukana..Ahsante sana


15: Nikushukuru wewe mume wa mtu unayewekwa mjini na mkeo lakini kutwa barabarani huishi mahawara wakati hata hizo hela za kulipia gesti umeachiwa na mkeo asubuhi za mishemishe mjini..Ahsante sana


16: Niwashukuru mahawara wote ambao wanajuwa wanatongozwa na mwanaume ambaye hela hana halafu wao wanachukuwa jukumu la kutoa hela zao na kulipia gest akapewe mzunguko..Ahsante sana


17: Niwashukuru wame za watu wote ambao wanaondoka nyumbani hela za matumizi hawaachi wakisema hawana hawajapata halafu jioni unampigia hawara unampa mzunguko na kumuachia hela ya matumizi..Ahsante sana


18: Niwashukuru wame za watu wote wanaopenda wanawake wazuri hapa mjini na kuwasifia uzuri wako na kuwatamani wakati wewe mkeo hata hela ya kujipamba humuachii nyumbani anachakaa kwa kulea nyumba na watoto..Ahsante sana


19: niwashukuru wake za watu wote ambao kisa kaolewa hataki hata mama mkwe aliyemtunzia huyo mumewe aje nyumbani kusalimia akisema kaolewa na mmoja sio na ukoo mzima..Ahsante sana


20: Niwashukuru watoto wote walio chini ya umri wa miaka mitano ambao kutwa wanalilia kulala chumbani kwa wazazi halafu ikifika saa saba baba akitaka mzunguko mtoto anaamka na kuomba maji na kumkuta baba juu ya kiuno cha mama na kuanza kulia anamuumiza mama halafu mzunguko unaisha katikati kabla ya kufika kileleni..Ahsante sana


MUNGU akipenda tukutane tena 2013....Gracias







Sunday, December 30, 2012

Shukrani..

Wapendwa napenda kuchukuwa nafasi hii kuwashukuru wote mlionitumia mail, kunipigia simu, BBM, Whatsapp kunitakia nipone haraka na kuniombea nawashukuru sana naendelea vizuri sana natumia dawa nilizopewa na ninazidi kumuomba MUNGU aniponye na huo ugonjwa.

Ahsanteni sana

Thursday, December 27, 2012

Uuuwwiiii...Naumwa

Wapendwa natumaini wote ni wazima naandika hii post leo nikiwa namaumivu sana mwanzo wa mwaka niligundua ninaukama mauvimbe kwenye ziwa langu la kushoto mama yangu akaniwekea appointment Ocean road nikaenda kuangaliwa kweli wakagundua kuna kama mauvimbe wakaniuliza kama bado nilikuwa nanyonyesha nikawaambia nilishamuachisha mwanangu wakanishauri niende Agakhan kufanya Ultrasound ya maziwa nikafanya wakasema hakukuwa natatizo lolote nikarudisha report Ocean road wakaniambia hakukuwa na tatizo lolote.

Sasa wiki mbili zilizopita nikaanza tena kusikia maumivu upande huohuo wa kushoto sasa mpaka mkono wa kushoto wote unauma nikijicheki mwenyewe bado naona kuna mauvimbe jumamosi iliyopita nikaenda kwa doctor wangu Agakhan akaniambia kesho nikafanye tena Ultrasound waangalie nikamuuliza kwani kama ni cancer inakuwaje akaniambia inakuwa inavimba na ugumu kama mfupa..

Leo nilivyoamka nikajishauri ngoja nijipime tena nikajipima nikagundua sasa kumevimba kitu kama kigumu au sijui ndio uoga ninahisi tu kukibonyeza kile kitu kama ndio nimetonesha ugonjwa yaani mkono wa kushoto unaniuma jamani sijapata kuona yani ninamaumivu hapa ndio najiandaa nirudi hospital kwahiyo leo sitapost kitu chochote wapendwa ila nitakapojisikia vizuri nitajitahidi kupost hata kwa mkono mmoja.

Ahsanteni na nawatakia weekend njema.

Kuvunja laana ya kitovu..

Najuwa kuna wamama wakwe wanamatatizo jamani lakini kwa upande mwengine hebu tuangalie tabu walizopata mpaka wakatutunzia hawa wame zetu leo tunaojitapa nao, kama tunavyojuwa ya kwamba unapozaa mtoto wa kiume hulali usingizi wiki nzima ya kwanza mpaka kitovu kimedondoka, maana unabaki unaangalia tu kile kitovu kisije dondokea kwenye uume wa mtoto na baadaye kumpa matatizo ya kutoutumia vyema uume wake.

Ikitokea kama mtoto wako amedondokewa na kitovu katika uume unajuwa cha kufanya wewe kama mama ama kama unamjuwa mama ambaye mwanaye kimemtokea hivyo unajuwa la kumshauri?

Juzi alikuja mama mkwe wangu (mama mkubwa wa mume wangu)  kwangu katika story nyingi sana tulizopiga za kuhusu maisha na jinsi wao zamani walivyoishi katika ndoa zao ikatokea tukagusia hilo swala mimi nikataka kujuwa kama kuna ukweli wa hilo swala na akaniambi ni kweli kabisa na yeye kuna mama ambaye ni ndugu yao anamjuwa mwanaye alidondokewa na kitovu umeni mpaka leo mzunguko hafanyi na kuzaa hajazaa wala hajaoa kwasababu kila mwanamke anayekuwa naye anamuacha hashughuliki kuna mwanamke anataka mwanaume wa hivyo.

Nikamuuliza ameshahangaika kwa tiba hospitalini ama kunywa dawa za kienyeji akaniambia ile haina tiba za namana hiyo mwanangu tiba yake no moja ambayo inawashinda wa mama wengi hata mama yake na yule kijana pia ilimshinda ndio maana yupo hivyo mpaka leo nikazodo kumdadisi kwanini na tiba yake inakuwaje???

Akaniambia tiba yake inafanya kazi mpaka kijana awe amekuwa na ameshajuwa mwanamke yupo vipi  kwahiyo bila kumwambia wewe mama mzazi unatakiwa uende chumbani kwako uvue nguo zako zote na ukae kitandani kama unamngoja baba aje akupe mzunguko ukiwa umelalia mgongo  ukiwa huna nguo kabisa umuite mtoto wako huyo wa kiume chumbani atakapokuja na kukuona ukeni akashtuka basi atashtuka moja kwa moja mpaka kwenye uume na ndio hapo ataanza kufanya kazi kama wanaume wengine.

Kwahiyo akishastuka tu unaamka unavaa nguo usibaki bila nguo tena mbele yake kwa muda tena akishtuka tu basi, kwahiyo mama wa yule ndugu yake yeye alisema kuliko mtoto wake aone alipotokea bora abaki hivyo ndio maana mpaka leo yupo vile.

Inasikitisha kwakweli lakini pia inahitaji moyo kufanya hiyo tiba wangapi wangeweza?? mimi kama inenitokea hivyo sitowaficha ningefanya ili mwanangu apone dunia ya sasa hivi heshima uume pesa nyongeza kama mwanaume hujui kujitumia vizuri unatupwa huko kwenye dustbin kwani ulisikia yeye kwao hali, havai, halali ndio maana kaja kwako???? kafwata heshima ya mwanaume huyo..

Wednesday, December 26, 2012

Kuna siku moja mimi na wanangu tulienda kumtembelea rafiki yangu mmoja nyumbani kwake, tukashinda huko siku nzima rafiki yangu huyu ameolewa na anawatoto wawili wakike na wakiume.

Kabla hatujaondoka kunakosa mtoto wake mmoja alifanya na mama mtu akawa anamkanya lakini hakusikia kutokana na hayo akachukuwa mwiko na kumchapa yule mtoto na baada ya kuchapwa kweli yule mtoto aliacha lile jambo alilokuwa anakatazwa kufanya na mama yake na chakushangaza watoto wangu walivyoona mwenzo anachapwa na mwiko wakaogopa sana na mimi moyoni nikafurahi ya kwamba nimepata kitu cha kuwatishia wanangu wakiwa hawasikii maana jamani watoto wangu ni watundu na kiburi ndio usiseme sijui wamerithi wapi.

Basi kuna siku mwanangu wa kike na yeye akaniletea kiburi nikamwambia msichana wangu wa kazi aniletee mwiko basi kusikia vile akaanza kuomba msamaha akilia hatarudia tena nikafurahi kweli kwamba nimepata kiboko yao huo mwiko sasa, cha kushangaza mtoto wangu wa kiume hata ukimtishia vipi hana habari na huo mwiko wako mpaka nikaanza kumchapa nao sasa akawa analia halafu mara nyengine anarudia tena kosa na mimi nikawa akirudia siku nyengine nachukuwa mwiko tena namchapa mpaka anaacha.

Siku moja nilikuwa nazozana na wanangu nje, sisi kwetu bwana ni uswahilini sana chezea mabibo na nyumba yetu ni ya wazi tu hamna geti kwahiyo kila unalofanya barazani kwenu mtu akipita anaona, anyways basi majuzi mwanangu wakiume kuna kosa aifanya na siku hiyo nilikuwa nimekaa nje na mke mwenzangu (mke wa shemeji yangu) nikamwambia dada lete mwiko nimchape pasua maana kwajinsi alivyokuwa mtundu mpaka tumemtunga jina la pasua.

Dada akanipa mwiko nikamchapa pasa kidogo akapita mama mmoja hivi akaniona nilivyokuwa namchapa mtoto wangu wa kiume na mwiko akanifwata na kuniambia mama khloe acha kabisa kumchapa mtoto wa kiume na mwiko!!!!!nikamuuliza kwanini akaniambia mtoto wakiume unapomchapa na mwiko unamvunja ngu za kiume!!!!!!!!eenehhee ndio jamani nilishangaa kitu ambacho wewe unaona ni adhabu kumbe kinaweza kikawa na madhara makubwa nikamuuliza na mtoto wa kike akaniambia haina madhara kwa mtoto wa kike nikamuuliza kwahiyo mtoto wa kike nguvu zikimuisha sio mbaya hakunijibu alichoniambia nisimchape mtoto wa kiume na mwiko..Makubwa

Haya mama kama na wewe ulikuwa na tabia kama yangu ya kumchapa mtoto wa kiume na mwiko japo kidogo atambue kosa naomba uache tena uache kabisa ni vibaya.



Msaada Tutani...

Shikamoo dada Rosemary,

Kwanza kabisa ningependa kukupongeza sana kwa nafasi ya kutuelimisha wanawake kupitia Mwanamke na Nyumba. Kwa kweli kama binti ambaye bado hajaolewa nimejifunza mengi mazuri ya kuniandaa kuwa mke na mama mwema.

Kwa kweli mimi swali langu ni dogo ila naomba nikuulize maana sijasikia ikizungumzwa mahali popote na ninahope wewe kama kungwi utakuwa na a unique perspective. Nina rafiki yangu ambaye tokea sekondari ya boarding alikuwa anapenda kusugua chuchu zake ili asikie raha ya kimapenzi. Hadi hapa alipo yupo chuo na ni bikira anayekaribia kuolewa ila anaogopa kama tabia yake ya kusugua chuchu zake itamuletea madhara kwenye ndoa. Naomba dada Rose unisaidie kumsaidia rafiki yangu ili tujue:

1. Je tabia yake ni ya kawaida kwa wanawake ambayo ni bikira wanapopata hamu ya kimapenzi?

2. Kama tabia yake ina madhara mbeleni kwenye ndoa afanyaje ili aache?

Nitashukuru sana kwa jibu lako dada Rosemary na ukipenda unaweza ukaliweka kwenye blog yako kwa njia yoyote unayoona itasaidia kuelimisha umati.

Ubarikiwe sana mama na heri ya Krismasi na mwaka mpya.

Wako,

Elizabeth





Monday, December 24, 2012

Nawatakia Xmass njema na mwaka mpya wenye baraka na mafanikio..kumbukeni hakuna kama MUNGU siku zote tukumbuke kumuweka mbele katika kila jambo la maisha yetu na hatakuacha kamwe..

Friday, December 21, 2012

Laana...

Wapendwa leo nataka niongee na wame zetu kama unajuwa wewe ni mume wa mtu hii inakuhusu, mume tambua kitu kimoja tokea ulipozaliwa ulikuwa unaweza kupata laana moja tu ni kutoka kwa mama yako mzazi ndiye aliyeweza kukulaani ulipokosea na akikunya moyo wake najuwa mnajuwa kwamba hakuna tena mafanikio hapo.

Baada ya kuoa laana nyengine ikaongezeka katika maisha yako ni laana ya mke wako najuwa wengi haya yamewakuta labda ni kwavile hatuwi wawazi katika mambo hayo lakini hakuna laana nyengine mbaya kama laana ya mke.

Wengi tumewaona kwenye jamii baada ya kuoa wakafanikiwa sana lakini katikati ya ndoa zao wakawadharau na kuwanyanyasa wake zao labda hata kuwafukuza na kuoa wengine na baada ya siku kadhaa wakaporomoka sana kimaendeleo wengine wakajikuta baada ya kuachana na wake zao wakaanza kuwa na wanawake tofauti nje wakajikuta wanapata magonjwa na wengi kupoteza maisha.

Tunapenda sana kuwachukulia wake zetu poapoa kabla hujamuoa mapenzi yalikuwa motomoto outings haziishi, mazawadi hayaishi na maneno ya mahaba ndio kila dakika lakini baada ya kumuoa hakunaga tena kitu kama hiko hapa nikiuliza lini mara ya mwisho ulimwambia unampenda mkeo wala hujui, nikuuliza hata kama unakumbuka siku yake ya kuzaliwa ndio hujui kabisa, na je lini hata ulimchukuwa mkeo na kumpeleka hata bar ya jirani ukamnunulia soda moja kama sio mnywaji wa beer ndio kabisa wewe kutwa na marafiki kwenye mabar mnyweee na mtafute na wanawake cha muhimu kwako unajuwa nikifika nyumbani nikitaka mzunguko yule mama atanipa na chamuhimu ninahela ya kumuachia kesho asubuhi hiko sindio cha muhimu kwake.

Kutwa mkeo alee watoto wenu, aende na yeye kutafuta riziki, arudi nyumbani wasichana wa kazi wamsumbue kichwa na kuzozana nao kuhusu kuweka nyumba sawa na kama hamna wasichana wa kazi akirudi aanze kufanya usafi na kuweka nyumba sawa, akupikie pamoja watoto halafu wewe unarudi saa tisa usiku aamke akufungulie mlango huo usiku akutengee na akae na wewe ule chakula na labda huli uende ukalale na labda usitake kulala ukataka akupe mzunguko hata humuandai vizuri ilimradi tu umemaliza shida zako kweli hii ni ndoa unategemea mkeo anapoamka asubuhi akiwa anasali atakuombea kwa mapenzi mema????? hapana  kuna kipindi mimi rafiki yangu aliniambia yani Rose siku nikiwa mjane nitafurahi sana kuliko kuishi maisha haya unajuwa unamume kumbe sio chochote wala lolote mateso tu.

Wazazi wenu wapo mjini au ndugu zenu mnao waamnini hata siku moja umeshawahi kumwambia mkeo tupeleke watoto huko kwa siku mbili tu ukamchukuwa mkeo mkaondoka hata hotel ya mjini tu au bagamoyo mkaenda mkiwa wawili tu mkaonyeshana jinsi gani bado mnapedana na mnamapenzi bado yanachemka kama zamani ni kazi na kulea tu ndipo kunawafanya msipate muda wa kukaa pamoja, mkitumia siku mbili kila baada ya miezi mitatu kuwa pamoja na kwambia huyo mama hata siku ukimkosea atajuwa ni shetani ama bahati mbaya maana bado unampenda na kumjali.

Hukujuwa hilo baba chukuwa ulitendee kazi huyo mama siku zote atakuombea na utafanikiwa sana kwakupitia maombi yake.

Chezea kufumaniwa weye...

  Wapendwa kwanza kabisa nawaomba radhi kwa hii picha najuwa ni mbaya lakini nimeiweka hapo ili nifafanue jambo moja ambalo huwa tunafanya tunapowafumania wake/wame zetu kwa bahati mbaya au nzuri hii ndio niliyoipata ya hivi karibuni na bado kabisa sijapata ya wanaume kufumania wake zao mara nyingi kilio ni wanawake kufumania wame zao.

Jamani usiombe ukafumaniwa kwanza ni aibu kubwa na pili huyu aliyekufumania anaweza akakutoa roho maana hasira alizokuwa nazo kwa wakati huo sio ya kuchezea yani mtu unakuwa kama unalishetani limekupanda kichwani unalotaka wewe ndio ulifanye na hamna hata siku moja likakupanda lishetani ya kwamba umemfumania mkeo au mumeo umchukuwe kwa mapenzi umrudishe nyumbani muongelee umsamehe maisha yaendelee, wee thubutu yani tena pale kama ndio kuna kiti ama hata jiwe kama unaweza kubeba yani chochote kilichombele yako unabeba na kumtwanga mtu na mara nyingi sana huwa wanawake ndio wanaopata tabu yani unapigwa wewe mwanamke uliyefumaniwa na mume wa mtu lakini muewe anamuacha kabisa na wakifika nyumbani wengine wanamalizia huko ugomvi mwengine akishabembelezwa anamsamehe ila ushari na ugomvi bado unabaki kwa yule mwanamke atamtafuta tu bado na kumfundisha adabu.

Mwanamke na hapa nataka niongee na wake za watu sipendelei sana kuongea na watu ambao hawajaolewa ama kuoa kwasababu wao bado hawajaujuwa uchungu wa mume au mke yale maumivu yake ya ukweli yanayochanganya mpaka mara nyengine mpaka watu kuuwana bado hawajayajuwa ila ni vyema wakawa pia wanasoma wakajiandaa na habari nzima ya ndoa wakaelewa wanachokiombea ni nini.

Wewe kama mke wa mtu cha kwanza kabisa nataka ujuwe nafasi yako katika maisha ya mumeo ya kwamba mpaka mumeo amekuoa wewe alishakuwa na wanawake wengi sana kwanini akakuoa wewe??? kwanini MUNGU hakumpa mke mwengine na sisi wake tunawajuwa sana wanawake wa zamani wa wame zetu tena wengine ndio tukipishana nao tunawapa vikumbo mpaka wanajuta ukijitapa wewe ndio mkewe kakuacha wewe kanioa mimi sasa kwanini mwanamke ukitikiswa kidogo unayumbishwa?????

Jamani mwanamke ukiolewa na baadaye mumeo aitongozwe na kupendwa nje shoga kutunza mume bado hujajuwa labda urudi kwenu ukafundwe upya,  hata kama akiwa ameokoka lakini kama ni mwanaume wa maana wanawake utaona tu wanajipitisha na kujigongesha mbele yake ilimradi tu wajitongozeshe sasa atakalofanya mumeo baada ya hapo ni kusudi lake..cha muhimu ni mwanamke umtunze mwanaume awe ng'aring'ari muda wote.

Unapomfumania mumeo kwamba anamwanamke iwe kwenye simu, au umemkuta live bila chenga shoga inauma lakini mwenzangu haiuhusu kuanza kujirusha roho kila mtu ajuwe kama umefumania malizana na mumeo chemba kwani wewe adhabu za wanawake huzijui ukawa unapayuka kama umemeza casset inahusu, wanaume hawapendi mwanamke mwenye maneno jamani wewe unapokuwa busy kumsema na kumpayaukia unampa nafasi ya kichwa chake kutokusikiliza wewe na kuwaza viuno alivyokuwa anapewa na huyo mwanamke unayemsema naye...hukujuwa chukua hilo

Kuna wanaake wengine washari jamani utapigiwa mpaka kigoma ukifumaniwa na mumewe na kutiwa aibu, lakini wewe mwanamke unapoenda na kumpiga na kumfanyia vituko huyo uliyemfumania na mumeo inasaidia nini??? kama uume kashaula kashaukatikia kashapewa raha kazikamua zote hata wewe nyumbani jana hukupewa sasa ukienda kumpiga na kumfanyia vurugu utarudisha yale masaa nyuma yale maraha aliyokuwa anampa mumeo uyarudishe kwa mumeo!!!!! 

Unajitapa atanikoma atakukoma nini na upinde mpaka wa nyuzi za kutahiriwa mumeo anazijuwa unachotaka kufanya ugomvi naye ni nini kwani yeye alijipeleka mwenyewe sehemu ya tukio akamvuta mume kwa nguvu na kumbaka?????? shoga wa kumkomesha ni mumeo utamkomesha vipi sio kwa kumnyima unyumba, sio kwa kuhama chumba kisa umegundua ni malaya na wala sio kwakulala mzungu wa nne adhabu zote hizo bado zitamfanya atoke nje ya ndoa.

Kuliko kumnyima unyumba basi adhabu yake mpe lakini kwa condom hakuna adhabu mbaya wanaume wasioipenda kama kulala na mkewe kwa condom ni adhabu kwakwe lakini utakuwa unajikinga na maradhi mpaka hapo utakapogundua mumeo ametulia kwakuwa namwaambia wanaume hutumia condom kipindi cha kwanza wakishamzoea mwanamke hawavai condom hao asikudanganye analala nao na condom, sasa muendekeze mfe watoto wabaki yatima wakizurura barabarani wakati serikali inatafuta majibu ya kuwapunguza wewe ukaongeze na wakwako.

Akikuletea vurugu kashtaki kwa wakubwa, lakini imefuiika sehemu mwanamke ukajisimamia wewe mwenyewe ndoa nyingi wamama wameambukizwa ukimwi kwakushindwa kujisimamia wenyewe kwa kuwa wanaheshimu ndoa zao na wame zao lakini matokeo yake wameathirika na kupoteza maisha na kuacha watoto wakiteseka..Jitambue na chukua hatua sasa usiwe bendera fwata upepo.



Jitambue....

Jamani wanawake na wanaume kuna mambo mawili leo nataka niongelee kuhusu kufumania wame/wake  zetu, kwanza kabisa mwanzo wa dunia wakati MUNGU alipomuumba adamu na hawa akawaweka katika bustani na kuwaamuru wale kila tunda kasoro la ule mti wa laana lakini sote tunajuwa ilivyotokea baadaye nini akaja shetani akamponza hawa mpaka akala lile tunda na siyo yeye tu hawa akafanikiwa kumshawishi adamu na yeye akala tuna na wakajikuta wote wamemkosea muumba wao ndio maana mpaka leo tupo hapa tulipo.

Kwanini nimewapa huo mfano nataka muelewe jambo ambalo linasumbua ndoa nyingi sana na kwasababu wanandoa wengi hawajalitambua ndio maana ndoa nyingi sana zinamatatizo na nyingi sana zinavunjika na nyingi sana hazina amani wanaishi kulea watoto tu na wengine hawalali pamoja wametengana vitanda, vyumba au hata kama wanalala pamoja basi ni mzungu wa nne.

Ukiwa kama mwanamke au ukazaa mtoto wa kike utambue jambo moja ya kwamba wewe unaweza ukawa katika mpango wa shetani mpango gani tokea siku ya kwanza wanaume wamekuwa ni wadhaifu sana kwa wanawake yani hata kama mwanaume ni hodari kiasi gani lakini hana nguvu za kupindua mipango ya mwanamke wamekuwa wadhaifu sana kwa wanawake.

Wewe kama mwanamke unapotongozwa na mwanaume ambaye kabisa unajuwa ni mume wa mtu mwenyewe unajisifia kabisa mkewe atakuwa hamtunzi vizuri ndio maana kanifwata miye tena unajisifu kabisa chezea miye..rubbish kabisa unajitapa bila kugundua shetani amekutumia wewe kumuharibu huyo baba kumtoa katika mpango wa MUNGU unaosema alichokiunganisha yeye hakuna wakukipangua kwahiyo kabla hujamkubalia huyo mume wa mtu ujuwe kama na wewe upo kwenye mpango wa shetani.

Au wewe mke wa mtu unapotongozwa pia nakutamaniwa na wanaume na wewe pia unakuwa katika mpango wa shetani kwakuwa huo sio ubavu wako ubavu wako ni mumeo lakini siku hizi tunajidanganya kwani inaandikwa usoni kama ninauhusiano na mumewe au mkewe haijiandiki leo lakini siku tukiwa katikahukumu ya aliyejuu ndio utaona itakavyojiandika na utakavyoumbuka.

kwahiyo mwanamke unapojitapa kuwa na huyo mume wa mtu au wewe mwanaume unapojitapa kuwa na huyo mke wa mtu kumbuka umeangukia katika mpango wa shetani wa kuharibu ndoa za watu na sio uzuri wako au hela zako zimekufanya umpate bali umempata kwa masaada wa shetani..jitambue sasa na ufanye maamuzi mema kila unapoishi katika dunia hii.


Wednesday, December 19, 2012

Chezea Jiji Hili...ukija na jembe utalima lami

Da Rose,

mimi ni msichana na ni mrembo pia nina elimu yangu namshukru MUNGU kwa kweli kipindi nipo a level nilikuwa na mwanaume wangu ambaye nae kipindi hicho alikuwa chuo tulipendana sana na baada ya yeye kumaliza chuo alienda nje kujiendeleza na masomo, aliniacha tz nikiwa bado namuhitaji.


nami baaada ya kumaliza shule nilijiunga na chuo cha sheria na baadae nikahitimu vizuri sana mwaka 2009 nikaja dar kwa ndugu yangu nikaishi nae japo kwa tabu maana huyo cousin wangu alikuwa si mtu mwenye famlia kwa hyo mara nyingi sana tukawa ni watu wa mitoko.

katikak toka toka zetu nikakutana na mbaba mmoja hivi.. nyote mnamjua maana ni mtu maarufu sana hapa dar, basi akanitongoza na mimi kwa kuwa sikuwa na mtu kwa kipindi kile nilimkubalia tukaanza mahusiano,hakunificha chochote aliniambia ana mke wake na watoto wawili, na ametokea kunipenda si unajua tena zetu watoto wa kike nikasema ngoja nijiweke angalau nivute nae muda wakati nasubiri wangu wa peke yangu.

basi tukaanza mahusiano rasmi na yule baba kusema kweli aliniomba mzunguko baada ya week moja tu yule baba si mzuri wa sura ila kweli alikuwa ananipa hela nyingi sana, akanitambulisha kwa marafiki zake , akanipeleka ofisini kwake, kila mahali nilifahamika, mimi sikuwa najua kudrive so alitoa gari yake moja ya kunipeleka popote ninapotaka pamoja na dereva wangu..... maisha yalibadilika sana nilinawiri na kung’aa sijawahi kupata mwanaume akanipenda kama Yule.

maisha yanasogea siku zinaenda dada mimi nina tako yaani nimeumbika haswa basi siku moja katikati ya mzunguko na yule baba akaniambia baby naomba nyuma nilishtuka sana maana mheshimiwa kama yule kuniambia neno kama hilo kwa kweli nilishtuka, nikamwambia hapana, akanibembeleza sana nikagoma.... ila ile kauli ilinitisha sana nikasema lazima nifanye uchunguzi nijue je ni tabia zake au alitaka kunipima mimi kama ni malaya.

basi siku moja tukatoka kwenda bagamoyo, kiukweli yule mzee nilikuwa nampagawisha sana akiwa amelewa penzi.

akiwa amelewa penzi tukiwa huko bwagamoyo nikachukua simu yake sijui hata ni kitu gani kiliniambia niifanye hivyo, nikaanza kuingia inbox na sent item kufika tuu kwenye sent item nakuta msg amemwandika mtu anaaitwa zainabu kuwa amemisi kumpa nyuma.


mimi kwa woga maana mzee mwenywe ana sukari na amelewa penzi nikachukua ile number nikaisave kichwani baadae kwenye simu yangu nikasema nitamtafuta huyo dada mpaka nijue habari za huyu dada.


Dada huwezi amini pamoja na pesa alizokuwa ananipa huyu mzee nilikuwa naugua magonjwa ya zinaaa kila week nipo hospital.

basi nilivyochukua ile number nikamtafuta huyo zainabu , si unajua mtu ukitaka lako utajitoa hata ufahamu ili uujue ukweli nikafanikiwa kukutana na zai ananishi mbagala, yaani kumuona tuu anaonekana malaya fulani hivi nikamchangamkia as if tulishaonana kwenye umalaya wetu nikajichetua na story za kimalaya.

kama mungu sijui au shetani yule baba akampigia zai nikiwa nae, zai kupokea simu akaniambia shoga ngoja nina kichwa naenda mara moja kariakoo kuna mheshimiwa fulani anapenda nyuma hatari, tena sijui hiyo nguvu anaitoaga wapi. na hapa itabidi nimpigie shoga(mwanaume) fulan hivi niende nae, maana anatakaga mwanamke mmoja mashoga wawili, au ngoja nimuulize kama leo atataka wanawake wawili na shoga mmoja.

simu ikapigwa wakaongea mwanaume akasema leo nataka mwanamke mmoja na shoga mmoja... basi nikamshukuru zai nikamwambia shongangu ukipata kichwa uwe unanishtua nikarudi home nasikia hadi kulia , hapo kumbuka ameshanipangia nyumba upande, naenda naye mzunguko kwangu, sikuwahi kumvalia yule baba condom, na alikuwa akija kwangu ki ukweli ananuka harufu ambayo mimi siielewi hata kidogo, na siku aliyonitamkia anataka nyuma ndio nikajua huyu anakujaga hapa akiwa amechafuka mavi, na baada ya kuongea na zai nikapata uhakika kabisa.

bs nikazidi kumchunguza yule baba, raha niliyokuwa nayo ya kuhongwa ikazidi kushuka siku hadi siku, siku moja nikamwita dereva wangu nikaongea nae nikamwambia aniambie tu ukweli kuhusu boss wake nikampa na laki moja yule dereva alitirirka jamani, mpaka nilitamani kufa.

mtu mheshimiwa mkewe mtu mkubwa tuu tra anafanya madhambi hivyo,dereva akasema hata hivyo kuna siku dereva wa boss alishindwa kuvumilia maana yule dereva alikuwa muislam swala 5 akawa anampeleka boss kwenye maeneo yake hatarishi siku akasema kama kazi ndo hii bora niache kabisaaa kwa hvyo akamwambia mke wa boss in and out.. kuwa mumewe anatembea na mashoga na biashara zake ni za kula nyuma.

mke wa mtu alichanganyikwa akaamua kupaki aondoke ila watoto wake akawaonea huruma so ile ndoa yeye na mkewe hawalali chumba kimoja huu mwaka wa nne.

dada kidogo nizimie nikajua kweli yule baba kama ndo michezo yake hii basi na gonjwa hatarishi litakuwa langu, nikakosa amani nikasema hapa lazima nirudi kwa cousin wangu nikamwambia kuhusu yule baba maana cousin wangu nilimwambia kuhusu huyu baba kunitongoza kunipangia na kunitaka nyuma ila kila nilikomba ushauri kwa cousin namuona hana cha maana cha kunishauri.

sasa maji yalipofika shingoni nikaenda huku nalia sana namwambia cousin yule baba ni mbwa anatembea na mashoga wenye majina hapa mjini.. cousin wangu akalia pamoja na mimi nikajua ananihurumia alichoniambia pole sana mdogo wangu nilishindwa kukuambia mapema kuwa yule baba hafai ni malaya mbwa hata mimi niliachana nae kwa tabia zake za kutaka nimpe nyuma.

mimi presha ikazidi kupanda, tena na cousin ametembea nae? na kwanini cousin hakuniambia mapema, nililia kwa uchungu sana siwez hata kukuelezea nikaanza kudhoofu nikapungua sana sina amani wala furaha, kumbuka yule mzee ndo alikuwa ananiweka mjini bado sijapata kazi,niliishi maisha magumu ya mawazo mpaka nikasema nitakufa.

siku ya siku mzee amempigia zai simu anataka wanawaweke wawili na shoga mmoja zai akaniambia nimfuate hotel fulani kariakoo nikasema naenda najitia nguvu mwenywe,kufika reception zai akaniambia njoo moja kwa moja chumba no 204.

Jamani wanawake wenzangu nilichokiona kule yule mzee tayari alishaanza kazi alikuwa anamla yule shoga kwa macho yangu nilishuhudia, yule mzee yupo busy wala hakuangalia mteja mimi nafananaje zai haraka haraka akavua nguo yule baba akaanza kumshughulikia na zai, mimi nipo nyuma yao, naona nazidi kuishiwa nguvu kwa tendo naloliiona pale.

nikasema kama noma na iwe noma shoga analalamika utamu zai nae alalamika ya kumuibia mhe wa watu mm nikampiga kofi la mgongo yule baba akajua ni mapenzi hakugeuka nikampiga tena ndo kwanza anallalamika utamu, nikamnasua cha nguvu zaidi mgongoni akageuka kutahamaki ni mm uso kwa uso na tukio mzee wa watu ana kama kilo 80 alidondoka mie huyo nikaondoka zaidi ananikimbilia mie natoka resi nalia nikavamia tax ya mtu nikaondoka zangu.


Pale yule baba aliponipangia nikahama siku ile ile, nikabadili na number zangu za simu nikaanza maisha mapya japo ya chini sana na yenye maumviu, kila mwanaume aliiyekuwa ananitaka nikakataa katu katu mpaka sasa hvi dada kuna kaka ananipenda ila mimi moyo wa kupenda tena sina kabisa.

Natoa hili ili na wadada wengine wanaopenda maisha ya mjini wajifunze kupenda maisha ya mkato ni vibaya na yanamadhara yake.






Monday, December 17, 2012

Hehe Heiya....

Asilimia kubwa ya wenye ndoa zenye umri wa miaka mitatu na kuendelea kwa utafiti nilioufanya karibia kila ndoa kuna wanandoa kipindi fulani walishalala mzungu wanne, ndio kwa nini nitakupa sababu zinazofanya wanandoa na  kulala mzungu wanne kwa wanaoishi pamoja bila ndoa hao siwezi kuwasemelea kwasababu kila mmoja bado anaficha makucha yake kwa mwenziye kwahiyo mara nyingi matatizo yao huwa sio makubwa kama ya wale walio kwenye ndoa.

Kwanza utakuta mwanaume anarudi saa saba, saa tisa au hata asubuhi kweli wewe mwanaume unategemea utamrudia mkeo saa tisa za usiku halafu akupe mapenzi motomoto na wanaume wengi wanasema kitchen party kwani hamfundishwi mumeo akichelewa kurudi umpokee na umkaribishe, kiukweli kabisa kiubinadamu wewe mwanaume mkeo akikurudia saa tisa usiku utampokea na kumpa penzi motomoto au kwasababu yeye ni mwanamke ndio anatakiwa awe mtumwa??? asiumie moyo asionyeshe kwamba anataka kuheshimiwa na kuthaminiwa??? hapana lazima utamkuta amekasirika tena mwengine hata mlango akufungulii urudi hukohuko ulipotoka lakini yule mstaarabu atakufungulia japo atakupa hata chakula ule lakini usitegemee ukitaka mzunguko utapewa kwa mapenzi na akikupa anatimiza wajibu wake kama mke lakini anamaumivu na uchungu sana, ndio maana wengine wajikuta tu hawataki hata kulala na wewe karibu bora ageukie upande mwengine.

Pili, wanaume wakishaoa huwa wanajisahau sana, yani wanaona kama umeshampata basi ni wako utamuonyesha mapenzi unapojisikia wewe cha muhimu ukirudi nyumbani kila kitu kipo sawa na ukitaka mzunguko upewe, hapana hizo enzi kama zilikuwepo zilikuwa za zamani wanawake siku hizi wamejanjaruka wanataka kupendwa, na sio kupendwa bali umuonyeshe unampenda, umpe muda wako, muongee utakuta wanandoa wengine hata muda wa kukaa na kuongea mambo ya kuhusu familia yao hawana haitakiwi hivyo maana mkiongea ndipo unapozidi kumjuwa mwenzio na kuona msimamo wake kwa familia yake, sasa hiyo attention mke anapoikosa ndipo anakuwa na maumivu moyoni anakuona unamchukulia poapoa na ikiendelea kwa muda mwanamke anajikuta anapoteza mapenzi na mumewe kabisa naye anajikuta hataki kabisa hata kuguswa na mwanaume unamkuta anageukia upande mwengine wakitanda.

Tatu, mwanaume usiombe matatizo yakatokea ndani ya ndoa yenu na mkashindwa kuyatatua sisi wanawake tunapenda kutunzwa kama yai matatizo mnaposhindwa kuyatatua katika ndoa wanawake wengi hutafuta sehemu ya kumalizia matatizo japo sio kwa mzunguko ni kwa maneno atatafuta mtu wa kuongea naye kuhusu matatizo yake ya ndoa na usiombe akampata mwanaume wa kuzungumza naye na huyo mwanaume akawa muelewa na kumsikiliza vyema na kumbembeleza mkeo sisi wanawake hatuna hisia za kuchezea eti huku unamzungusha mchana fatuma jioni unaenda kumpenda mkeo hapana mwanamke akiamua kuzungusha kwa john ataanza na kumpenda john na wewe baba nanihii mapenzi kwako ndio mpaka next time, akikolea na penzi la nje amini na kwambia ataishi na wewe kwasababu ya watoto tu tena wengine ndio mpaka vyumba wanahama akikuheshimu asipohama chumba atalala mzungu wanne.

Nisiwachoshe hiyo ni mifano tu michache ya kusababisha wanandoa kulala mzungu wa nne cha muhimu ninachotaka kuwaambia labda kama uliamuwa kuolewa au kuoa utoe nuksi sawa lakini kila ndoa ni mpango na baraka ya MUNGU hakuna anayeolewa kwa bahati kila mwanamke ametoka kwenye ubavu wa mwanaume kwahiyo ujuwe kama wewe ni mwanamke unamwanaume wako yupo sehemu na kama wewe ni mwanaume unambavu yako inatembea sehemu cha muhimu nikumuomba sana MUNGU amlete kwako na akuwezeshe kuishi naye kwenye shida na raha.

Arusha Mpoooooooooo...

Haya sasa baada ya kutoka Geita mwezi wa kwanza ni zamu yenu wana Arusha, Moshi na wote wajirani na hapo wadada mpo tayari kufundwa mambo yootee yanayohusu chumba chako wewe na mpenzi/mume wako.

Mwanamke unajiamini hii ni yako sio ya kuikosa njoo ukiwa umeshakula umeshiba upo tayari kuchukuwa maujuzi kwa kiingilio cha 20,000/= tukutane Penguin Resort Hotel - Sakina kwanzia saa nane na mafunzo kuanza rasmi saa tisa wala usibebe kinywaji tutakupa siye.

Mwanamke nyonga bwana njoo ujione mwenyeweeeeee..

Lipia nafasi yako kwa tigo pesa tu 0717 019320 utapewa number yako ya siri na hiyo ndio kiingilio chako hakikisha huisahau, tunafanya hivi kwasababu haya ni mambo ya ndani na hatutaki kumfurahisha kila mtu anayelipia ndio anayejifunza.

Chezea siye weye....

Kitanda cha NDOA....

Jamani wanandoa hivi kitanda chako unakijuwa vizuri? haswa wanaume ama kwa vile sio jukumu lako kutandika na kununua mashuka hujui kabisa kitanda chako kipo vipi wewe ukija umechoka ulale ukitaka mzunguko ukitumie lakini hukijui kabisa.. unajuwa ni godoro gani zuri kulalia unajuwa ni mbao gani murua ngumu za kitanda cha ndoa, mashuka je unajuwa kama kunamashuka yana maana yakiwa kitandani..hehe heiya ndio maana mwakani MUNGU akipenda nataka nifunde wanaume na wanawake kwa pamoja ili mengi myajuwe.

Sharti kuu la kitanda cha ndoa lazima ulale bila nguo yani mtupu kama ulivyozaliwa kwa waliofundwa haya wanayajuwa lakini kwakuwa ndoa za siku hizi tunazichukulia poapoa tu wanawake hawataki kabisa kufundwa kabla hawajaolewa wanafanya tu wanavyojuwa wao na wayaoangalia kwenye tv wakidhani hayo ndio maisha wakati mwanamke mweusi wa kiafrica unatofauti nyingi na mahaba tele unayotakiwa kuyafanya chumbani ukijitambua.

Kitanda cha ndoa unatakiwa ulale bila nguo labda kwa heshima ya watoto kama wale wangu ambao wao chumba cha baba na mama ni kama chao ndio unavaa kitenge ukijifunika ili hata wakiingia ghafla umesahau kufunda mlango wasione walipotokea lakini ikifika wakati wa kulala chumba kikiwa kimefungwa kitenge tupa huko.

Kitanda cha ndoa mwiko kulala mzungu wa nne, yani wanandoa mimi nashangaa unalala na mumeo mzungu wa nne halafu iweje nitaandika mada kuhusu madhara ya mzungu wa nne, unatakiwa kile kitanda mlale hata kama hamuongei mmegombana lala tu wote mmegeukia upande mmoja hata kama hamtashikana usiku kucha lakini usiruhusu kulala mzungu wa nne kwenye kitanda chako cha ndoa.

Wanawake wengi wanapoolewa hata mimi nikiwa mmoja wapo unapewa godoro, unalijuwa maana yake ya kwamba umeshakuwa nenda kaanze nyumba yako na wewe ukifika sio lile godoro kisa mnachumba cha wageni ndio ukalipeleke kule hapana, lile godoro unatakiwa mlalie nyie, kama umeolewa na mumeo alikuwa anagodoro lake utalitoa na kupeleka chumba cha wageni halafu lile ulilopewa ndio utandike kwenye kitanda chenu mlalie hiyo ndio maana ya lile godoro yani mmeanza upya katika kila kitu mpaka kulala.

Kama ulikuwa hulijui chukua hilo...




Msaada Tutani...

Dada Rose, na wote mnaoingia humu mimi ni mwanaume nimeoa na ndoa yangu inamiaka sita sasa mimi na mke wangu tumebarikiwa kupata watoto wawili wakike na wakiume, ninamiezi miwili sasa dada naishi nikiwa sijielewi nimeona nikuandikie hapa pamoja na wengine mnipe ushauri nini cha kufanya. Miezi miwili iliyopita siku moja mke wangu alilalamika anaumwa na kweli alikuwa sio wa kawaida anatapika na kuishiwa nguvu kabisa ikafikia mpaka akawa anapungua sana kila nikimshauri alikuwa ananiambia ningoje ataenda tu hospital akizidi kujisikia vibaya na kweli kunasiku mpaka akashisi kuzimia ndipo aliponiambia nimpeleke hospital. Tulipofika akapimwa malaria na typhoid akawa hana lakini akawa anaishiwa nguvu ikabidi wamlaze ili wamfanyie uchunguzi zaidi baada ya uchunguzi doctoa akaniita asubuhi niliyoenda kumuona mke wangu na kuniambia anamazungumzo nami ndipo aliponiambia mke wangu alikuwa ameathirika ana ukimwi. Rose sitakaa kusahau nilipoyasikia hayo maneno niliishiwa nguvu,nikataka kupiga makelele lakini doctor aliniambia nichukuwe taarifa hizo kijasiri. nilikuwa sijui ni namna gani nitaenda kuongea na mke wangu na pia nikawa nashauku ya kujuwa afya yangu maana kama mke wangu ameathirika basi na mimi nitakuwa nimeathirika tutawaachaje watoto na bado wadogo, sikumwambia kitu mke wangu siku hiyo nikaamua kwenda nami kupima chakushangaza sikuwa nimeambukizwa sikuamini nikarudi kwa yule doctor akaniambia hilo linawezekana kwamba nisubiri tena miezi mitatu ndio nipime. mke wangu sasa alianza kupata nafuu ndipo yule doctor na mimi tukakaa naye siku hiyo na kumueleza ukweli kuhusu afya yake lakini hatukumwambia kama mimi nilipima nikawa sina. alipatwa na mshangao na huzuni akawa kama anataka kuzimia akapewa husia wa kuishi na huo ugonjwa na vitu vya kula pamoja na kuanza kutumia dawa siku hiyo tukaruhusiwa kuondoka kurudi nyumbani. ni mwezi wa pili huu sasa sijamgusa mke wangu, sijamwambia kama nimepima sina maambukizi, hatujaongea amepataje na alikuwa na husiano na nani yani sijielewi nini cha kufanya Rose nipo tu nahisi kuchanganyikiwa sijui jinsi ya kuongea ili nisiwe na jazba sijui kwakweli naombeni mnisaidie.

Victor

Sunday, December 16, 2012

Aaaahhhhh Mama Mkwe wee....

Natumaini wote humu ndani ni wazima jamani, weekend ilikuwaje majumbani wote wazima namshukuru MUNGU kama kila kitu kwenu ni sawa hata mimi kwangu kila kitu ni safi kabisa.

Leo jamani nataka niongelee swala la mama wakwe na hii iwaendee wote mliokwenye ndoa na mnaotaka kuingia kwenye ndoa haswa wanawake, jamani kuna wanawake wengine vichefuchefu yani jamani kisa yeye kaolewa na huyo mumewe anajiona yeye ndio yeye mumewe amsikilize yeye na wengine wanakataza hata wame zao kuwa na ukaribu na mama zao kama zamani.

Kumbuka ni huyuhuyu mama ndio aliymbeba huyo mumeo miezi tisa tumboni, alipomzaa hakulala kwa amani wiki ya kwanza kabla kitovu kudondoka anakesha ahakikishe kitovu kisidondokee umeni kijana akaja kukosa nguvu za kukupa wewe raha, akamtunza mpaka akasoma akakuwa kijana akalishwa kapendeza ndio ukamuona na kumpenda wewe sasa kwanini wewe usimpende mama mkwe wako..INAHUSU

Tena utamkuta mwanamke anampiga kikumbo mama mkwe wake na maneno kibao akija kuwatembelea nyumbani jamani hata MUNGU hapendi hebu tujaribu kuwapenda hawa wamama tuone kama ndoa zetu hazitakuwa na baraka na amani tele.

Natambua kuna wa mama wengine wanagubu tena kubwa lakini akifanya gubu jitahidi kumpenda na kumuheshimu usitukanane naye na kumfanyia vituko kama mke mwenzio haipendei kabisa..

Sikukuu ndio hiyo yaja hebu mnunulie mama mkwe wako hata tenge la wax bubu kama huwezi kumnunulia wax jifanye tu umempelekea zawadi uone kama hatafurahi na umshukuru kwa kuwa mama mkwe wako na kukupa mumeo, shukrani watafurahia na kujiona ni wamuhimu sana katika maisha yenu.


Thursday, December 13, 2012

Mwanamke tepetepe.....

 Jamani wanawake na kama wewe mwanaume unasoma hapa mweleze kabisa mkeo au huyo mchumba wako uliyenaye jitie fundi saa kukorokochoa kila tundu ukamueleza mke wa mtu akafanya haya ukamletea balaa kwenye ndoa yake maana mimi siwapendi nyie mnaojifanya mnakula wake za watu halafu mnajifanya mafundi hodari eti kuliko mumewe mbafu kabisa unadhani unaubavu wa kumuachanisha na mumewe shida tu na maumivu ya moyo ndio yamemfanya atoke nje ya ndoa ngoja mumewe aanze matunzo mema uone kama kwako atarudi...Anyways ngoja nirudi kwenye point.

Wewe mwanamke kungu unazijuwa??? hata kusikia pia hujawahi sikia makubwa basi kama hujazisikia shoga hii dunia sikuhizi nyengine mwanamke lazima uwe wa kileo haswa kwenye mambo ya chumbani juzi katika kufunda tukawafunda kwamba kuna wanaume wanakata viuno chumbani mnabaki mnashangaa unashangaa nini kwani umesikia shoga yule hapana raha hizo kijana anapata mpaka anajikuta na yeye anakufwata kwenye pindo zako ukienda kulia na yeye yumo kushoto yumo basi ilimradi wote mfurahie....tuachane na hilo

Mwanamke kungu ni muhimu sana, na sio ndio ule kila siku kwasababu ndio umelijuwa, kungu unaila siku moja kama unajuwa kabisa siku hiyo wewe na mumeo mpo pamoja siku nzima yani hatoki kabisa au hata kama atatoka atarudi mapema kungu inakusaidia macho mtoto yanarembuka yanakuwa nyoronyoro sio mtoto wa watu kila siku unamtolea mimacho mikavu kama umebanwa na mlango wewe mtoto wa kike jicho limekutoka kama ngumi ya mtoto mchanga..Inahusu 

Kungu pia inasaidia kulegeza viungo yani unakuwa mtoto mwepesi unajisikia kabisa baada ya muda fulani ukishakula na chamuhimu wanawake kungu zinaleta hamu ya mzunguko, ndio ukila zile baasi unapata hamu ya kwenda mzunguko mtoto unakuwa tepetepe baba akija wala hatumii muda mrefu kukuandaa maana kuna wanawake wengine mwanaume akikuhadithia unataka kulia mwanaume kukuandaa mpaka atokwe jasho inahusu...kama ulikuwa hulijui chukua hilo 

Japo kungu inakauchungu fulani hivi ndio maana watu wanaitengenezea na kitu kingine kama kashata, kama uji mliokuja kufundwa mwezi wa kumi mlipata kunywa uji wa kungu nadhani mliufurahia nitautengeneza tena MUNGU akipenda wakati mwengine.

Sasa shoga mimi kungu ninazo za pakti na zimechanganywa na maziwa yani kungu ya maziwa..miye napenda ladha bwana na ya maziwa ndio zaidi basi shoga kama unataka hizi kungu za maziwa nipigie unitafute nikupe 3,000/= yako tu number yangu hiyo hapo juu..

Na mambo yakuniambia upo mjini unataka nikuletee kungu moja koma..sitaki kabisa kama mnachukuwa nyingi ndio nitakuja kama hiyo moja unifwate nikupe..

Am Back...

Jamani niliwamisije sasa hii siku moja na nusu, kweli nimeamini maisha yangu sasa yapo kwenye blog daima, uuwwiii yule kaka alivyoniambia naweza endelea nikamwambia yessuuuu ulijuwaje aisee maana nilikuwa napata tabu sana..hehe heiya chezea mchaga miye

Naanza kutiririka sasa....

Tuesday, December 11, 2012

PING!!!!!!!!!PING!!!!!!!!!PING!!!!!

Wapendwa wangu natumaini wote ni wazima siku hii ya leo napenda kuwataarifu kwamba blog ipo katika matengenezo ili kuifanya izidi kupendeza zaidi na iwe ya kisasa nawaomba mnivumilie kipindi hiki wakati inafanyiwa ukarabati tukirudi mwendo ni uleule...Ahsanteni na nawapenda wote.

Tahadhari Wazazi......

Hivi karibuni vyombo tofauti vya habari vimeripoti kugundulika kwa mtandao wa kuiba watoto baada ya kubainika kuwepo kwa nyumba inayotumika kuhifadhi watoto wanaoibiwa jijini Dar es Salaam.

Watu hawa wanawafuata watoto shuleni hasa saa ya kutoka na kufanya wanawajua, na wengine kufanya wanawasaidia kuwavusha barabara na baada ya hapo kuwaahidi kuwapa hela na vitu vingine.Wanawachukua watoto na kuwapeleka kwenye nyumba hiyo na kuwafungia humo.

Hadi sasa haijafahamika wanawafanya nini baada ya hapo, na wala watu hao hawajakamatwa bado.Hivyo wazazi tuwe makini katika uangalizi wa watoto wetu hasa ukiona muda wa kawaida wa mwanao kurudi nyumbani na bado hajarudi.

Pia tuwafundishe watoto kutokukubali kuchukuliwa na mtu yeyeto ambaye hajawahi kumwona hata kama atamwita kwa jina lake.

Msaada Tutani....

Habari,

mimi ni mwanamama nina mtoto mmoja. nimeolewa ndoa ya serikali kwani mimi nilikua muislam na mume wangu mkristo. tunaishi Morogoro na ndoa ina miaka 7 sasa. tulipata ushauri wakufunga ndoa ya katoliki ili mume wangu aweze kujumuika na masuala ya kikatoliki na mimi nibatizwe nimekubali.

kabla hatujafunga ndoa hiyo ya kanisani, tumekua na kutoelewana kwa muda sasa..Mume wangu si muajiriwa anafanya biashara ambazo ni za wazazi wake kwa maana yeye ni msimamizi na anapata kiasi kidogo cha pesa kwa ajili ya sisi yaani mkewe na mtoto. mimi nimeajiriwa ila sina kipato kikubwa. kwakweli wazazi wake wameshikilia maamuzi ya mume wangu na inafikia hatua mipango tunayopanga haiendi shauri ya hilo.

mimi ndo nalisha familia, na majukumu mengi sana. sasa mtoto ameanza shule hata ada hatoi. pesa yote inaenda kwao na yeye ana madeni kila siku. nilimshauri aache hiyo biashara waajiri mtu wa kusimamia ili yeye atafute mtaji au kazi yoyote ili awe na maamuzi ya pesa yake tujijenge kama familia pia haafiki hilo suala kwamba yeye lazima afanya hiyo kazi.

maisha hayana raha, sasa mimi ninapata wasiwasi je, nikifunga ndoa hiyo itakuaje na naona kama muelekeo haupo wa yeye kutujali sisi. na huwa natamani hata niachane nae nilee mwenyewe mtoto maana ni mzigo kwani ndugu zake nawalisha mimi pamoja na huduma nyengine.


naomba unishauri kabla sijatumbukia humo. tafadhali nishauri na unaweza kuipost wengine washauri pia.



Clare!

Monday, December 10, 2012

Chezea kinywaji mlipuko weye...

Hehe heiya hapa bwana ndio wanawake wote waliokuja kufundwa walipochanganyikiwa, bwana wanawake kweli mambo mengi hatuyajui basi ukiona wanavyofundwa wanavyoshangaa yani mpaka unasikia raha, waliposikia kuhusu champaigne je uuwwiiiiii...ni hivi

Unapokuwa kwenye mzunguko na mwenzio hii style inapendeza kama mmekaa style kati ya hizi mwanamke akiwa chini (kifo cha mende) ama chuma mboga kama wenyewe waswahili tunavyooita huku ukiwa unampa mwenziyo maraha ukikatika taratibu basi pale unapoona anatoka sasa wewe mwanamke unatakiwa ukaze kuta za uke wako bila kuachia unapavuta ndani mpaka atakapomaliza kutoka kabisa yani usiachie katikati ukiachia utakuwa hujafanya linalotakiwa.

Baada ya kufanya vyema bila kuachia utamsikia mwanaume wako anapiga kelele sana sio kwa maumivu bali kwa raha anazozipata maana utakuwa kama unamkamua shahawa zote na usimuachie mpaka atakapotaka kutoka mwenyewe baada ya hapo cha kwanza kufanya ni kulala usingizi mzito sana na usishangae akishindwa kurudia tena mzunguko siku hiyo hata wiki nzima maana ile shughuli sio nyepesi jamani.

Wanawake waliojaribu hii wanasema wataifanya sana hii pindi wame zao wanaaga kwenda safari maana anauhakika hatazungusha wiki nzima na wengine waliojaribu wamenipigia simu na kutoa shukrani zao maana hawajawahi sifiwa kama walivyofanya style hii ndio nikagundua nahitaji sana kufunda wanawake naamini ndoa nyingi na mahusiano mengi ya halali yatazidi kudumu mwanamke unapokubali kujifunza na kumfanyia wako wa halali.

Hii ni picha moja ambayo niliruhusu hawa shoga zangu wanipige nilipokuwa nawafunda kukata kiuno style ya chuma mboga..hehe heiya mama wee shanga zangu nazo hazikutaka kujificha mpaka zijitokeze zionekane..mwanamke kiuno bwana mengine yote matokeo.

Na siyo ukizungushe kama mcheza shoo ukaja kukata uume wa watu au kuuvimbisha kiuno cha kitanda ni taratibu utamsikia tu mwenyewe anamaliza ahsante kila ukipiga kona..chezea siye weye huku matendo tu hakunaga maneno maana watu wananogewa mpaka nguo wanavua kweli hakuna starehe na utamu zaidi ya utamu wa kitanda.

Karibu na wewe wakati ujao

Sunday, December 9, 2012

Kama ni tamu naupenda, Kama ni ladha nailamba.....

Shoga sasa mafuta mengine muhimu ya chumbani ni mafuta ya mchaichai..ndio machaichai huohuo tunaopikia kwenye chai zetu kutupa ladha sasa mafuta yake ndio muhimu shoga.

Mafuta ya mchaichai yanasaidia kuleta nyege..ndio jamani kunawanawake wengine yani kupata hamu ya kwenda mzunguko ni ishu kubwa sana na hii jamani sio kawaida maana MUNGU aliumba liletendo liwe tamu yani tamu zaidi ya asali sasa kama wewe huna hamu nalo basi ujuwe unamatatizo ama kama wewe mpaka upewe mzunguko kijana wa watu afanye shughuli kubwa basi ni matatizo kisa cha kumnyima raha mtoto wa mwanamke mwenziyo nini nini kijana mpaka akifikiria kukupa mzunguko akabebe chuma kutengeneza pumzi inahusu.

Shoga chukuwa hii utachukuwa mafuta yako ya mchaichai kwa siku utakunywa kidogo tu mara tatu na kama ukiamua kupaka pia upake chini ukeni kidogo tu jamani kama wewe huna mwanume wa kueleweka tusipeane lawama ukaja pata nyege na kuparamia waume za watu raha ya hii kitu unywe siku kama ya ijumaa au jumamosi asubuhi upo ndani na mwenzako unamkatikia mpaka mwenyewe anachanganyikiwa utaona mtu anatetemeka tu kwa maraha kama anadegedege..hehe heiya chezea miye weye.

Jamani kama unahitaji na haya mafuta nipigie 10,000/= 

Namshukuru MUNGU tumemaliza salama kufunda kwa mwaka huu kwa wana wa dar tukutane tena 26/4/2013 MUNGU akipenda mimi kungwi wangu wawili na kungwi mpya tutamleta kujifunza mengi tena jamani huyu kungwi mgeni anamambo namjuwa miye kwasababu kashanifunda nafanya naye kazi yani jamani mimi ninamakungwi nikianza kuwapanga wanafika morogoro lakini haya yote ili mimi na wewe siku zote tuwe juu katika mahusiano yetu.




Hehe heiya chezea vitunguu swaumu weye...

Haya sasa mashoga wote mliokuja kufundwa nadhani mnakumbuka mlivyofundwa vyema kuhusu mafuta ya vitunguu swaumu..

Unaambiwa mwanamke unavyokuwa kabla ya kutolewa bikra unakuwa unanyama ukeni ambazo zinakuwa zimekaza uke ambapo mwanamme akiingia anasikia raha za ajabu lakini pindi pale mwanamke unapoanza kukutana na kujaamiana mara kwa mara zile nyama kwasababu ya msuguo zinakuwa zinaisha na hata kwa kuzaa pia pale tunapokuwa tunzaa watoto mara kwa mara haswa kwa njia hii ya kusukuma pia zile nyama zinakuwa zinasinyaa na kuisha kabisa.

Asilimia kubwa ya kila mwanamke kwanzia umri wa miaka 22 ambaye yupo katika uhusiano wa muda mrefu na mpenziye na mpaka kwenye ndoa hawana hizi nyama kutokana na mizunguko ya mara kwa mara na baadaye kuzaa, sasa wewe utakuta mtu kwa usiku mmoja anenda mara tatu au mara mbili ukifanya hivyo kwa wiki mara mbili kwa mwezi je na mwaka????? na ukizaa ndio kabisa ndio maana nimepata malamiko yawanawake wengi sana kwamba tokea wamezaa wanahisi wamekuwa wawazi ukeni na waume zao hawapati raha kabisa wanapofanya mzunguko hiyo ndio sababu kuu..

Utafanyaje kama mafuta ya ndimu utatumia mafuta ya vitunguu saumu ukeni lakini kumbukeni jamani kama unatumia mafuta ya kitunguu swaumu usichanganye na mengine basi kwasababu ushajuwa matumizi mchana upake hii usiku ile hapana usije jiletea matatizo baadaye kama unataka kukaza ukeni tumia mafuta haya ya vitunguu swaumu acha hayo mengine na kama wewe unaona uke umekaza unataka kusafisha tumia mafuta ya ndimu tu acha mengine.

Narudia USICHANGANYE mafuta mawili kwa siku moja ukeni.....

Ukitaka mafuta haya nipigie ni  10,000/=

Chezea mafuta ya ndimu weye..

Jamani wanawake woote mliofika siku ya kufundwa hongereni sana yani manajuwa na kujiamini kwamba nyie ni wanawake na mnatakiwa muwaje kuwa ng'aring'ari siku zote na hayo ndio maisha mwanamke ujipe raha mwenyewe bwana mengine yote yatafata baadaye.

Wliokuja ijumaa wanakumbuka walifundwa kuhusu mafuta na matumizi yake chumbani kulikuwa na mafuta ya kila aina leo nitaweka mafuta matatu tu na ndio mwisho kwa yeyote anayetaka kujuwa basi asubiri tukifunda tena ndio aje asidandie gurudumu la wenzao.

Mafuta ya ndimu katika mwili wa mwanamke husaidia kuusafisha uke na kutoa bacteria zote zilizopo mule, namaanisha nini wanawake sisi huwa ukeni kunapitia mambo mengi sana ukiacha uume tuna bleed, huwa tunajifukiza huko, tunatumia sijui madawa gani ya kuoshea huko yani vurugu kibao na haswa haya madawa tunayonawia huko huwa yanamadhara sana ndio maana mimi na kungwi wangu tunashauri kutumia vitu vy aasili ambavyo havina chemical.

Mafuta ya ndimu ni mazuri sana katika kusafishia huko ukeni utafanyaje ukishamaliza kuoga na kutawaza ukeni utachukuwa gozi utovye katika yale mafuta yako ya ndimu na kulitumbukiza gozi ukeni ukisafisha taratibu katika kila kuta uhakikishe umesafisha vizuri kabisa toa gozi lako usinawe kwa maji vaa chupi yako endelea na kazi zako mpaka jioni ukiwa unaoga ndio upasafishe ulale ukiwa fresh baada ya kuoga jioni usipake tena kitu chochote kile lala hivyohivyo.

Endelea kutumia mafuta ya ndimu mara kwa mara utaona kama utalalamika mambo ya UTI na madhara mengine ya ukeni. kwa anayetaka mafuta haya anipigie simu chupa ni 10,000/= kwa waliokuja kufundwa waliuziwa kwa nusu bei ndio maana nashauri sana tukiwa tunafunda wanawake mjitokeze jamani na muwe waangalifu kwasababu nimeanza kufunda basi kila mtu nasikia na yeye anataka kufunda kuweni makini na mnapopeleka hela zenu na mtakachopata.


Tuesday, December 4, 2012

Hehe heiya chezea siye...

Unaambiwa MUNGU aliumba kufanya mzunguko starehe kwa kila binadamu sasa basi kwanini ulalamike unaumia, husikii raha, huna hamu ya kwenda mzunguko au ukienda wa kwanza hutaki kabisa kurudia!!!!! baassiii tatizo lako sasa limefikia mwisho tukutane ijumaa 7/12/2012 utafundwa cha kufanya na kupewa mafuta ya asili kwa kujirutubisha shoga ukikutana na mpenzi basi mambo ng'aring'ari utakuja kutuambia hapa.lipia nafasi yako sasa tumebaki na kesho tu..

Ndoa hizi......

Jamani kwanza mimi naamini mwanamke yeyote sio mpaka awezeshwe ndio ayaweze haya maisha unaweza ukahangaika mwenyewe juu chini kwa njia za halali na zinazompendeza MUNGU huku ukimuomba kwa roho ya ukweli atakuinua tu, sio njia za mkato ili upate jambo ndio ujisifie kwamba umetoka na upo juu hapana.

Ndoa tunazitaka na kuzililia lakini je mnajuwa ya kwamba sio kila anyeamua kukuoa ama kuolewa na wewe anakupenda wengine wanakuja na mipango yao moyoni wengine wanataka kutoa nuksi kwao kwahiyo wanaolewa tu na ndio maana hawajali hata wakiachika baada ya mwezi.

Kuna wanaume wengine wanaoa kisa wameona mwanamke yule kwao ni matajiri kwahiyo wanatafuta njia za mkato za kupata mafanikio.

Kuna dada mmoja ameolewa na mzungu na kiumri wamepishana sana huyu dada ni mdogo sana kwa mumewe na MUNGU aliwapa utajiri kwakeli huyu mumewe ana kampuni moja kubwa sana na wanabonge la jumba na magari tele yani ni mwanamke ambaye ukipishana naye unaanza kwanza kujiangalia mara mbili maana ananukia pesa na utajiri.

Sijui ni matatizo gani waliyokuwa nayo ndani ya ndoa maana kuta zinaficha mengi na niwao tu wenyewe wanajuwa naona mdada kachoka akaamua kwenda kumchomea jamaa uhamiaji jamaa akafukuzwa ndani ya hiyo nchi masaa 24 na sirudi tena humo.

Lakini kama ninanvyosema huwezi juwa walikuwa na matatizo gani kabla hajafukuzwa muda fulani nyuma kumbe yule jamaa alibadilisha mali zake na kuandika jina na mtu mwengine ambaye hata mkewe hamjui ambaye hata mkewe hamjui mpaka magari na kampuni.

Yule mwanamke ndio kuhaha sasa kampuni na mali hana na mume pia hana alidhani kapata kumbe kapatikana.

Jamani tuweni makini na ndoa hii sio fashion na sio lazima kwamba kila mwanamke au mwanaume atembee na pete za ndoa mkono wa kushoto kama unaona bado hujapata ubavu wako subiri atakuja na labda hamna kabisa usijilazimishie hata kwenye bibilia imeandikwa kwamba kuna watu wataoa na kuolewa na wengine hawatakaa kuoa ama kuolewa labda na wewe ni mmoja wapo.

Kuwa na uhakika kwanza kabla hujamkubalia huyo unayetaka kumuoa/kuolewa naye.

Monday, December 3, 2012

Hehe heiya...Huku kazi tu

Ladies zimebaki siku tatu tumfichue mwali...hehe heiya ni ijumaa hii 7/12/2012 umelipia nafasi yako..chezea siye weye 4x4x by far

TBC Oyeee....karibu kundini Grace

                                         Julius Kihampa na mkewe Grace Kingalame.


 Desemba 29, mwaka huu familia ya Grace iliangusha shughuli ya kumuaga (send off) mtangazaji huyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Mwenge Social, Dar es Salaam.

Cheers kwa maisha marefu ya ndoa, na yenye kujaa furaha na upendo wa kweli na MUNGU awabariki na kuwajazia meza yenu na izungukwe na watoto wakiume na wakike mfurahie maisha yenu kwa pamoja.